Friday, June 5, 2020

Juni 5: Time for Nature

Mnamo Juni 5, 1974 kwa mara ya kwanza dunia iliadhimisha siku ya Mazingira na siku hiyo ilifanyika  ulimwenguni kwa shughuli mbalimbali. Hadi sasa siku hii hufanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya kutoa hamasa ya kuendelea kutunza mazingira kwa kizazi cha leo na kijacho.

Tangu ilipozinduliwa mwaka wa 1974, Siku ya Mazingira Duniani imepanuka kuwa jukwaa la kimataifa la kuhamasisha na kushughulikia masuala nyeti kuanzia uchafuzi wa bahari na ongezeko la joto duniani hadi uhifadhi wa mazingira na uwindaji haramu. Mamilioni ya watu wameshiriki katika miaka iliyopita, hivyo kusaidia kubadilisha jinsi tunavyotumia rasilimali pamoja na kuchangia katika sera ya kitaifa na kimataifa ya mazingira.

Siku ya Mazingira Duniani imejumuisha mataifa madogo zaidi na yaliyoachwa nyuma kimaendeleo huku ikishughulikia mada nyeti zaidi: kuanzia uhifadhi wa mazingira hadi biashara haramu ya wanyamapori.

Umoja wa Mataifa ulitenga Juni 5 kuwa Siku ya Mazingira Duniani mwaka wa 1972. Miaka miwili baadaye, siku hii ilisherehekewa mara ya kwanza kauli mbiu ikiwa “Dunia Moja Pekee.” Mwaka 2020 siku hii imepambwa na kauli mbiu ya 'Time for Nature,' 


0 Comments:

Post a Comment