Februari 13, 2013 alifariki dunia mbunifu wa mavazi na mitindo na mwanasheria wa Afrika Kusini Reeva SteenKamp.
Usiku wa kuamkia Februari 14, 2013 Reeva Steenkamp aliuawa na rafiki yake wa kiume na mwanariadha Oscar Pistorius.
Mwanadada huyo alitandikwa risasi mara nne kupitia katika mlango wa chooni alipokwenda kumsalimia rafiki yake huyo.
Mwili wa mwanadada huyo ulifanyiwa sala zya mwisho mjini Port Elizabeth Februari 19, 2013 na ibada ya mazishi iliongozwa na Mchungaji Kurt Sutton wa Kanisa la Oasisi Family.
Pistorius alikamatwa na polisi kwa tukio hilo na aalikubali kuwa alitandika risasi kwani alidhani kuna mvamizi alikuwa akiingia katika nyumba yake.
Septemba 12, 2014 mahakama haikumkuta na hatia ya mauaji isipokuwa alikutwa na mauaji ya kutokusudia. Mahakama ilimhukumu Pistorius kwenda jela miaka mitano lakini mwanariadha huyo alitumikia miezi 10 tu.
Desemba 2015 mahakama ya rufaa nchini Afrika Kusini ilimkuta na hatia ya mauaji.
Julai 6, 2016 Jaji Masipa alimhukumu Pistorius miaka sita jela licha ya kuwa na sheria ambayo kwa makosa kama hayo ni kifungo kisichopungua miaka 15.
Novemba 24, 2017 Mahakama ya Rufaa iliongeza kifungo hicho hadi miaka 13 na miezi 13 jela kwa mwanariadha huyo.
Enzi za uhai wake aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchezaji wa raga wa klabu ya Springbok Francois Hougaard kabla hajaingia katika penzi na mwanariadha wa Palalimpiki Pistorius mnamo Novemba 2012.
Akiwa na miaka 20 aliwahi kuvunjika mgongo wakati akiendesha farasi hivyo alijifunza kuanza kutembea tena.
Steenkamp alikuwa mtu wa watu nchini Afrika Kusini akionekana katika matamasha mbalimbali ya mavazi, mitindo na utoaji jijini Johannesburg.
Pia alikuwa mtangazaji katika FashionTV katika masuala ya mavazi na mitindo. Alionekana katika bidhaa za makampuni ya magari kama Toyota Land Cruiser, Clover "The One", Redds na Aldor Pin Pop
Katika medani ya mavazi, mitindo na fasheni kwa ujumla wake Steenkamp alianza akiwa na umri wa miaka 14.
Steenkamp alikuwa akifanya kazi kama mwanasheria wa kujitegemea na alikuwa na matumaini kuwa atakafikisha umri wa miaka 30 angeweza kuwa wakili kamili wa sheria.
Alizaliwa Cape Town kwa wazazi Barry Steenkamp ambaye alikuwa mwalimu wa farasi na mkewe wa pili June Marshall mzaliwa wa Blackburn, England.
Baada ya maisha ya hapo Cape Town familia hiyo ilihamia Port Elizabeth ambako Reeva Steenkamp alianza kusoma huko Shule ya Mtakatifu Dominic.
Baada ya hapo alikwenda kusoma Chuo Kikuu cha Port Elizabeth ambacho baadaye kilikuja kuwa tawi la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela. Steenkamp alihitimu shahada ya sheria chuoni hapo mnamo mwaka 2005.
Steenkamp alizaliwa Agosti 19, 1983
Steenkamp alizaliwa Agosti 19, 1983
0 Comments:
Post a Comment