Friday, February 21, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Billy Graham ni nani?

Februari 21, 2018 alifariki dunia mwinjilisti wa Kimarekani Billy Graham. 

Alifariki dunia kutokana na uzee. Graham anasalia kuwa nembo ya kikristo katika huduma ya Uinjilisti na mtu aliyejitoa kikamilifu kusambaza neno la Mungu chini ya mwavuli wa Kanisa la Kibaptisti ambao unashika nafasi ya pili kwa kuwa na waamini wengi nchini Marekani.
  
Alianza kufahamika zaidi kimataifa tangu mwaka 1940 hadi alipostaafu mnamo mwaka 2005.

Mojawapo ya biographers wanamchukuliwa kuwa ni miongoni mwa Viongozi wa Kikristo waliokuwa na ushawishi kwa karne ya 20.

Wakati wa Mazishi yake Rais wa Marekani Donald Trump alisema Graham alikuwa Balozi wa Kristo. 

Mwinjilisti mwingine wa Kimataifa zamani akiwa na Assembiles of God nchini Marekani Jim Bakker alitoa heshima zake na kusema Graham alikuwa  mhubiri mkubwa tangu Yesu alipoondoka dunia. 

Pia Bakker aliongeza kuwa Graham alimtembelea alipokuwa jela miaka ile ya 1970. Graham alizikwa pembeni ya kaburi la mkewe  katika Upande wa Kaskazini Mashariki mwa Maktaba ya Billy Graham huko Prayer Garden, Montreat, North Carolina.

Graham alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 99 akiwa ameacha watoto watano, wajukuu 19 wakiwamo Graham na Tullian Tchividjian na vitukuu 41 na vilembwe sita

Graham alizaliwa Novemba 7, 1918 katika ghorofa ya chini katika nyumba ya kulala huko mashambani karibu na Charlotte, North Carolina. 

Mhubiri huyo alizaliwa katika kizazi henye asili ya Uskochi na Ireland na alikuwa mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Morrow na William Franklin Graham Sr. ambaye alikuwa mkulima na mfugaji. 

Grahama alikulia huko huko mashambani akiwa na ndugu zake Catherine Morrow, Jean na Melvin Thomas. Akiwa na umri wa miaka minane (8) mnamo mwaka 1927 familia ilihama kutoka katika nyumba ya mbao na kuhamia kwenye nyumba ya matofali ya kuchoma. 

Wazazi wake walikuwa ni waumini wa Kanisa la Associate Reformed Presbyterian.

Graham alianza kusoma katika shule ya Sharon Grammar ambako alianza kusoma vitabu tangu akiwa mdogo na alipendelea zaidi kusoma riwaya hususani  ya Tarzan. 

Alivyokuwa Tarzan naye Graham alikuwa akipendelea kukaa juu ya miti na kuwapigia kelele farasi na madereva. Kwa mujibu wa baba yake, alisema kitendo hicho kilimaanisha kuwa angekuja kuwa mtumishi wa Mungu. 

Alipokuwa na umri wa miaka 14 wakati ambapo katazo la matumizi ya vinywaji vyenye kileo lilipomalizika mnamo Desemba 1933 ; baba yake aliwalazimisha Graham na dada yake Katherine wanywe bia hadi wawe wagonjwa. Kitendo hicho kiliwafanya Graham na dada yake waachane na vileo katika maisha yao yote.

Agosti 13, 1943 Graham alimwoa Ruth Bell ambaye walisoma naye darasa moja huko Wheaton, Ruth alikuwa na wazazi waliokuwa wakifanya kazi ya umishionari nchini China chini ya mwavuli wa Presbyterian. 

Baba yake Ruth alikuwa Daktari Mkuu wa Upasuaji. Mkewe huyo alifariki dunia Juni 14, 2007 akiwa na umri wa miaka 87. Wawili hao walikuwa wamekaa katika maisha ya ndoa kwa takribani miaka 64.

