Thursday, February 6, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Unamkumbuka mvumbuzi wa vibonzo Jack Kirby?

Februari 6, 1994 alifariki dunia mwandishi, mahriri na mchoraji wa vibonzo nchini Marekani Jack Kirby. Jina lake halisi ni Jacob Kurtzberg. 

Alifariki dunia kwa maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 76 huko Thousands Oak, California. 

Kirby amekuwa akichukuliwa kuwa ni miongoni mwa wavumbuzi na wenye ushawishi katika kuanzisha vibonzo ulimwenguni. 

Mkali huyu wa Kimarekani katika uandishi wa vitabu vya vibonzo ametengeneza mamia ya vibonzo maarufu ulimwenguni vikiwamo Captain America, Incredible Hulk na Fantastic Four, Kirby aliondoka high school akiwa na umri wa miaka 16 na akaanza kufanya kazi na studio za katuni zinazotembea za Max Fleischer ambazo zilikuwa zikitengeneza vikaragosi vya Betty Boop na Popeye. 

Alikuwa huko kabla hajaungana na msanii mwenzake wa vibonzo Joe Simon manmo mwaka 1941. 

Pia Kirby alishafanya kazi na Timely ambao baadaye walifahamika kwa jina la Marvel ambao nao walikuwa wakijihusisha na vibonzo. 

Akiwa na Joe Simon ndio walitengeneza Captain America. Kibonzo hicho kilichukua umaarufu haraka sokoni. Kirby na Joe Simon walitengeneza hadithi kwa kibonzo hicho katika maudhui tofauti yakiwamo ya kutisha, kuudhi, upelelezi wa kesi na kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1947 walitengeneza kibonzo chenye sifa za kimahaba. 

Hata hivyo urafiki baina ya wawili hao ulikoma mwaka 1956 na Kirby ikabidi arudi katika uchoraji wa vibonzo katika magazeti. Miaka hiyo hiyo ya 1950 Kirby alianza kufanya kazi na National Comics baadaye ilikuja kufahamika kwa jina la DC Comics kuwa na National pia aliendelea kufanya kazi na Marvel ambao kwa wakati huo walikuwa wakiitwa Atlas Comics. 

Kirby alitengeneza vibonzo kama Goom, Sporr, na Fin Fang Foom. Vibonzo hivyo viliongeza mauzo, Hata hivyo mnamo mwaka 1961 Mhariri wa Marvel Stan Lee ambaye ni mvumbuzi wa Spiderman hawakuelewana na Kirby hivyo ilimbidi Kirby atumie ujanja wa kutengeneza kibonzo kingine ambacho aliikiita Fantastic Four. 

Ubunifu aliokuwa nao Kirby ulikifanya kitabu hico chenye kibonzo cha Fantastic Four kupata umaarufu mkubwa sokoni. Mnamo mwaka 1962 Marvel wakaja na kitu kingine lakini Kirby akatoa kibonzo kingine alichokipa jina la Incredible Hulk. 

Sasa ukiangalia kwa makini utagundua kwamba kupambwa kwa Marvel kulitokana na ubunifu mkubwa wa Kirby kwani akiwa hapo alitoa vibonzo vingine kama X-Men, Silver Surfer, the planet-devouring Galactus, na  revived Captain America. 

Mnamo mwaka 1970 Kirby aliona kwamba anaonewa na Marvel akaamua kuondoka zake na kuanzisha DC Comics. Akiwa na DC alitengeneza Fourth World ambayo haikufanya vizuri sokoni hivyo akaamua kuachana nayo. 

Akaamua kurudi Marvel kwa muda miaka ya mwishoni  ya 1970. Ambapo Kirby akaanza kufahamika kwa jina la William Blake of Comics hivyo akaanza tena kurudi sokoni ndipo mnamo mwaka 1987 akawa miongoni mwa waanzilishi wa Will Eisner Comic Book Hall of Fame. 

Mnamo mwaka 2017 Stan Lee alimtamja Kirby kuwa ni mkongwe wa Disney kwani mchango wake ndio uliofanya kuwepo kwa Kampuni ya Walt Disney na Marvel Cinematic Universe. Lee alifariki dunia Novemba 12, 2018 jijini Los Angeles majuma sita kabla ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake akiwa na umri wa miaka 95.

Kirby alizaliwa katika jiji la New York Agosti 28, 1917 na kukulia jijini humo na mwanzoni mwa miaka ya 1930 aliingia katika medani ya uchoraji wa vibonzo. 

Alimuoa Rosalind Goldstein mnamo mwaka 1942 na walifanikiwa kuzaa watoto wanne.
Captain America

0 Comments:

Post a Comment