Thursday, June 11, 2020

Unaijua Vita ya Fakhkh ya Juni 11, 786?

Juni 11, 786 AD kulizuka machafuko katika mji wa Makka, Saudia Arabia yaliyosababisha kuibuka kwa vita vya Fakhkh. Hassanid Alid zilikuwa ni koo mbili kutoka kwa Hassan ibn Ali na Ali ibn Abi Talib zilipigwa na Abassids ambao walikuwa ni wa ukoo wa Abbas ibn Abd al-Muttalib.

Huyu Abbas ibn Abd al-Muttalib alikuwa mjomba wa Mtume Muhammad S.A.W. Ukoo wa Abassids ulikuwa ukitawala kutoka Baghdad mji mkuu wa Iraq  hadi pwani ya Mediterania katika nchi za sasa ambazo ni Tunisia. Libya na Misri.

Sulayman ibn Abi Ja'far ambaye alikuwa miongoni mwa watoto mtawala al-Mansur (Abu Ja'far Abdallah ibn Muhammad al-Mansur) alipambana vikali na waungaji mkono wa Alids ambao walikuwa Washia waliotokea katika ukoo wa Ali ibn Abi Talib, mjini Makka.

Alids walikuwa wakiongozwa na Husayn ibn Ali ambaye alikuwa mjukuu wa Hassan ibn Ali. Katika historia miaka ya baadaye alifahamika kama Ṣāḥib Fakhkh yaani mtu wa Fakhkh.

Majeshi cha Abassid yaliwatandika vibaya wafuasi wa Alid katika bonde la Fakhkh karibu na Makka. Husayn na wenzake walikamatwa na Abassid huku miongoni mwa Alid aliyefahamika kwa jina la Idris ibn Abdallah alikimbia vita hivyo na kwenda zake huko Maghreb (Morocco) ambako alifanikiwa kuanzisha kizazi chake (Idrisid). Kwa maana hiyo ushindi ulikwenda kwa ukoo wa Abassid.


0 Comments:

Post a Comment