Thursday, February 13, 2020

Hatimaye Moi azikwa Kabarak, Nakuru

Mwili wa aliyekuwa rais wa pili wa taifa la Kenya, Daniel arap Moi, umezikwa kwenye shamba la Kabarak, katika mji wa Nakuru, ambapo mwanaye alikabidhiwa ‘kirungu' chake kama ishara ya kuendelezwa uongozi wa familia.

Viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta wamemkumbuka Rais Moikama mtu mkarimu, mpenda amani na kiongozi shupavu, huku wanachama wa KANU, chama ambacho alikitumia kama tiketi yake ya uongozi, kikitangaza siku 40 za maombolezi kwa wanachama wake.

Rais Uhuru Kenyatta aliwavunja mbavu waombolezaji katika hafla ya kumzika kiongozi wa pili wa taifa, hayati Rais Daniel arap Moi, alipozungumzia wakati mmoja alipoamriwa na Rais Moi kusafiri kutoka Nairobi hadi Nakuru kwa chini ya saa moja kufuatia kosa alilofanya. 

Rais Uhuru amemuomboleza Rais Moi kama kiongozi muadilifu na ambaye uongozi wake utaenziwa. Alitumia fursa hiyo kuzindua tena mradi wa hospitali ya Kabarak uliokuwa mradi wa mwisho wa hayati Rais Moi
CHANZO: DW

0 Comments:

Post a Comment