Wednesday, April 1, 2020

Mfahamu Mfalme Tutankhamon wa Misri 1347K.K-1339 K.K


Ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka 1922, huko Kaskazini Mashariki mwa Afrika, jua lililikuwa kali na joto katika Valleys of the Kings, ambalo ni bonde lililopo nchini Misri karibu na sweeping curve ya mto Nile.

Mwana akiolojia wa Uingereza Howard Carter (1874-1939) alikuwa nchini Misri kwa miaka sita ambako alikwenda kwa ajiliya kufanya utafiti wake katika makaburi ya Wafalme wa Misri ya Kale hususani Wafalme waliotawala miaka ya mwishoni mwa enzi za taifa hilo.

Miaka zaidi ya 3,000 imekwisha pita tangu wafalme hao walipozikwa. Kwa karne nyingi tu, wezi wamefukua makaburi hayo na kujichukuliwa vito vya thamani walivyozikwa navyo wafalme hao. 

Novemba 26, 1922, Carter alisimama mbele ya upande ambao ulikuwa umezibwa lakini hakufikiria kama ndoto zake zingekuja kuwa kweli kwani katika eneo hilo ndiko mali na utajiri wote wa Mtawala Tutankhamon. Carter alichimba shimo dogo katika mlango  na kuweka mshumaa.

Baada ya kufanya hivyo alipata majibu ya nini kilichokuwamo ndani ya kaburi hilo. Carter alisema, “ At first I could see nothing…but presently as my eyes grew accustomed to the light , details of the room within emerged slowly from the mist, strange animals, statues and gold-everywhere the glint of gold.”
Utajiri wa dhahabu ndani ya kaburi hilo ikiwamo four golden chariots, gilded couches, a golden throne with lions’ heads carved in arms, and much more. Hivyo vyote vilikuwa kwa ajili ya mtawala Tutankhamon (King Tut) aliyetawala Misri.

Tutankhamon alishika mamlaka hayo akiwa na umri wa miaka minane ikiwa ni mwaka 1347 K.K na alifariki miaka tisa baadaye akiwa na umri wa miaka 17 hiyo ilikuwa mwaka 1339 K.K

Hakika Carter alifikia kilele cha kile alichokuwa akikitafuata lakini alisalia na swali moja wapi alipozikwa Malkia huyo Kifalme. Hatimaye walifanikiwa kuchimba na kukutana na alipozikwa kwani walikutana na sanduku kubwa lililotengenezwa kwa mahesabu.

Walipolifunua sanduku hilo walikutana na kinyago kilichonakshiwa kwa dhahabu, macho ya bluu yaliyotengenezwa kwa mawe ya thamani.Carter aliandika, “ Among all that regal splendor, that royal magnifence… there was nothing so beautiful as those few withered flowers…They told us what a short period 3,300 years really was.”

Utawala wa Tutankhamon ulikuwa ni mfupi katika historia ya Misri ya Kale. Misri ilikuwa tayari ni Muungano wa Falme kwa takribani miaka 1,700 kabla ya ujio wa Tutankhamon katika kiti cha enzi. Nchi aliyokuwa akiitawala ilikuwa ya siku nyingi kama miji mingine ya Sumeri.

Licha ya kwamba Misri ya Kale iliibuka sawa na enzi za Wasumeri lakini ustaarabu wa Misri ulikuwa tofauti kabisa kutoka katika namna ya maisha yalivyokuwa hadi kuwa Fertile Crescent.

Tofauti na ilivyokuwa Kusini Magharibi mwa Asia, Misri ilikuwa tayari imeshaungana na kuwa kama nchi kwa miaka mingi. Misri ya Kale ilipitia vipindi vizuri na vigumu kwa zaidi ya miaka 3,000.

Hata hivyo mwanzo wa Misri ya Kale ndio umekuwa mwanzo wa kuwapo kwa story kuhusu Nile, Kwani mto Nile uliyatengeneza kwa kiasi kikubwa maisha ya Wamisri.

FEATURE STORY: Jabir Johnson
PHOTO BY: Jabir Johnson/Maktaba
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Aprili 1, 2020



0 Comments:

Post a Comment