Monday, February 24, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Malcolm Forbes ni nani?

Februari 24, 1990 alifariki dunia Mjasiriamali wa nchini Marekani ambaye alifahamika sana kwa kuchapisha jarida la Forbes ambalo lilianzishwa na baba yake na yeye kuliendelea.

Malcolm Forbes alikuwa mahiri katika kuutangaza ubepari na soko huru la biashara. Pia Forbes alikuwa na biashara nyingine kama mashua, ndege, pikipiki na vito vya thamani. 

Forbes alifariki kwa maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 70 akiwa nyumbani kwake Timberfield huko Far Hills, New Jersey. 

Dkt. Oscar Kruesi ambaye alikuwa rafiki na daktari wake alitanza kifo cha mjasiriamali huyo. Mnamo Machi 1990 baada ya kifo chake jarida la OutWeek lilichapisha katika ukurasa wa mbele  habari, iliyopambwa na kichwa "The Gay Life of Malcolm Forbes," na mwandishi aliyeandika alikuwa ni Michelangelo Signorile. 

Habari hiyo ilikuwa ikimwangazia Forbes kuwa ni mtu aliyekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja. 

Tangu alipofariki dunia milionea huyo jarida lake limekuw alikiendeshwa na mtoto wake Steve Forbes mjukuu wake Moira Forbes. 

Milionea huyo alimwoa mwanmke mwenye umri wa miaka 39 Roberta Remsen Laidlaw kabla hawajapeana talaka mnamo mwaka 1985. 

Walifanikiwa kuzaa watoto watano; ambao ni Malcolm S. Jr., Robert Laidlaw, Christopher Charles, Timothy Carter, na Moira Hamilton. 

Malcolm S. Jr amekuwa akifahamika kwa jina la Steve ambaye tangu mwaka 1996 alianza kuongoza kama Rais wa kampuni za baba yake. 

Forbes alizaliwa Agosti 19, 1919 huko Englewood, New Jesrey kwa wazazi Adelaide Mary na mwandishi wa habari za biashara na uchumi pia mwandishi wa vitabu Bertie Charles Forbes aliyekuwa na asili ya Uskochi. 

Alihitimu katika shule ya Lawrenceville mnamo mwaka 1937 na baadaye katika chuo kikuu cha Princeton. 

Forbes alitajwa katika orodha ya wanajeshi wa Marekani mnamo mwaka 1942 akihudumu katika kitengo cha silaha katika kikosi cha 84 cha Waenda kwa Miguu  barani Ulaya. 

Akiwa jeshini alifanikiwa kupanda cheo hadi Staff Sergeant na kupata medali kadhaa za kijeshi.


0 Comments:

Post a Comment