Monday, February 10, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Papa Pius wa XI ni nani?


Februari 10, 1939 alifariki dunia kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Pius wa XI. Jina lake halisi Ambrogio Damiano Achille Ratti. 

Alikuwa Papa wa Kanisa Katoliki kutoka Februari 6, 1922 hadi mauti yalipomkuta. Papa huyu enzi za utawala wake alikuwa na kauli mbiu ya "Amani ya Kristo katika Ufalme wa Kristo". 

Papa Pius wa XI alianza kuugua Novemba 25, 1938 ambapo alipata shambulio la moyo mara mbili ndani ya saa kadhaa. 

Kushindwa kupumua na kushindwa kuondoka katika eneo lake  kulionyesha dhahiri kuwa kiongozi huyo alikuwa mgonjwa. Watalaamu wa Afya wa Vatican walisema virba hewa katika mapafu yake ndio chanzo kikuu cha matatizo hayo.

Hatimaye saa 11:31 alfajiri kwa saa za Rome alipatwa na shambulio la moyo kwa mara ya tatu na kufariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Waliokuwa karibu yake walisema Papa  alizungumza maneno yenye kutia matumaini, : "Nafsi yangu inaachaana nanyi nyote kwa amani". Wengine waliamini kuwa Papa Pius XI alikuwa ameuawa.

Papa Pius wa XI anakumbukwa sana kutokana na kuliongoza kanisa hilo wakati wa vita kuu mbili za dunia. 

Pia kiongozi huyo anakumbukwa kutokana na kuwa alikuwa akipendelea kupanda milima kama vile milima ya Alps.

0 Comments:

Post a Comment