Juni 30, 350 alifariki dunia mtawala wa Rumi mwite
Kaisari Nepotianus. Kaisari huyu alifariki dunia kwa kuuawa baada ya kukalia
kiti cha kuliongoza taifa hilo kwa siku 28 tu.
Jina lake halisi ni Flavius Julius Popilius Nepotianus
Constantinus. Nepotianus alikuwa ni wa ukoo wa Constantino ambaye alitawala
isivyo halali baada ya kuchukua nafasi hiyo kimabavu. Waliofanikisha jaribio la
kummaliza kiongozi huyo walikuwa ni kundi jingine lililokuwa na tamaa ya
kushikilia usukani wa kuliongoza taifa hilo.
Mauaji hayo yalifanywa na Jenerali Marcellinus wa
kikosi au wafuasi wa Magnentius. Baada ya kufanya mauaji hayo Magnentius alishika
utawala huo hadi mwaka 353.
Siku ya kukalia kiti hicho ilikuwa Juni 3, 350 ambapo Nepotianus
aliingia jijini Rome akiwa na bendi ya waliokuwa wakimuunga mkono. Kwa kawaida
kila mji wakati huo ulikuwa na kiongozi alitekuwa akifahamika kama Praefectus
urbi.
Sasa wakati Nepotianus alipokuwa akiingia jijini humo
Praefectus urbi wa wakati huo alikuwa
Titianus (Anicius) ambaye alishindwa kumzuia Nepotianus. Pia inaelezwa Titianus
alikuwa mfuasi wa Magnentius , hivyo kuona mambo yameharibika alikimbia mji na
Nepotianus akashikilia mahali pale.
Magnentius kwa haraka sana akajibu mapigo hayo kwa
kumpeleka mtu aliyekuwa akiijua sharia vizuri na aliyemwamini Marcellinus huko
jijini Rome.
Kwa mujibu wa mwanahistoria wa Rumi aliyefahamika kwa
jina la Eutropius alisema, Nepotianus aliuawa wakati akipambana Juni 30, 350 na
kichwa chake kilitundikwa katika fimbo ndefu na ikatembezwa katika viunga vya
jiji la Rome ili watu wajionee.
0 Comments:
Post a Comment