Kija Elias Kisena |
“Namshukuru
sana Mungu kwa siku hii ya leo kwa kunifikisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa
kwangu ndivyo ninavyoweza kusema.
kwa muda mrefu ni kwa nini Mimi ninaishi!?...Nimekuwa
nikijiuliza nimempa chochote huyu Mungu ili niendelee kuishi?
Je? waliokufa kwa ajili na magonjwa mbalimbali hao sio wana
wa Mungu au walikuwa na dhambi nyingi sana, Hakika nimegundua kwamba Ninaishi
kwa Neema tu!
Kwa neema ya Mungu ninaishi, kwa neema ya Mungu niko
mzima, niamkapo mzima ni kwa neema, nitembeapo njiani ni kwa neema, baraka
nizionazo ni kwa neema tu!
Naamini kwa neema zake Mungu, atanifanya niishi miaka
mingi mpaka kuiona ile nchi ya ahadi aliyowaahidi wana wa Israeli na dunia kwa
ujumla.
Kuna wengi walitamani kuongeza miaka yao lakini
hawakuweza kufikia matumaini yao, kuna
wengine sasa hivi wanagombea uhai wao huko hospitalini, wengiine wako vitani,
wengine wapo barabarani na hata mahala pengine ili waweze japo kufikisha siku
nyingine kama hii niliyoifikia mimi leo. lakini Muumba ameniona Mimi kunibariki
kwa kunipa uhai na furaha yangu siku hii ya leo.
Ahsante Baba yangu mzazi, ahsante sana Mama yangu
kipenzi kwa zawadi hii ya kunileta duniani najua ni magumu mengi mlipitia mpaka
kunifanya leo hii nami nionekane mtu katika watu, sina cha kuwalipa zaidi ya
kuendelea kuwaombea kwa Mungu.”
Kija Elias Kisena ni mwandishi wa habari nchini
Tanzania. Alizaliwa Mei 18, 1975 katika kijiji cha Nyanguge wilayani Magu
mkoani Mwanza. Kwa sasa ameweka makazi yake mkoani Kilimanjaro huku akiendelea
kufanya kazi zake za uandishi wa habari.
Amewahi kuwa ripoti wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) katika kipindi cha miaka 2010-2012. Katika medani ya
uandishi alianza mwaka 2006 hadi sasa. Pia kituo cha Televisheni cha Star TV. Kutoka mwaka 2019 amekuwa mwandishi wa gazeti La Jiji mkoa wa Kilimanjaro. Amekuwa mahiri zaidi katika uandishi wa
habari za mazingira, kilimo na utalii.
STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
DATE: May 18, 2020
0 Comments:
Post a Comment