Mwenyekiti wa MECKI Bahati Nyakiraria |
Klabu ya Waandishi wa
habari mkoani Kilimanjaro (MECKI), imewaomba wadau mbalimbali kuweza kuwasaidia
vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona pindi pale
wanapotekeleza majukumu yao.
Akizungumza na
wanahabari mkoani hapo Mwenyekiti wa MECKI, Bahati Nyakiraria alisema wadau
mbalimbali wamekuwa wakielekeza juhudi zao kwa wananchi huku wakiwasahau
wanahabari kitendo ambacho sio sahihi kwa wanahabari nao ni wananchi
wanaopaswa kulindwa.
“Katika mapambano
dhidi ya virusi vya Corona nchini, vitakasa mikono kwa waandishi wa
habari vinahitajika sana, ili viwasaidie kuwakinga na ugonjwa huo, sote
tunatambua kazi kubwa inayofanywa na mwandishi wa habari hasa katika kutoa
elimu kwa umma kuhusu Corona hivyo ni kuna umuhimu mkubwa kwa wanahabari na wao
wakapatiwa vifaa hivyo ili kuweza kujikinga na kuwa salama zaidi,” alisema
Nyakiraria.
Nyakiraria alisema
mwandishi wa habari ni anatakiwa kwenda na kufika katika eneo la tukio kwa
ajili ya kuandika na kutangaza kile kilichotokea katika tukio hilo tofauti na
kada nyingine ambao wanaweza kufanya kazi zao akiwa nyumbani.
“Vita vinapotokea
askari lazima atatoka na kwenda kuimarisha usalama katika eneo husika, vilevile
na mwandishi wa habari ni lazima atoke ili kwenda kuandika habari zilizotokea
katika eneo husika hivyo anahitaji kujikinga na usalama wake hivyo wadau
wanapaswa kutambua umhimu wa wanahabari katika kuhabarisha umma wa
Watanzania masuala mbalimbali yanayotokea hapa nchini,” alisema.
Hata hivyo ameitaka
jamii kuondoka na fikra potofu kuwa wanahabari wanaishi maisha mazuri kuliko
watu wengine katika jamii akisisitiza kuwa umahiri na umaarufu wao usiwafanye
kuona kama hawastahili huduma kama kada nyingine.
“Tumekuwa tukitumika
penye uhitaji lakini kuna wakati maisha yanakuwa magumu kutokana na kuonekana
kuwa ni kazi ya kujitolea na kuonekana ni watu wenye maisha mazuri hali ambayo
imekuwa ikiwaacha wanahabari njiapanda katika maisha,” alisisitiza Nyakiraria.
Klabu ya Waandishi wa
habari mkoani Kilimanjaro (MECKI), imewaomba wadau mbalimbali kuweza kuwasaidia
vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona pindi pale
wanapotekeleza majukumu yao.
Akizungumza na
wanahabari mkoani hapo Mwenyekiti wa MECKI, Bahati Nyakiraria alisema wadau
mbalimbali wamekuwa wakielekeza juhudi zao kwa wananchi huku wakiwasahau
wanahabari kitendo ambacho sioi sahihi kwa wanahabari nao ni wananchi
wanaopaswa kulindwa.
“Katika mapambano
dhidi ya virusi vya Corona nchini, vitakasa mikono kwa waandishi wa
habari vinahitajika sana, ili viwasaidie kuwakinga na ugonjwa huo, sote
tunatambua kazi kubwa inayofanywa na mwandishi wa habari hasa katika kutoa
elimu kwa umma kuhusu Corona hivyo ni kuna umuhimu mkubwa kwa wanahabari na wao
wakapatiwa vifaa hivyo ili kuweza kujikinga na kuwa salama zaidi,” alisema
Nyakiraria.
Nyakiraria alisema
mwandishi wa habari ni anatakiwa kwenda na kufika katika eneo la tukio kwa
ajili ya kuandika na kutangaza kile kilichotokea katika tukio hilo tofauti na
kada nyingine ambao wanaweza kufanya kazi zao akiwa nyumbani.
“Vita vinapotokea
askari lazima atatoka na kwenda kuimarisha usalama katika eneo husika, vilevile
na mwandishi wa habari ni lazima atoke ili kwenda kuandika habari zilizotokea
katika eneo husika hivyo anahitaji kujikinga na usalama wake hivyo wadau
wanapaswa kutambua umhimu wa wanahabari katika kuhabarisha umma wa
Watanzania masuala mbalimbali yanayotokea hapa nchini,” alisema.
Hata hivyo ameitaka
jamii kuondoka na fikra potofu kuwa wanahabari wanaishi maisha mazuri kuliko
watu wengine katika jamii akisisitiza kuwa umahiri na umaarufu wao usiwafanye
kuona kama hawastahili huduma kama kada nyingine.
“Tumekuwa tukitumika
penye uhitaji lakini kuna wakati maisha yanakuwa magumu kutokana na kuonekana
kuwa ni kazi ya kujitolea na kuonekana ni watu wenye maisha mazuri hali ambayo
imekuwa ikiwaacha wanahabari njiapanda katika maisha,” alisisitiza Nyakiraria.
0 Comments:
Post a Comment