Sunday, February 2, 2020

Moshi Stampede: A black day in Kilimanjaro

Tukio la watu 20 kupoteza maisha katika tukio la kukanyagana mjini Moshi na wengine zaidi ya 16 kujeruhiwa katika ibada ya Utakaso iliyoendeshwa na Mtume na Nabii Boniface Mwamposa imeifanya Februari Mosi, 2020 kuwa siku mbaya kuwahi kutokea mjini humo katika historia yake. 

Huduma ya Arise and Shine au Inuka na Uangaze inayosimamiwa na Mwamposa maarufu Bulldozer imeweka doa katika mji wa Moshi kutokana na kitendo cha watu hao kupoteza maisha wakati wakiwania kukanyaga mafuta kwa ajili ya uponyaji wao.

Watu zaidi ya 4,500 walihudhuria ibada hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Majengo mjini humo ambapo

Kwanini iwe "Black day in Kilimanjaro"  kwa ufupi nianishe kupitia maneno haya; 

"February 1, 2020: At least 20 people died and 16 injured in stampede at a church in Moshi, Kilimanjaro in Tanzania. The incident took place when church faithful were being ushered through an exit so that they could walk on “anointed oil.” More than 4,500 worshipers were attending a prayer meeting led by Boniface Mwamposa, a popular preacher who leads the Arise and Shine Ministry Tanzania."

Maneno hayo niliyatupia katika Kamusi huru ya Mtandaoni ya Wikipedia katika article hii "List of human stampedes and crushes."

Haifurahishi kuona ndugu, jamaa na marafiki wakipoteza maisha kwa mara moja katika matukio kama hayo ya kanisani. 

Kwani kila mmoja anafahamu kuwa kanisani ni mahali pa amani ambapo uponyaji wa mtu upo. Inapotokea tukio kama hilo lazima kila mmoja ashike kichwa chake. 

Hata hivyo ningependa kuangazia matukio kadhaa yaliyowahi kutokea katika makanisa na kusababisha vifo.

Desemba 28, 2018

Nchini Afrika Kusini watu watatu walipoteza maisha kwa tukio la kukanyagana katika Kanisa la Nabii Shepherd Bushiri la Enlightened Christian Gathering. Bushiri alishawahi kufika mjini Moshi katika huduma ya ECG kwa mchungaji mwenzake Pastor Ikera mwaka 2019 ambapo alipokelewa kwa nguvu kubwa. Mchango huu niliuchangia katika kamusi huru ya Wikipedia 

"28 December 2018: The three lost their lives when an apparent stampede broke out at Bushiri’s Enlightened Christian Gathering Church. Police confirmed the identity of the three women killed in a stampede at controversial prophet Shepherd Bushiri’s church in Pretoria. Preliminary reports indicate that the community assembled at the show grounds to attend Shepherd Bushiri’s church service, when the rain started, the congregation started to push each other and the stampede occurred."

Itaendelea....

Imetayarishwa na Jabir Johnson..........................Februari 2, 2020.

0 Comments:

Post a Comment