Jina halisi
la mfanyabiashara huyo wa dawa za kulevya ni Juan Carlos RamĂrez AbadĂa maarufu
kwa jina la Alias Chupeta. Hadi kukamatwa kwake alikuwa miongoni mwa viongozi
wakubwa wa genge la Norte del Valle Cartel. Genge hili lilijizolea umaarufu
mkubwa kutokana na mauaji na uuzaji wa dawa haramu za kulevya nchini Marekani.
Chupeta
alikuwa mfanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya Cocaine. Inaaminika kwamba
Chupeta alikuwa akijihusisha na utapeli wa fedha na uuzaji wa dawa haramu za
Heroin. Chupeta ni raia wa Colombia.
Alizaliwa
Februari 16, 1963 huko Palmira. Mkurugenzi wa Idara moja nchini Marekani Adam J.
Szubin aliwahi kukaririwa akimtaja Chupeta kama mmoja wa wafanyabiashara wa
dawa wenye nguvu na mgumu sana huko Colombia.
Chupeta
alitupwa jela nchini Colombia mnamo mwaka 1999 hadi 2002 baada ya kujisalimisha
kwenye mamlaka. Kinachostaajabisha zaidi alipotoka jela ni pale alipofanya
upasuaji katika uso wake ili kuondoa sura yake na kuiweka mpya. Agosti 7, 2007
alikamatwa jijini Sao Paulo nchini Brazil katika eneo la Aldeia da Serra.
Alihukumiwa
miaka 30 jela nchini Brazil mnamo Aprili 2008. Mnamo Machi 13, 2008 Mahakama ya Juu nchini Brazili ilitoa hati ya
kumkabidhi kwa mamlaka za Marekani. Tukio hilo lilikuja kufanyika Agosti 22,
2008.
Baada ya
kukabidhiwa kwa mamlaka za Kisheria za Marekani alitoa ushahidi wa kuwa
mshirika wa karibu wa Joaquin “El Chapo” Guzman ambaye ni mfanyabiashara
mashuhuri wa dawa za kulevya raia wa Mexico.
0 Comments:
Post a Comment