Juni 12, 1982 alifariki mwanasayansi wa Austria Karl von
Frisch. Frisch alikubuhu katika masuala ya madawa (physiology/medicine) na
etholojia. Ni mshindi wa tuzo ya Nobel katika kategori hiyo mwaka 1973.
Mwaka huo huo alishinda na wenzake wawili Nikolaas Tinbergen na
Konrad Lorenz. Alifariki jijini Munich nchini Ujerumani akiwa na umri wa miaka
95 (alizaliwa Novemba 20, 1886 huko Vienna, Austria). Frisch alifanya kazi
nyingi za kisayansi lakini alikuwa maarufu kwa utafiti wake kwenye nyuki na
namna ya utengenezaji wa asali.
Frisch ndiye wa kwanza kurekodi tukio la namna nyuki
wanavyocheza (waggle dance) pindi wanapotafuta mali ghafi kwa ajili ya
utengenezaji wa asali. Katika nadharia yake mnamo mwaka 1927 kupitia kitabu
chake cha ‘Aus dem Leben der Bienen’ ikiwa na maana ya ‘The Dancing Bees’ yaani
‘Nyuki Wanaocheza’ alionyesha utafiti huo ambao hakukubaliwa haraka lakini
baaadaye aliukubali.
Frisch alijikita katika kategori ya kuwaangalia viumbe hao na
tabia zake (etholojia) ikiwamo namna wanavyohama kutoka sehemu moja kwenda
nyingine. Hapo ndipo Frisch alipowaangazia nyuki katika kategori ya
utengenezaji wa asali. Nyuki aliowaangazia ni wale wa aina ya Carniolan
kitaalamu wanajulikana ‘Apis mellifera carnica’ ambao wanapatikana kwa wingi
huko Slovenia, maeneo ya Kusini ya Austria, pia baadhi ya maeneo nchini Croatia,
Bosnia & Herzegovina, Serbia, Hungaria, Romania, na Bulgaria.
Frisch aligundua kuwa nyuki wanaweza kutofautisha mimea mbalimbali
inayokua na harufu yao. Kwa kushangaza, unyeti wao kwa ladha "tamu" una
nguvu kidogo tu kuliko kwa wanadamu. Aliwafundisha nyuki kula kwenye sahani ya
maji ya sukari iliyowekwa kwenye kadi ya rangi. Frisch alibaini kuwa nyuki
watatembelea zaidi kadi za rangi ya bluu kuliko kijivu.
Pia Frisch alibaini kuwa nyuki wana saa ya ndani na njia tatu
tofauti utunzaji wa wakati. Ikiwa nyuki anajua mwelekeo wa mahali pa kula
unaopatikana wakati wa safari ya asubuhi, inaweza pia kupata eneo sawa, na
wakati unaofaa ambapo chanzo hiki hutoa chakula, wakati wa mchana hutegemea na mahali
jua lilipo.
0 Comments:
Post a Comment