Tuesday, June 23, 2020

Mfahamu Catherine the Great II alivyowatendea Wayahudi

Juni 23, 1794  Malkia wa Urusi aliyefahamika kwa jina la Catherine The Great, aliwapa ruhusa wayahudi waweze kukaa katika mji wa Kiev.

Malkia huyu alitawala Russia kutoka mwaka 1762 hadi 1796 akiweka rekodi ya kuwa mtawala wa kike alikalia kiti hicho kwa muda mrefu.

Aliingia madarakani baada ya kumpindua mumewe Peter III katika jaribio alilolitengeneza mwenyewe. Malkia huyu aliitawala Russia wakati ambao ilikuwa ikitanuka kwa kasi huku akisaidiwa na makamanda wa kijeshi alioendana bega kwa bega Grigory Orlov na Grigory Potemkin.

Pia alikuwa na wanajeshi wengine waliompa msaada mkubwa wakati wa utawala wake Jenerali Alexander Suvorov na Jenerali Pyotr Rumyantsev.

Magavana wa kijeshi walimpa ushirikiano mkubwa kama Fyodor Ushakov. Catherine the Great aliitawala Russia kwa kijeshi na maridhiano.

Anakumbukwa kutokana na namna alivyoweza kuufanyia marekebisho mfumo wa kiutawala ikiwamo majimbo (guberniyas) ambapo miji mipya ilianzishwa wakati wake kutokana na amri aliyokuwa akitoa. Kipindi alichotawala Catherine the Great kinachukuliwa kuwa ni Kipindi Muhimu katika historia ya Russia (Golden Age of Russia).

Aliamuru kujengwa kwa majengo mengi ya kifahari katika usanifu ambao ulipitishwa na Malkia huyo. Alibadilisha mwonekano wa Dola ya Russia. Aliunga mkono maoni ya kpindi cha mwangaza.

Catherine the Great alifariki dunia mnamo mwaka 1796 akiwa na umri wa miaka 67 kwa kiharusi kilichotokana na msongo wa mawazo.

0 Comments:

Post a Comment