Saturday, May 30, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Voltaire ni nani?

Francois-Marie Arouet (Voltaire)
Mei 30, 1778 alifariki dunia mwandishi wa kipindi cha mwangaza nchini Ufaransa, mwanahistoria na mwanafalsafa Francois-Marie Arouet maarufu kwa jina la Voltaire.

Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 84. Anakumbukwa kutokana na ukosoaji wake katika dini ya Ukristo hususani kanisa la Roman Catholic. 

Pia anakumbukwa kutokana na umahiri wake wa kuzungumza na kuandika mambo kwa akili na yenye kuchekesha. Uwezo huo ulimfanya Voltaire awe mtu muhimu sana katika kipindi cha mwangaza barani Ulaya hususani nchini Ufaransa katika karne ya 17 hadi 19. 

Voltaire alipigania uhuru wa kuzungumza, uhuru wa kuabudu pia alitoa ushauri kuwepo na utengano baina ya kanisa na serikali (nchi). Voltaire alikuwa mwandishi ambaye alikuwa na uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira (versatile). Alifanikiwa kuandika insha, mashairi, riwaya na tamthilia. Aliandika zaidi ya barua 20,000; vitabu na vitini zaidi ya 2,000. 

Ukosoaji wake haukuweza kuvumilika mbele ya watawala wa wakati huo na wenye kushikilia mafundisho ya dini. Katika maisha yake, Voltaire aliwahi kuwekwa mahabusu mara mbili na kubadilishwa kwa muda wa miaka mitatu nchini Uingereza. Kitendo hicho kilimkasirisha sana Voltaire na kuwa dhidi ya utawala wa Ufaransa. Mnamo Februari 1778 Voltaire alirudi kwa mara ya kwanza jijini Paris baada ya kupita miaka 25. 

Katika safari ya siku tano akiwa na umri wa miaka 83 iliaminika kuwa angefariki dunia mnamo Februari 28 mwaka huo huo. Ndipo Voltaire alipochukua kalamu na karatasi kisha kuandika maneno haya, 

Ninakufa huku nikimuabudu Mungu, nikiwapenda marafiki zangu, na sio kuwachukia maadui zangu na nikiuchukia ushirikina.” 

Baada ya kuandika hayo hakufa ambapo mnamo mwezi Machi na kuona onyesho lililopewa jina la Irene. 

Katika tamasha hilo Voltaire alishangiliwa na washiriki na kuchukuliwa kuwa ni shujaa aliyerudi. Hata hivyo hali yake ya afya ilibadilika tena na kufariki dunia Mei 30, 1778 licha ya kwamba chanzo cha kifo chake hakijawekwa bayana hadi leo. Isipokuwa maadui zake walikaririwa wakisema Voltaire alitubu na kukubali sakramenti ya mwisho kutoka kwa Padri wa Katoliki. 

Pia kuna chanzo kimoja kilidai kuwa wakati wa mazungumzo na kiongozi wa kanisa kwamba amkatae Shetani Voltaire alisema, “Huu sio muda wa kutengeneza maadui wapya.” 

Miaka ya 1856 kauli yake hiyo ilionekana kama ulikuwa utani ulichapishwa katika gazeti moja huko Massachussets nchini Marekani. Hata hivyo kutokana na kuwa mkosoaji wa Kanisa, Voltaire alikataa maziko ya Kikristo jijini Paris. Ndugu, jamaa na marafiki walifanikiwa kumzika kwa siri mwanafalsafa huyu huko Champagne katika makaburi ya Abbey Scellieres. 

Aidha moyo na ubongo vilitenganishwa na kuoshwa. Mnamo Julai 11, 1791 Bunge la Ufaransa lilimtambua rasmi Voltaire kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Mapinduzi ya Ufaransa hivyo iliamuru mabaki ya mwili wake kurudishwa Paris kisha kuzikwa tena upya katika makaburi ya  Pantheon. Maelfu ya watu walihudhuri hafla hiyo jijini humo.

0 Comments:

Post a Comment