Wanahistoria ni watu ambao
wamejikita katika kujifunza mambo ya kale au mambo yaliyopita. Baadhi yao ni
wataalamu ambao wanaishi kwa kujifunza mambo ya kale.
Wengine ni wanahistoria
ambao wanajifunza mambo hayo kwa ajili ya furaha zao tu. Na wapo wengine ambao
ni wanahistoria kama wewe ambao ni wanafunzi wanaojifunza kozi ya Historia.
Wanahistoria ambao ni wataalamu hujumuisha watu wanaofundisha na kuandika
masuala mbalimbali ya kihistoria.
Wataalamu wengi wa historia
wamekuwa na mchango mkubwa katika uandishi wa vitabu mbalimbali. Katika hilo
wamekuwa na kazi ya kuchagua taarifa za matukio muhimu ambayo kwa kiasi kikubwa
yametoa mchango mkubwa wa kuielewa historia kwa undani.
Pia wataalamu hao wametoa
mchango wao katika kuyatafsiri kutoka katika lugha ya asili ya matukio yenyewe
na kuyaweka katika mwonekano wa sasa.
Historia ina upana wake
ikijumuisha uzoefu wa binadamu mwenyewe katika maisha yake. Wanahistoria walio
wengi wanaendelea kujikita katika eneo moja la historia ili kulichimba kwa kina
na kuleta maana iliyokusudiwa. Kwa mfano;
Historia
ya Masuala ya Siasa,
Hii imejikita katika
historia za serikali mbalimbali, sheria na viongozi wa kisiasa. Kwa mfano
utawala wa Farao wa Misri na namna alivyotawala taifa hilo ni miongoni mwa
historia ya masuala ya siasa.
Historia
ya Masuala ya Kijeshi,
Imejikita katika kujifunza
migogoro, vita, silaha, sufundi na mbinu za kivita. Pia imejikita ni kwa namna
gani watu walisuluhisha migogoro katika jamii zao.
Historia
ya Masuala ya Jamii,
Imejikita katika kuelezea
kila hatua ya maisha ya watu, zana walizokuwa wakitumia, sanaa waliyokuwa nayo,
chakula walichokuwa wakila, na wakati mwingine imejikita kwa namna ambavyo watu
walikuwa wakiitazama dunia na maadili yao kwa ujumla na namna walivyokuwa
wakiwafundisha watoto wao. Wakati ambapo tunatazama mchango wao katika sanaa,
fasihi, sayansi hiyo ni Historia ya Masuala ya Jamii.
Historia
ya Masuala ya Kitaaluma,
Imejikita katika mawazo
ambayo yanahamasisha na kuiongoza jamii. Baadhi ya mawazo hayo ndio yalikuwa
chanzo cha wanafikara wa enzi hizo. Hapa ndipo mawazo ya kiteolojia na
kifalsafa yanapojumuishwa katika Historia ya Masuala ya Kitaaluma.
Historia
ya Masuala ya Kiuchumi
Imejikita katika bidhaa na
huduma za watu katika kuuza na kununua bidhaa zao walizokuwa wakitengeneza.
Namna walivyotumia malighafi katika mazingira yao. Bussiness, finance (fedha)
and trade (biashara) huwekwa katika kundi hili la Historia ya Masuala ya Uchumi.
0 Comments:
Post a Comment