Sunday, June 14, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Kurt Waldheim ni nani?

Juni 14, 2007 alifariki dunia mwanasiasa na mwanadiplomasia wa Austria Kurt Josef Waldheim.  Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Alizaliwa Desemba 21, 1918 huko Sankt Andrä-Wördern, Austria. 

Alifariki dunia kwa maradhi ya moyo na mazihi yake yalifanyika Juni 23 mwaka huo huo  katika Kanisa la Stephen na alizikwa katika makaburi ya Marais wa taifa hilo. 

Alikuwa Katibu Mkuu wa nne wa Umoja wa Mataifa kutoka mwaka 1972 hadi 1981. 

Aliingia tena katika kinyang'anyiro cha urais wa Austria mnamo mwaka 1986 baada ya kushindwa katika awamu ya kwanza. Wakati wa kampeni za kuwania nafasi hiyo alibanwa mbavu kutokana na huduma yake wakati akiwa Afisa wa Kijeshi katika Vita vya Pili vya Dunia huko Thessalonike, Ugiriki na Yugoslavia. Kipindi hicho alikuwa askari wa Jeshi la Adolf Hitler (mwavuli wa Nazi).  

Alimaliza kuhudumu katika nafasi hiyo mwaka 1992 na mwaka huo huo akatunukiwa kuwa mjumbe wa heshima ya K.H.V. Welfia Klosterneuburg ambayo hupewa mwanafunzi wa Kanisa la Roman Katoliki ambapo yeye alipewa heshima hiyo.  

Mnamo mwaka 1994 Papa Yohana Paulo II alimtunuku Pian Order ambayo iliasisiwa na Papa Pius IX miaka ya 1560 kwa ajili ya kutambua mchango na uaminifu wake katika Kanisa Katoliki. 

Mapema mwaka 1941 Waldheim alikuwa miongoni mwa maafisa wa Kinazi katika Kikosi cha Mashariki ambapo aliongoza mapambano. Mnamo Desemba 1942 alijeruhiwa katika vita hivyo. Huduma yake katika Wehrmacht (majeshi muungano ndani ya Nazi) kutoka mwaka 1942 hadi 1945 ilikuwa ndio mjadala mkuu wakati akiwania urais wa Austria.

Katika autobiography yake alisema aliondolewa katika kuongoza kikosi hicho katika mstari wa mbele hadi mwishoni mwa vita hivyo na ndipo alipopata fursa ya kwenda kusoma masuala ya sheria katika Chuo Kikuu cha Vienna. Akiwa huko alioa. 

Baada ya kuchapishwa kwa autobiography yake, nyaraka na ushahidi ulionekana kuwa huduma yake katika jeshi iliendelea hadi mwaka 1945 ambapo alikuja kupanda cheo na kuwa Oberleutnant ikiwa ni nafasi ya juu ya Luteni katika jeshi la Ujerumani (Bundeswehr), Austria na Uswisi. 

Baada ya kushindwa Urais wa Austria Waldheim aliingia katika kusaka nafasi kwenye Umoja wa Mataifa ambako alikuwa akiungwa mkono na Urusi. Katika mizunguko miwili ya kwanza alipata uungwaji mkono. Hata hivyo alikuwa akipingwa na China, Uingereza na Marekani. 

Katika mzunguko wa tatu wa uchaguzi wa kumpata Katibu Mkuu wa UN, Waldheim alishinda kwa bahati baada ya wajumbe wa kudumu wa UN waliposhindwa kukubaliana kwa kutumia kura ya Veto. Waldheim alikalia kiti kilichoachwa na U Thant mnamo mwaka 1972. 

0 Comments:

Post a Comment