Mei
25, 2016 alifariki dunia msanii, mwandishi wa vitabu na mkalimani wa China Yang
Jiang. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 104.
Yang Jiang aliandika
vichekesho vingi vilivyopata umaarufu mkubwa na huyu aliweka rekodi ya kwanza
nchi China ya kumaliza toleo la Kichina la Riwaya ya Miguel de Cervantes’ Don
Quiote.
Alizaliwa Julai 17, 1911 mjini Beijing na kufariki dunia katika mji
aliozaliwa. Wakati anazaliwa alipewa jina la Yang Jikang na alikulia katika
mkoa wa Jiangan. Baada ya kumaliza katika Chuo Kikuu cha Soochow mnamo mwaka
1932, Yang Jiang aliingia tena darasan katika Chuo Kikuu cha Tsinghua.
Akiwa
huko ndipo alipokutana na Qian Zhongshu na wakaoana mnamo mwaka 1935. Mumewe
huyo alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 mnamo Desemba 19, 1998. Kutoka
mwaka 1935-1938 alikwenda kusoma nje ya nchi na nchi aliyokwenda ilikuwa ni
England ambapo alitua katika Chuo Kikuu cha Oxford akiwa na mumewe. Akiwa
nchini England alimzaa mtoto wake aliyempa jina la Yuan mnamo mwaka 1937.
Pia
baadaye walikwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Pantheon-Sorbonne jijini Paris
nchini Ufaransa. Katika maisha yao walipokuwa nchini China walikuwa
wakizungumza Kiingereza na Kifaransa. Walirudi nchini China mnamo mwaka 1938 na
wakawa wanaishi Shanghai.
Akiwa hapo Shanghai aliandika tamthilia nne katika muundo wa vichekesho ambazo zilipata
uungwaji mkono Heart's Desire (稱心如意) mnamo mwaka 1943, Forging the Truth (弄真成假)
mnamo mwaka 1944, Sporting with the World (游戏人间) mnamo
mwaka 1947, na Windswept Blossoms (风絮) mwaka 1947. Kwa upande wa Riwaya Yang Jiang
aliandika Baptism (洗澡)(1988) na After the Bath (洗澡之後)(2014).
Hata hivyo kabla hajageukia uandishi wa riwaya Yang Jiang aliandika insha tatu
miaka ile ya 1980 ambazo ni Six Chapters from My Life 'Downunder' (幹校六記)
(1981) na About to Drink Tea (將飲茶) (1987) kisha insha moja aliiandika mnamo mwaka
2003 ya We Three (我們仨).
Akiwa na umri wa miaka 96 hiyo ilikuwa mwaka
2007, Yang Jiang aliushangaza ulimwengu kwa kuandika insha aliyoipa jina Reaching
the Brink of Life (走到人生邊上).
Uandishi wa kitabu hicho kwa mfumo wa Insha
ulikuwa katika mfumo wa kifalsafa, ambao vichwa vya kila ukurasa alichukua
kutoka katika insha za mumewe Magnalia to Life.
Uandishi wa Reaching the Brink
of Life umemweka Yang Jiang kama kitabu pekee kinachohusu maisha yake Yang. Nusu
ya kwanza ya kitabu hicho Yang anajipambanua yeye mwenye katika suala la
Maisha, Kifo na Maisha baada Kifo na nusu ya pili ya kitabu hicho imechukua
masuala ya kifamilia na mistari kadhaa ya kusoma.
Hata hivyo Insha yake ya Six
Chapters from My Life 'Downunder' kwa hakika inaendelea kukonga nyoyo za watu
kutokana na uandishi mzuri uliomo ndani yake.
0 Comments:
Post a Comment