Mei 17, 1919 alifariki dunia mwanasiasa na Rais wa 25 wa
Nicaragua Jose Santos Zelaya. Alifariki dunia jijini New York nchini Marekani akiwa
na umri wa miaka 65.
Zelaya anakumbukwa kutokana na kuikalia nchi hiyo kimabavu
wakati wa utawala wake kupitia mapinduzi mwaka 1893.
Alipinduliwa mwaka 1910 na
Dkt. Adolf Diaz aliyehitimisha utawala wa miaka 13 ya Zelaya.
Kisiasa, akiwa
madarakani Zelaya alikifanya chama chake cha Liberal kuwa cha kipekee katika
historia ya Nicaragua hadi 1930 na kuwasili kwa utawala wa kidikteta wa Somoza
ambao ulikalia taifa hilo kwa miaka 43 kutoka mwaka 1936 hadi 1979.
Utawala
wake ulififisha na kufadhili jamii ya Wanicaragua kwa wakati mmoja. Kiuchumi,
Zelaya aliongoza upanuzi wa kibiashara ambao ulikuwa na athari kubwa kwa raia
wa Nicaragua.
Ulimwenguni, utawala wake uliambatana na kipindi cha ushawishi
mkubwa wa Nicaragua kwa majirani zake wa Amerika ya Kati.
Katiba ya mwaka 1893
iliimarisha serikali za manispaa, ikatenganisha kanisa na serikali, ilizuia
marufuku na nyumba za watawa, ilitoa kipaumbele cha elimu bora, ilianzisha
bunge lisilo la kisheria, na kukomesha hukumu ya kifo.
Kama viongozi wengine wa
Amerika ya Kusini, Zelaya alijitolea kuleta maendeleo ya kiuchumi katika nchi
yake, hata kwa njia za kimabavu.
Alichukua hatua za kukuza kilimo cha kuuza nje
(kilimo biashara) na kukafikiwa makubaliano kwa madhumuni ya kutumia rasilimali
asili. Ujenzi wa reli na matumizi ya meli za mvuke kwenye maziwa ya Managua na
Nicaragua yalipewa kipaumbele katika utawala wake.
Mnamo mwaka wa 1907, wakati
ugomvi kati ya Nicaragua na Guatemala ulipoenea Honduras na El Salvador, na
kutishia utulivu katika Amerika ya Kati, Washington ilianza kumwona Zelaya kama
tishio la amani na utulivu katika eneo hilo.
Tukio la mwaka 1909 lililohusisha
kuuawa kwa mamluki wawili wa Marekani lilisababisha uamuzi wa Washington kuunga
mkono uasi dhidi ya Zelaya. Dikteta huyo alijiuzulu na kwenda uhamishoni mnamo
Desemba 1909.
0 Comments:
Post a Comment