Tuesday, February 25, 2020

Unaikumbuka Liverpool iliyotwaa Kombe la Ligi 2001?

February 25, 2001 katika Kombe la Ligi nchini England Liverpool na Birmingham City zilikutana katika fainali kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Millenium jijini Cardiff.

Fainali hiyo ilikuwa ikiweka rekodi ya kuwa fainali ya 41 ya michuano hiyo  ambayo hushirikisha timu 92 zikiwamo za Ligi Kuu na zile za madaraja ya chini.

Liverpool ambao waliibuka mabingwa katika fainali hizo walikuwa wakiingia katika fainali ya nane wakiwa wameshinda sita na kuzikosa mbili. 

Wakati Birmingham ilikuwa ni fainali yake ya pili ya Kombe la Ligi. Katika fainali yake ya kwanza ambayo ilikuwa mwaka 1963 ambayo walipoteza mbele ya Aston Villa.

Birmingham walikuwa tayari wameshacheza mizunguko miwili zaidi ya Liverpool ambao walikuwa wamecheza mzunguko wa kwanza na wa pili. 

Hivyo basi Birmingham ilisonga mbele ikiwa imecheza mizunguko sita kufika katika fainali hizo huku Liverpool ikiwa imecheza mizunguko minne.

Katika mechi zote za mechi ilizocheza Liverpool zikiwa mteremko lakini sio dhidi ya Birmingham. Liverpool ilikuwa ikipata ushindi wa sio chini ya mabao matatu, isipokuwa dhidi ya Chelsea ilioshinda kwa mabao 2-1 katika mzunguko wa tatu.

Dhidi ya Birmingham Liverpool ilinyakua taji hilo kwa changamoto ya mikwaju ya penanti 5-4 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare.

Siku hiyo Robbie Fowler alilichungulia lango la Birmingham City kwa mkwaju wa mbali katika dakika ya 30 ya mchezo lakini katika dakika za majeruhi Darren Purse aliisawazishia timu yake baada ya Martin O'Connor kuangushwa chini na Stephane Henchoz na baadaye dakika 30 za muda wa ziada ambao ulimalizika bila nyavu kutikiswa na mikwaju ya penati kuamua fainali hiyo.

Liverpool ilikuwa ikibeba taji la kwanza kwa miaka sita tangu ilipchukua taji kama hilo mnamo mwaka 1995.

0 Comments:

Post a Comment