Friday, February 7, 2020

Unakumbuka George Best alichowafanya Northampton mwaka1970?

Februari 7, 1970 mshambuliaji machachari wa Manchester United George Best aliweka rekodi muhimu katika michuano ya Kombe la FA nchini England kwa kutupia mabao sita kwenye mzunguko wa tano wa mashindano hayo dhidi ya timu ya daraja la nne ya Northampton Town. 

Katika mchezo huo Manchester United ilishinda kwa mabao 8-2. George Best alifunga mabao hayo akitoka kumalizia kifungo cha majuma manne kwa kitendo cha kuupiga mpira ukiwa mikononi mwa mikono ya mwamuzi mwanzoni mwa msimu huo. 

Kwa mujibu wa maelezo ya mlinda mlango wa Northampton Kim Book aliwahi kusema kuwa kocha wa timu yao wakati huo Dave Bowen hakuwahi kufikiri kuwa Best atakuwamo katika mchezo huo na wala hakuwahi kumtaja kama ni mchezaji hatari kwenye mechi hiyo katika maandalizi ya mwanzo kuelekea mchezo huo dhidi ya Manchester United. 

Baada ya mchezo huo gazeti la Mirror la nchini Uingereza liliandika, " Best destroyed them as completely as one man can destroy others without inflicting physical damage," noting that the six goals "came from the full range of his ability. " 

Kwamba Best amewamaliza kabisa kama vile mtu anavyoweza kuwaharibu wengine bila kuonyesha majeraha mwili na mabao sita aliyofunga ni kutokana na uwezo wake.

Hata hivyo bao lake la sita kwenye mchezo huo lililowaweka mbele Manchester United kwa mabao 7-1 lilikuwa kali kwani Best aliukokota mpira na kumfuata mlinda mlango wa Northampton kisha kumdanganya kama anapiga upande mwingine kisha akauminya ule mpira na kuunyanyua kidogo juu ya bega kisha kuusukumiza nyavuni. 

Hata hivyo mwishoni mwa mchezo huo mashabiki wa Northampton Town walikuwa wakimpigia makofi George Best kutokana na kiwango chake alichokionyesha katika mchezo huo. 

Aidha katika michuano hiyo Mashetani wekundi waliendelea katika mzunguko wa sita ambako waliizabua Middlesbrough kwa mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano. 

Katika nusu fainali Manchester United ilitupwa nje na Leeds United kwa uwiano wa bao 1-0 baada ya mchezo wa marudiano kutoka sare tasa.

0 Comments:

Post a Comment