Dunia ni sayari pekee kwenye himaya ya sayari zilizopo chini ya jua ambayo jina lake halitokani na majina ya "Miungu wa Dola" ya Kigiriki au ya Kirumi. Pia Dunia hii ambayo viumbe hai tunaishi kuna maajabu mengi na mengine inakuwa vigumu kuamini.
Dunia yetu imejaa mambo kadhaa ya ajabu ambayo hata hatuyafikirii. Watu wachache wanajua ujumbe mfupi unavyopita kutoka simu moja ya kiganjani hadi nyingine na wachache zaidi wanajua kwa nini matairi ya gari ni meusi? Maajabu haya kuna yale yanayotokana na asili yake lakini kuna mengine ni akili tu ya binadamu kuyatengeneza. Sasa basi umewahi kusikia kuhusu marathon ya kupigana busu? Inawezekana ikawa ni jambo geni kwa wakazi wa ukanda wa Afrika Mashariki lakini sio kwa watu wa Asia hususani Thailand.
Mnamo Februari
12-14, 2013 katika mji wa Pattaya uliopo katika pwani ya Ghuba ya Thailand,
umbali wa kilometa 100 kutoka mji mkuu wa taifa hilo wa Bangkok, wapenzi
Ekkachai Tiranarat (44) na mke wake Laksana (33) waliweka rekodi ya kupigana
busu. Busu hilo nimelipa jina la ‘Ekkachai Tiranarat’
Tiranarat alikuwa
mlinzi wa hospitali na Laksana akiwa ni mama wa nyumba maisha yalibadilika
kutoka kwenye umaskini hadi kuwa watu wenye hadhi na dunia haitakuja kuwasahau
kwa rekodi waliyoweka.
Mji wa Pattaya ni
miongoni kati ya miji ya starehe ambayo ina hali ya hewa ya kitropiki na
kiangazi nchini humo. Desemba hadi Februari ni wakati ambao huwa ni majira ya
joto na kiangazi, Mwezi Machi na April ni majita ya joto na unyevunyevu kutoka
mwezi Mei hadi Novemba ni majira ya joto na mvua nyingi.
Tiranarat na mkewe
waliweka rekodi ya ‘Kissmarathon’ wakitumia saa 58 dakika 35 na sekunde 58
(dakika 3,515 na sekunde 58) katika tukio lililoandaliwa na ‘Ripley’s Believe
It or Not’.
Kwa kifupi ni
kwamba washindi hawa walikaa siku mbili wakiwa wanapigana busu pasipo kuachana.
Katika Makumbusho hayo ya Ripley mjini Pattaya inasalia kuwa alama muhimu ya
kumbukumbu ya Kissmarathon kushikilia rekodi ya dunia ambayo ni takribani miaka
saba haijavunjwa popote pale ulimwenguni.
Washindi hao walivunja
rekodi iliyopita ya saa 50 dakika 25 na sekunde 1 iliyowekwa na raia wa
Thailand Nonthawat Charoenkaesornsin na Thanakorn Sitthiamthong. Siku ya
shindano hilo walikuwepo kutaka kuweka rekodi zaidi lakini hawakufanikiwa
kuwazidi Tiranarat na Laksana kwani walizimia dakika mbili kabla ya Tiranarat
na Laksana.
Siku ambayo
Tiranarat na Laksana wanaibuka washindi wa shindano hilo ulikuwa ni usiku wa
mwisho wa Siku ya Valentine.
Tiranarat na
Laksana walijishindia kitita cha fedha za Thailand baht 100,000 ambazo ni sawa
na shilingi za Tanzania milioni 7.6 pia washindi hao walipewa pete za almasi
kila mmoja.
Uongozi wa
waandaji wa shindano hilo kupitia kwa Makamu wa Rais Sompron Naksuetrong
aliviambia vyombo vya habari, “Walikuwa wamechoka kwkasababu hawakulala kwa
siku mbili na nusu, walikuwa wamesimama muda wote, na ndio sababu wako dhaifu.”
ILIKUWAJE WAKAWEKA
REKODI HIYO?
Waratibu wa
shindano hilo la ‘Kissmarathon’ waliweka vigezo ambapo kigezo cha kwanza
kabisa kilikuwa ni kwamba busu lilitakiwa kuendelea bila kusimama na lips
zilitakiwa wakati wote ziwe zimegusana baina ya wawili hao. Endapo lips
zingejiacha au kutogusana basi washiriki wa mashindano hayo wangeshindwa
kufuzu.
Pia washiriki
walitakiwa kuwa na umri unaoruhusu mambo hayo yaani kufuatana na kanuni za
Thailand wale waliokuwa wameoana au ni wapenzi. Halafu washiriki hao walitakiwa
kuwa macho muda wote kama ‘mwaaa…mwaaaa….mwaaa…’ ilikuwa iendelee bila
kupumzika na ukumbuke walikuwa wakifuatiliwa kwa karibu na kamera.
Washiriki
walitakiwa kuwa wamesimama muda wote wa shindano hilo na hawakutakiwa kuwa
wameongezewa nguvu kama kuwekewa mto au kuegemea sehemu yoyote au watu. Pia
kigezo kingine kilikuwa hakuna mapumziko hata kidogo maana yake ni mwanzo
mwisho. Pia hawakutakiwa kuvaa taulo za kunyonya jasho (adult diapers) na
mwisho kabisa ilikuwa washiriki hawakutakiwa kuondoka katika eneo la tukio
mpaka uwezo wako utakapofikia.
Sipati picha kama
ingekuwa hapa Tanzania shindano kama hili lingekuwaje kwa washiriki. Midomo
ingevimbaje? Nafahamu mwingine ataanza kusema hizo ni tamaduni za kimagharibi
lakini Thailand ipo Asia lakini katika rekodi ya ‘Kissmarathon’ kwa kweli
wakaona isiwe taabu.
Unaweza kuona washiriki hawa waliingia kwenye mfungo mrefu wa bila kuonja chochote chakula zaidi ya….
0 Comments:
Post a Comment