Thursday, April 2, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Papa Yohana Paulo II ni nani?


Aprili 2, 2005 alifariki dunia Papa Yohana Paulo II. Alikuwa papa wa 264 kuanzia Oktoba 16, 1978 hadi kifo chake akidumu katika huduma hiyo kirefu kuliko mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pius IX. 

Huyu ndiye Papa wa kwanza asiye Mwitaliano kwa takribani miaka 455, tangu wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena papa wa kwanza kutoka Polandi (na makabila yoyote ya Waslavi) katika historia ya Kanisa. 

Alifuatiwa na Papa Benedikto XVI. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef WojtyÅ‚a
(1920-2005)

0 Comments:

Post a Comment