Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Elisha Osati amesema changamoto kubwa inayowakabili madaktari ni tabia ya baadhi ya viongozi na wanasiasa kuagiza wataalam wa afya wanaofanya kosa la kitaalam kuwekwa ndani.
Dk Osati alisema hayo jana Alhamisi Februari 20, 2020 katika mkutano wa madaktari na watumishi wa sekta ya afya unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Alisema sheria inayowapa mamlaka viongozi wa Wilaya na Mikoa kuwaweka watu ndani masaa 48 imekuwa mwiba kwa taaluma ya utabibu.
“Kumekuwa na tabia ya viongozi wa kisiasa kwenda hospitali na kukuta kosa limefanyika, anapokuja kiongozi mkuu wa wilaya, mkoa na viongozi wengine wa kisiasa akisema weka ndani daktari, mfamasia au nesi hatudhni kuwa inatutendea sawa,” alisema Dkt. Osati.
Amesema katika changamoto wanazozipata katika kazi zao hiyo ni kubwa.“Katika changamoto tunayoipata kwenye taaluma, hii ni kubwa kwa sababu inatuondolea heshima ya taaluma,” aliongeza.
CHANZO: Mwananchi
0 Comments:
Post a Comment