Black Death ni janga la pili kubwa kulikumba bara la Ulaya
katika kipindi cha kati, janga la kwanza ilikuwa ni njaa. Black Death ilitokea
kati ya mwaka 1346 hadi 1353.
Inakadiriwa kuwa ugonjwa huo uliua asilimia 30 hadi 60 ya
watu barani Ulaya. Kwa ujumla ugonjwa huo wa tauni ulipunguza idadi ya watu
hapa ulimwenguni wakati huo kutoka milioni 475 hadi milioni 350 katika karne
hiyo ya 14. Watu wapatao milioni 75 hadi 200 walifariki dunia kutokana na
ugonjwa huo wa tauni barani Ulaya.
Mnamo Oktoba mwaka 1347 ugonjwa wa tauni ulifika barani Ulaya
baada ya meli 12 kutoka Bahari Nyeusi zilipotia nanga katika bandari ya Messina
huko Sicily nchini Italia. Watu walistaajabishwa na walichokiona siku hiyo
kwani ilikuwa ni hali ya kuogofya.
Wengi wa manahodha na baadhi ya watu walikuwa wamefariki
dunia na wachache wakiwa hai lakini wakiwa hoi.
Miili ya waliokufa ilikuwa ikivuja damu na usaha ikitoa halafu mbaya.
Mamlaka za Sicily ziliamuru meli hizo zitokea katika bandari
hiyo lakini amri hiyo ilikuwa imechelewa. Miaka mitano baadaye watu wapatao
milioni 20 barani Ulaya walipoteza maisha, ikiwa ni theluthi moja ya watu wa
bara hilo.
Ugonjwa wa tauni unafikiriwa kuwa asili yake ni barani Asia
ambako miaka zaidi ya 2000 ulianza na kusambaa kwake kulitokana na biashara
ambayo ilikuwa ikifanyika kupitia njia ya Mashariki ya kati hadi Mashariki ya
mbali kwa kutumia meli.
Tafiti mbalimbali za miaka ya hivi karibuni zinaonyesha kuwa
ugonjwa huu ulianza barani Ulaya mapema mwaka 3000 KK. Katika miaka ya mwanzoni
ya 1340 tauni ilizikamata China, India, Uajemi, Syria na Misri.
Inaelezwa kuwa meli zile zilipotia nanga viroboto walionekana
katika meli hiyo na kwamba walikuwa wakiishi kwenye panya weusi ambao
walijificha kwenye meli za wafanyabiashara wa Genoa.
0 Comments:
Post a Comment