Friday, February 14, 2020

Ifahamu Valentine Day

......Wakristo walianza kuteswa na Dola la Rumi tangu wakati wa Nero mnamo mwaka 64 B.K hadi mwaka 313 B.K wakati wa utawala wa Constatine  I na Licinius ambao waliufanya ukristo kuwa dini halali katika dola hilo......

Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka Dola ya Warumi. Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi.

Sababu ya kutetea waumini wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu. Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku ya mapenzi kinyume cha dhamira ya Mt. Valentine.

Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa, ili wawe huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi.

Wakioa hawangekuwa na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao. Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.

Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu.

Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu wachache), alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka amri ya wakuu wa dola ya kirumi.

Baadhi ya watu walifichua siri hiyo, hivyo Padre Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.

Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa. Ikaenea katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka Mt. Padre Valentin.

Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama mtetezi wa Ndoa.

Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa bali mradi wanapendana, kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt. Padre Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawala tu (vimada).

Mfia dini huyu Valentine alifariki dunia Februari 14, 269 B.K jijini Rome akiwa na umri wa miaka 43.

Wakristo walianza kuteswa na Dola la Rumi tangu wakati wa Nero mnamo mwaka 64 B.K hadi mwaka 313 B.K wakati wa utawala wa Constatine  I na Licinius ambao waliufanya ukristo kuwa dini halali katika dola hilo. 

Ukristo wa Mashariki hususani wa ORTHDOX husherekea siku hii Julai 6 na Julai 30. Makanisa ya Romani, Anglikana na Lutherani yaliiteua siku yake ya kufariki kuwa siku muhimu ya kumkumbuka mfia dini huyu.

0 Comments:

Post a Comment