Februari 18, 1546 alifariki dunia msomi,mwanazuoni, mchungaji, mtunzi wa nyimbo na mtumishi wa Kanisa wa Kijerumani Martin Luther ambaye anachukuliwa kuwa kiungo muhimu katika kuanzisha Uprotestanti barani Ulaya.
Luther alifariki dunia kutokana na kuugua muda mrefu maradhi makuu yaliyokuwa yakimsumbua yakiwamo kuumwa sikio ambapo alikuwa akihisi kama kuna vitu vinazunguka kumbe sivyo kitaalamu unajulikana kama Meniere, pia alikua akizimia, kushindwa kuona vizuri, Kutoka mwaka 1531 hadi 1546 hali yake ya kiafya ilikuwa mbaya.
Inaelezwa kuwa hali yake ya afya ilizidi kuwa mbaya kutokana na kashfa ambayo iliwakumba wenzake. Pia kashfa ya kutaka kuharibu ndoa ya Phillip I, Landgrave of Hesse kwamba hayo yote yalichangia kwa kiasi kikubwa.
Mnamo mwaka 1536 Luther alianza kuugua maradhi ya figo, kibofu kujaa mawe, jointi kuvimba, sikio kuuma hali iliyosababisha kuharibi ngoma ya sikio.
Manmo Desemba 1544 alianza kuhisi maumivu ya kifua ambayo kitaalamu hufahamika kwa jina la angina ambayo yanatokana na damu kushindwa kufika vizuri.
Luther alikuwa akichukuliwa kuwa kiungo muhimu katika kutoa changamoto katika Ukristo wa Magharibi katika karne ya 16 barani Ulaya.
Changamoto hiyo ilisababisha masuala ya dini na siasa kwa kanisa la Roman Katoliki kuwa katika wakati mgumu pia mamlaka ya Papa katika kanisa Katoliki yalikuwa katika changamoto hiyo.
Luther alichapisha mawazo yake 95 mnamo mwaka 1517 na kupitia hapo ndipo mtafaruku ulipozidi katika kisiasa na kidini katika Kanisa la Roman Katoliki.
Licha ya Luther kutoa chapiso lake hilo lenye mambo 95 lakini hakuwa ameligawa kanisa Katoliki hadi ilipofika mwaka 1521 wakati ambao mtawala wa Dola ya Rumi Charles V alipotangaza kwamba Luther achukuliwe kama mkaidi na msaliti na asiwepo yeyote wa kufuata aliyoyaandika.
Kwa kuanza Charles V alitangaza kufuta uraia wake katika dola la Rumi.
Mkutano huo ulifanyika katika Bustani ya Heylshof kwenye mji wa Worms ambao upo umbali wa kilometa 60 Kusini-Kusini Magharibi ya Frankfurt na baadaye katika miji mingine iliyokuwa ikijitawala katika dola la Rumi.
Charles V aliendesha mkutano huo kumhusu Luther na matokeo ya kuibuka kwa Uprotestanti barani Ulaya kutoka Januari 28 hadi Mei 25 mwaka 1521.
Mara baada ya kipindi hiki cha mabadiliko kilifuata kipindi kingine ambacho kilitoa mwanya kwa Waorthodoksi kustawi barani Ulaya.
Alizaliwa Novemba 10, 1483 huko Eisleben, nchini Ujerumani wakati huo ikiwa katika dola la Kirumi. Luther aliingia katika utumishi wa Kanisa mnamo mwaka 1507.
Akiwa na kanisa la Roman Katoliki alipinga mafundisho mbalimbali ya kanisa hilo pia adhabu zilizokuwa zikitolewa kwa yeyote aliyekuwa akitenda dhambi.
Luther alifundisha kwamba wokovu haupatikani kwasababu ya matendo mema lakini unapatikana kwa neema ya Mungu ikiwa ni zawadi lakini zawadi hiyo ni sharti uwe unamwamini Yesu Kristo kuwa mkombozi kutoka katika dhambi.
Mafundisho hayo ya kitheolojiwa yalipeleka changamoto kwenye mamlaka za dola la Rumi na Ofisi ya Papa kuwa Luther anafundisha kuwa Biblia ni chanzo pekee cha maarifa ya kiroho.
Pia mafundisho yake Luther yalikwenda mezani kwa Papa kuwa wachungaji na watumishi wa Mungu ndio daraja la mwamini kuunganishwa na Mungu, yeye alikuwa akidai kuwa wakristo wote waliobatizwa ni wa ukuhani mtakatifu.
0 Comments:
Post a Comment