Friday, April 3, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Carl Burton Stokes ni nani?



Aprili 3, 1996; alifariki dunia mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Marekani Carl Burton Stokes ambaye alihudumu  katika wadhifa wa Umeya wa 51 Cleveland, Ohio. 

Anakumbukwa kutokana na kuwa Mmarekani wa kwanza kushika wadhifa huo katika Cleveland. Alihudumu kutoka Novemba 7, 1967 hadi Januari 1, 1968. Alifariki dunia Aprili 3, 1996 akiwa na umri wa miaka 68. 

Kutoka mwaka 1983 hadi 1994 alihudumu kama Jaji wa Manispaa ya Cleveland. Enzi za utawala wa Rais Bill Clinton, Stokes aliteuliwa kuwa Balozi wa Marekani huko Ushelisheli. 

Enzi za uhai wake Stokes alitunukiwa shahada 12 za heshima na tuzo nyingine za kiraia. 

Alifariki dunia kwa maradhi ya saratani koo katika mfumo wa chakula. Alizikwa katika makaburi ya Lake View, Cleveland, Ohio. (1927-1996)

0 Comments:

Post a Comment