Monday, June 15, 2020

Mfahamu First Lady Abigail Adams

Taifa la Marekani lilipata uhuru wake mnamo mwaka 1776 na cheo hiki cha First Lady hakikuwepo hapo awali hadi Aprili 30, 1789 ikiwa ni miaka 13 baada ya uhuru. Rais wa kwanza wa Marekani alifahamika kama George Washington ambaye alikalia kti hicho kutoka mwaka 1789 hadi mwaka 1797. 

Huyu ndiye anayechukuliwa kuwa mwasisi wa jina hilo la 'First Lady'. Mwanamke wa kwanza kupata cheo hicho alikuwa Martha Washington ambaye alikuwa mke wa George wa Washington. 

Baadaye Wamarekani walipendelea kumwita Lady Washington. Hivyo hata marais wengine walipokalia kiti hicho wake zao waliitwa First Lady. Hadi sasa inatumika hivyo kama ilivyo kwa marais wote duniani. 

Baada ya kuondoka madarakani Washington kiti chake kilichukuliwa na John Adams ambaye alikuwa mwanasiasa, mwanasheria, mwanadiplomasia, mwandishi na mwanzilishi wa taifa hilo akiwa na kina George Washington katika harakati za kulitengeneza taifa hilo. John Adams alitawala kipindi kimoja tu kutoka 1797 hadi 1801. 

Alifariki dunia Julai 4, 1826 akiwa na umri wa miaka 90 huko Quincy Massachussets. Enzi za uhai wake alimuoa Abigail Adams mnamo mwaka 1764 na first lady huyu alifariki dunia mnamo Oktoba 28, 1818 akiwa na umri wa miaka 73. 

Abigail anachukuliwa kuwa ni miongoni mwa wapigania uhuru wa taifa la Marekani pia First second lady na second First Lady. Abigail alimzaa mtoto wa kiume John Quincy Adams ambaye alikuja kuwa Rais wa sita wa taifa hilo kutoka mwaka 1825 hadi 1829. 

Hivyo Abigail na Barbara Bush nchini Marekani ambao pekee wameweka rekodi ya kuwazaa watoto ambao walikuja kuwa Marais wa taifa hilo. Barbara Bush alikuwa First Lady kutoka mwaka 1989 hadi 1993 kwa rais wa 41 wa taifa hilo George H. W. Bush. 

Barbara Bush alimzaa George Walker Bush aliyekuwa Rais wa 43 wa Marekani. Pia mwanamke huyu alikuwa mbele katika kutaka wanawake wapewe nafasi katika katiba ya taifa hilo. 

Mnamo Machi 31, 1776  Abigail Adams alimwandikia mumewe barua na barua hiyo aliipeleka katika bunge akisisitiza maneno haya, “ Wakumbuke wanawake na uwe mkarimu na neema kwao kuliko baba zako. Usiweke nguvu kama hiyo isiyo na kikomo mikononi mwa wanaume. Kumbuka, wanaume wote wangekuwa madhalimu kama wangeweza. Ikiwa uangalifu na umakini hautawekwa kwa wanawake, tumedhamiria kuchochea uasi, na hatutajifunga kwa sheria zozote ambazo hatuna sauti wala uwakilishi.”  

Abigail aliandika barua hiyo wakati huo akikaa Philadelphia, Pennsylvania. First Lady huyo alikuwa akimwandikia barua nyingi mumewe ambapo uandishi wa barua zake zilitumika kama ushahidi wa kuanzisha vita vya ukombozi iliyopiganwa dhidi ya Waingereza kutoka mwaka 1775–1783 ambapo makoloni 13 yaliungana kupambana na utawala huo wa kikoloni. 

Vita hivyo vya kudai uhuru vilipiganwa kwa miezi 8, miezi 4 na siku 15 na ndipo Marekani ikawa imara hadi sasa. Kwa mara ya kwanza Abigail walikutana akiwa na umri wa miaka 15 hiyo ilikuwa mwaka 1759.   

Mnamo Oktoba 25, 1764 walifunga ndoa na ndani ya miaka 12 walifanikiwa kuzaa watoto sita. baada ya muda kupita na harakati mbalimbali zikiendelea mnamo Machi 4, 1797, huko Philadelphia Abigail alitunukiwa cheo cha kuwa First Lady wakati mumewe akiapishwa kuwa Rais wa pili wa taifa hilo. 

0 Comments:

Post a Comment