Tuesday, February 4, 2020

Wanafunzi 14 wafariki dunia katika mkanyagano Magharibi mwa Kenya





Polisi wa Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio la kukanyagana lililotokea kwenye shule ya msingi magharibi mwa Kenya ambalo lilisababisha vifo vya wanafunzi 14 na wengine 38 kujeruhiwa.

Kamanda wa polisi David Kabena amesema tukio hili lilitokea kwenye shule ya msingi ya Kakamega saa 11 jioni Februari 3, ambapo wanafunzi wengi walikimbia nje ya madarasa.

Kabena amesema tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi wa darasa la 5 lililoko kwenye ghorofa ya 3 ya jengo la shule walipoondoka.

Wanafunzi 13 ambao wengi walianguka kwenye ngazi na kufariki papo hapo, na wengine 39 walipelekwa hospitali, mmoja akafariki baadaye, na wengine wanne walijeruhiwa vibaya.

Wanafunzi 20 wametoka hospitali baada ya kutibiwa.

Inaelezwa kuwa mwalimu mmoja alipojaribu kumwadhibu mwanafunzi, wanafunzi wengine walikimbia nje na kwenye kukimbia huko baadhi walianguka kwenye ngazi na kukanyagwa.


0 Comments:

Post a Comment