Jabir Johnson, Tanzanian Journalist and Radio Presenter |
Katika jitihada za kutafuta elimu duniani, ni juu yetu kujitahidi
sana kusoma mambo yenye faida kwa maisha yetu. Katika jitihada hizi, mtu
huambulia elimu za namna mbalimbali kutoka vyanzo mbalimbali.
Dunia inahitaji utaalam/ufundi wa namna nyingi kwa mtu mmoja
ili afanikiwe kuwa kivutio katika soko la ajira; lakini pia ili mtu huyo aweze
kwenda na wakati.
Hivyo nawahimiza Watanzania na Waafrika wenzangu tusijiweke
nyuma katika elimu yoyote iwayo yenye faida katika maisha yetu. Japo
"elimu yenye faida" inaweza kuwa na tafsiri tofauti kwa watu tofauti.
0 Comments:
Post a Comment