Graham na mkewe walifanikiwa kuzaa watoto watano ambao ni Virginia Leftwich (Gigi) Graham (waliyemzaa mwaka 1945), ambaye ni mwandishi wa vitabu na mtoa hotuba za kuhamasisha; Anne Graham Lotz (waliyemzaa mwaka 1948), anaendelea kusimamia Huduma ya AnGeL; Ruth Graham (waliyemzaa mwaka 1950), huyu ni mwanzilishi na Rais wa Ruth Graham & Friend ambapo huongoza makongamano mbalimbali kati ya Marekani na Canada.

Pia walimzaa Franklin Graham (mwaka  1952), kwa sasa anahudumu kama Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Billy Graham Evangelistic Association. Franklin ni Rais na Mkurugenzi Mtendaji International Relief Organization, na Samaritan's Purse

Na mtoto wa mwisho ni Nelson Edman Graham (waliyemzaa mwaka  1958), ambaye ni Mchungaji anayeendesha huduma ya East Gates Ministries International, ambayo hufanya huduma yake kwa kupeleka vitabu vya Kikristo chini China.

Mnamo mwaka 1950 Graham alifungua huduma ya Billy Graham Evangelistic (BGEA) makao yake makuu yakiwekwa Minneapolis. 

Huduma hiyo ilizidi kukua akafungua pia Charlotte na Noth Calorin mnamo mwaka 1999. Mnamo Aprili 2013 Huduma ya BGEA  ilianzisha 'My Hope with Billy Graham' ikiwa na maana ya kuwahamasisha watu wasambaze Injili. " 

Wazo ni hili kwa Wakristo kufuata mfano wa Mwanafunzi wa Yesu Mathayo katika Agano Jipya na kueneza habari njema katika nyumba zao," alisema Graham.

Mwanzoni mwa miaka yake ya Uinjilisti, Graham alikuwa akifanya mikutano yake ya Injili kwa kubagua lakini alianza kubadilika kadri siku zilivyokuwa  zikiendelea. Aliwapendelea zaidi wazungu. 

Mnamo mwaka 1953 aliondoa kamba zote katika mikutano yake huko Chattanooga, Tennessee ambazo zilikuwa zimewekwa kuwatenga watu kutokana na rangi zao. 

Aliwaambia wazungu wenzake, " Tumekuwa tukijisifu na kufikiri kuwa sisi ni bora  zaidi kuliko wengine. Ndugu zangu tutakwenda Jehanamu kwasababu ya kibu chetu."

Mnamo mwaka 1957 Graham alianza kuonyesha kwa nguvu zaidi ubaguzi wa rangi sio kitu cha kukumbatia pale alipowaruhusu watumishi Thomas Kilgore na Gardner C. Taylor  kuwa miongoni mwa waratibu wa Kamati ya Mkutano Mkubwa wa Injili wa New York.

Haikutosha alimwalika Mchungaji Martin Luther King Jr. katika mkutano wake ambaye aliweka rekodi ya kuwa wa kwanza baada ya mgomo wa Montgomery mnamo mwaka 1955.

Alimwalika Martin Luther King Jr. kwa siku 16 zote alizokuwapo jijini New York kwenye mkutano huo ambapo watu milioni 2.3 walihudhuria katika viunga vya Madison Square, Uwanja wa Yankee na viunga vya Times Square kwa ajili ya kumsikiliza.

Graham aliwahi kusema katika maandiko yake kuwa Martin Luther King Jr alikuwa rafiki yake wa karibu mno na yeye alikuwa miongoni mwa watu wachache waliokuwa wakimwita 'Mike' kwani ndio jina pekee ambalo Martin Luther King Jr. aliwaambia watu wake wa karibu wawe wanamwita.

Hata baada ya mauaji ya Martin Luther King Jr. mnamo mwaka 1968 Graham alimlilia sana mwanaharakati huyo  na kwamba Marekani imepoteza kiongozi wa kijamii na nabii.

0 Comments:

Post a Comment