Friday, February 14, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA:Rafiq Hariri ni nani?

Februari 14, 2005 alifariki dunia mfanyabiashara mkubwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri. 

Rafiq Hariri alishika wadhifa huo wa juu katika taifa la Lebanon mara mbili mnamo mwaka 1992 hadi 1998 na mwaka 2000 hadi alipojiuzulu Oktoba 20, 2004.

Wakati wa utawala wake alikuwa na mabaraza matano tu ya mawaziri. Anakumbukwa sana kutokana na namna alivyoweza kuhusika katika kumaliza mgogoro wa vita vya wenyewe kupitia Makubaliano ya Taif ambayo yalifikiwa nchini Saudia Arabia katika mji wa Taif.

Hariri aliuawa kwa kutegewa bomu katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Wafuasi wanne wa Hezbollah walikamatwa kwa kuhusika na tukio hilo na walipelekwa katika mahakama maalum ya makosa ya uhalifu wa kivita ya Lebanon.

Wengi walihisi kuwa kifo cha Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Lebanon kilihusishwa na maofisa wa serikali ya Syria.

Mauaji ya Hariri yalikuwa kionjo muhimu cha mabadiliko ya kisiasa katika taifa la Lebanon. 

Maandamano makubwa yalifanyika katika taifa hilo kushinikiza kuondolewa kwa majeshi ya Syria nchini humo na mabadiliko ya serikali ya Lebanon kwa ujumla.

Hariri aljiingiza katika siasa za Lebanon katika miaka ya mwanzo ya 1980 akiwa mtu tajiri na alianza kujijenga mwenyewe kwa kuwa mchangiaji mkubwa katika makundi mbalimbali nchini humo.

Pia aliendelea kuwa mshauri mkuu wa kisiasa wa Prince Bandar bin Sultan mnamo mwaka 1983.

Kama haitoshi aliendelea kuwa mtu mwenye nguvu ambaye alikuwa upande wa Saudi Arabia baada ya kuanguka kwa PLO na uongozi wa Kisunni katika taifa hilo na kupanda kwa Washia katika ngazi za kijeshi. 

Hariri akiwa mjumbe wa kidplomasia wa Saudi Arabia alihusika kwa kiasi kikubwa kutengeneza Makubaliano ya Taif ambayo yalihitimisha safari ya miaka 16 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Mnamo mwaka 1992  Hariri alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe chini ya Rais Elias Hrawi.

Hariri aliirudisha nchi hiyo katika ramani ya kiuchumi kupitia kuruhusu matumizi ya Benki ya Dunia kufadhili fedha kwa ajili ya ujenzi wa taifa hilo hivyo hatua hiyo iliipandisha Lebanon tena. 

Mnamo mwaka 1998 Hariri aliishia hapo na Waziri Mkuu wa pili baada ya zama za Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe Salim Hoss. 

Ukweli ni kwamba mgongano wa kimadaraka baina yake ya Rais Emil Lahoud ambaye alikuwa ametoka kuchukua wadhifa huo ndio kulikosababisha asiendelee na nafasi hiyo.

Mnamo Oktoba 2000 aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu na kuchukua madaraka Salim Hoss na Hariri aliunda baraza la mawaziri.

Septemba 2004, Hariri aliyataka majeshi ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kuondoa majeshi yote yaliyobaki nchini humo.

Oktoba 20, 2004 katika kipindi chake cha pili alijiuzulu wadhifa huo na nafasi yake ilichukuliwa na Omar Karami.

Kutoka mwaka 1982 hadi kifo chake Hariri alikuwa akimiliki mojawapo ya jumba kubwa la thamani jijini London maeneo ya Rutland Gate , Knightsbridge.

Jumba hilo alizawadiwa Crown Prince wa Saudia Arabia Sultan bin Abdulaziz

Enzi za utawala wake anachukuliwa kuwa hakufanikiwa kudhibiti rushwa katika Lebanon hususani wakati wa ukaliaji kimabavu wa Syria katika ardhi hiyo.

Inaonyesha kuwa wakati akiteuliwa kuwa Waziri Mkuu kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1992 utajiri wake ulikuwa sio chini ya dola za kimarekani bilioni moja.

Lakini hadi kifo chake ulipaa hadi kufikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 16.

Katika maisha yake binafsi Hariri alioa mara mbili. Alizaa watoto saba. Mnamo mwaka 1965 Hariri alimwoa mwanamke wa Kiiraki Nidal Bustani ambaye alimzalia watoto watatu Bahaa (1967) ambaye ni mfanyabiashara;  Saad ambaye amefuata nyayo za baba yake kwa kuwa mwanasiasa na alimzalia Hossam ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari nchini Marekani miaka ya mwishoni ya 1980. 

Baada ya hapo waliachana na akamwoa mwanamke mwingine ambaye ni Nazik Audi mnamo mwaka 1976 ambaye alimzalia watoto wanne akiwamo Ayman Hariri, Fahd Hariri na Hind Hariri.

Hariri alizaliwa Novemba 1, 1944 kutoka katika familia ya kiislamu ya Kisunni katika mji wa baharini wa Sidon. 

Alikuwa na ndugu zake wengine wawili waliozaliwa katika familia hiyo Shafic na dada yake aliyefahamika kwa jina la Bahia.

Alisoma shule ya chekechea na Msingi hapo hapo Sidon pia Sekondari. Shahada ya Utawala wa Biashara aliichukua katika Chuo Kikuu cha Kiarabu cha Beirut.

0 Comments:

Post a Comment