Juni 28, 1836 alifariki dunia mwanasiasa, mwanadiplomasia, mwanafalsafa na mwanzilishi wa taifa la Marekani James Madison Jr.
Huyu alikuwa Rais wa nne Marekani
kutoka mwaka 1809 hadi 1817. Anachukuliwa kuwa mtu muhimu sana katika uandishi
wa katiba ya Marekani.
Madison amekuliwa akichukuliwa kuwa ‘Baba wa Katiba’ kutokana na mchango wake mkubwa katika uandishi wa mwongozo wa taifa hilo na muswada wa haki za Marekani.
Madison alikuwa mwandishi wa Magazeti ya Federalist pia miongoni mwa
waanzilishi wa Chama cha Democratic-Republican. Madison alianzisha chama hicho
akiwa na Thomas Jefferson.
Pia katika utumishi wake nchini Marekani alikuwa Katibu Mkuu wa Tano wa taifa hilo kwa miaka minane kutoka mwaka 1801 hadi 1809.
Alifariki dunia akiwa na
umri wa miaka 85. Madison hakuwa na umbo kubwa, pia alikuwa na macho ya bluu ya
kung’aa, alikuwa na msimamo imara, alikuwa akifahamika kwa uchangamfu akiwa na
mikusanyiko midogo.
Aliugua sana wakati wa uhai wake kutokana na msongo wa mawazo. Hata
hivyo alifariki dunia kutokana na kupatwa na hofu ya kuogopa kuumwa
(hypochondriac) inaelezwa kuwa Madison alikuwa anaogopa sana kuumwa. Alipoumwa
msongo wa mawazo uliofanya afya yake iteteleke.
Madison alizaliwa Machi 16, 1751 katika mashamba ya Belle Grove karibu na Port Conway, Virginia, kwa wazazi Madison Sr. na mama yake Nelly Conway. Familia yao iliishi huko Virginia tangu miaka ya 1600.
Madison alikuwa mtoto wa
kwanza kati ya 12 wa Mzee Madison Sr. alikuwa na kaka zake saba na dada sita.
Kati ya hao ni sita tu waliofika utu uzima.
Baba yake alikuwa mkulima wa tumbaku katika mashamba ambako sasa
kunafahamika kama Mount Pleasant. Alikuwa na watumwa 100 katika ekari 5,000.
Madison Sr. alikuwa mmiliki mkubwa wa ardhi na alikuwa akiongoza huko Piedmont.
0 Comments:
Post a Comment