Hali ya ukusanyaji wa
takataka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro inaweza kuwa na sura mbili tofauti hali
ambayo inaweza kumfanya yeyote anafahamu sifa za mji huo mashuhuri kustaajabu.
Wananchi wamekuwa wakiitia
wito wa kukusanya taka na kuziweka katika maeneo yanayotakiwa japo sio wote
lakini kwa asilimia kubwa mwitikio umekuwa zaidi ya asilimia 70.
Pia wananchi hao wamekuwa
wakitoa pesa ya taka kila mwezi. Katikati ya mji huo ambao upo katika Halmashauri
ya Manispaa ya Moshi Mjini suala la ukusanyaji halina shida limekuwa likifanywa
kwa uaminifu mkubwa na magari ya kisasa.
Nje kidogo ya mji huo ambako
kuna mitaa inayounda halmashauri hiyo ndipo unaweza kujiuliza ni kwa namna gani
wanafanya suala hilo.
Maghuba ya kutupa takata
yanaonekana kujaa hata kuleta harufu mbaya katika mitaa. Kwani usafi sio tu
ukusanyaji wa takata lakini pia na harufu mbaya katika mitaa ni uchafu kama
ulivyo mwingine.
Kama haitoshi dampo la
Kaloleni nalo limefurika hali inayotishia afya za wanaishi kuzunguka dampo
hili.
Uongozi wa halmashauri hiyo
upo mbio kufungua dampo jipya lililopo Mtakuja katika Halmashauri ya Moshi
Vijijini mwishoni mwa Aprili mwaka huu.
ALL PHOTOS BY: Jabir Johnson
0 Comments:
Post a Comment