Mradi wa uchafushaji nyuki katika Chuo cha Uhifadhi wa Wanyamapori (MWEKA) umetajwa kuwa ni muhimu kwa kukuza uchumi wa nchi hadi katika sekta ya kilimo.
Hayo yalisemwa na Profesa wa Chuo kikuu cha kilimo Sokoine Brayson Rwegasila, wakati wa kikao cha kutazama mwenendo wa uchafushaji nyuki unaoendelea katika chuo hicho wenye lengo la kubaini idadi ya aina ya nyuki waliopo Tanzania na changamoto wanazopata wadudu hao.
“Tunajua nyuki wamekuwa wakifanya kazi za kuchavusha mazao, kisha kile chakula tunachokipata kila siku kinatokana na nyuki wanaochavusha mazao, lakini hakuna aliyewahi kuwa na wazo la kuangalia kwamba kwa mfano katika nchi yetu tuna nyuki aina zipi, wanafanya shughuli gani, wanaathiriwa na nini,”alisema Prof. Rwegasila.
Alisema lengo la warsha hiyo ni kuangalia juhudi za watafiti wa chuo cha Mweka katika kujaribu kuangazia walau kazi ambazo zinafanywa na hao wadudu, ambao ni viumbe wadogo lakini shughuli yake ni kubwa na kwammba bila ya nyuki kufanya kazi zao kwa pamoja chakula ambacho tunakipata kila siku hakiwezi kuwepo.
Nae Mtafiti na Mhadhiri msaidizi wa Chuo Cha Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Wanyamapori Mweka Julias Laswai, alisema kuwa licha ya mradi huo kuwa wa muhimu bado jamii ya Watanzania hawajapata uelewa wa kufahamu umuhimu wa mdudu nyuki hasa katika ushiriki wake wa kuchavusha mazao.
“Kwenye maeneo ambayo tunafanya tafiti, watu wengi hawajui umuhimu wa hao nyuki, wengi wao wanaelewa nyuki umuhimu wake ni kutoa zao la asali pekee, na mazao mengine kama vile nta, lakini suala la nyuki anafanya uchafushaji hawana uelewa na suala hilo,”alisema.
Aliongeza kusema kuwa changamoto nyingine waliyoibaini ni matumizi ya viuatilifu vya kilimo vinavyopelekea kuwaua kwa nyuki hao na kuharibu shughuli zao za uchavushaji jambo linalohitaji kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa kwani kuna uwezekano mkubwa wa kuwakosa nyuki muhimu siku za usoni.
”Changamoto kubwa ya maeoeo mbalimbali yakitafiti tumekuta matumizi makubwa ya kilimo cha aina moja, tumegundua kwamba kinachosababisha kupata nyuki kidogo ni matumizi ya viuatilifu za kemikali, unakuta wakulima wanahitaji kutumia viuatilifu kupunguza hali ambayo inasababisha kuuawa wadudu hao ambao ni wachafushaji,”alisema.
Aidha Mhadhiri huyo alisema kuwa kundi la nyuki limegawanyika katika sehemu kuu tatu kiutendaji, Malkia Nyuki vibarua (nyuki majike) na Nyuki madume, kawaida kwenye mzinga nyuki vibarua huwa wengi zaidi hufikia hadi 60,000, hii ni tofauti sana na nyuki madume ambao wao huwa ni wachache sana.
Laswai alisema kila kundi kati ya hayo yana kazi yake, ambapo alisema kundi la malkia, kazi yake ni kutaga mayai na kawaida yeye hulelewa kama mtoto kwa maana yeye analishwa mdawote, Malkia anaweza kutaga mayai 1,500 hadi 2,000 kwa siku.
Alifafanua kuwa kazi kubwa za nyuki madume ni kumpanda malkia na anapompanda malkia tu, huwa dume anakufa, kawaida malkia hupandwa na madume saba na baada ya hapo huendelea kutaga mpaka mwisho wa maisha yake.
STORY BY: Kija Elias, Moshi..........................Februari 14, 2020
0 Comments:
Post a Comment