Kitambi ni mafuta ya ziada yanayojikusanya katika sehemu ya tumbo. Hii
inatokana na kula chakula kingi na kisicho na ubora, pia kuishi maisha ya kibwanyenye
yanayokunyima fursa ya kufanya mazoezi. Mafuta yanayofanya kitambi huweza
kujengeka chini ya ngozi, au ndani kabisa ya tumbo yakizunguka viungo kama
tumbo, utumbo na ini.
Mafuta haya, hususan yale yaliyo ndani ya tumbo ni hatari kwa afya zetu.
Ikumbukwe pia kwamba, kitambi huwa na mwonekano wake kutokana na misuli ya
tumbo kuwa legelege. Hii husababisha mafuta yaliyo tumboni kuusukuma ukuta wa
tumbo kiurahisi hivyo kutengeneza shepu ya mbinuko.
PUNGUZA SUKARI NA VYAKULA VYA WANGA: Kutokula vyakula vya wanga kunasaidia kupunguza njaa hivyo kunafanya upunguze kiasi cha chakula unachokula. Kwasababu miili yetu hutumia wanga kutengeneza nguvu ya kujikimu na shughuli zote za mwili, uhaba wa fungu hili la chakula mwilini husababisha miili yetu kutafuta mbadala wa kutengenezea hii nguvu kwa ajili ya uhai. Kwa hiyo miili yetu huamua kutumia glycogen na mafuta ambayo yanakuwa yametunzwa mwilini ambayo yanatufanya tuonekane wanene ili kutengeneza nguvu kwa ajili yetu.
Mafuta yanapotumika
kutengeneza nguvu badala ya wanga ndipo tutaona mabadiliko ya kupungua
mwili. Pia kupunguza vyakula vya
wanga kunaleta kupungua kwa hormone ya insulin. Hii inasababisha figo kuondoa
chumvi na maji mwilini hivyo kama tumbo limejaa linapungua haraka sana. Mara
nyingi watu wanapata tumbo kujaa na wanadhani ni gesi tu inasababisha lakini
kula vyakula vingi vya wanga na chumvi nyingi kunasababisha mwili ujae maji
hivyo tumbo linakuwa limechomoza sana.
KULA PROTINI, MBOGA MBOGA NA MAFUTA YA MIMEA: Hakikisha kila mlo
wako una protein, kuanzia chakula cha asubuhi!. Chai na chapati/maandazi/vitumbua/cutlets/mihogo/viazi/keki
n.k achana navyo kabisa. Kila mlo lazima uwe na protein na mbogamboga. Mfano
wa vyakula vyenye protini; Nyama: Ya ng’ombe, kuku, mbuzi n.k Samaki: Salmon,
sato, sangara, prawns n.k Mayai: Ya kuku wa kienyeji ni mazuri zaidi; Mbegu na
karanga: Mbegu za chia, karanga za almonds. Utajisikia
kushiba kwa muda mrefu, hamu ya kula kula hovyo au kula usiku wa manane vitapungua
sana hivyo kukufanya kula kwa kiasi.
FANYA MAZOEZI YA KUNYANYUA UZITO: Ukipunguza
vyakula vya wanga ni muhimu kutopunguza mafuta aina hii, ukipunguza mafungu
haya mawili ya chakula kwa wakati mmoja utapata tabu sana na hautafurahia
healthy lifestyle yako. Utachoka na kukosa nguvu muda mwingi kwahiyo usisahau
kutumia healthy fats kwenye milo yote. Kufanya mazoezi ya weight
lifting matokeo yatakuwa makubwa zaidi. Kama hauwezi kunyanyua uzito basi
unaweza kufanya mazoezi ya cardio kama jogging, kuendesha baiskeli, kuogelea, n.k
Utaongezeka uzito kidogo tu ambao unasababishwa
na maji kwasababu kula vyakula vya wanga kunafanya mwili ushikilie maji mengi,
ukipunguza tena vyakula hivi figo itatoa hayo maji na huo uzito kidogo
ulioongezeka utatoka. Kwa hiyo usiogope/usishtuke/usishangae! Ni kitu rahis tu.
Jitahidi kujidhibiti (self control) usipitilize siku moja tu ya kula hivi
vyakula vya wanga, na pia usifanye maajabu kwa kula hadi kupitiliza kama kulipizia.
Ni muhimu kujifunza kuwa na kiasi. Kula kadri ya mahitaji usipitilize.
KULA TARATIBU: Hili huwa linawashinda wengi
hususani jamii ya Watanzania kutokana na kushindwa kupangilia vizuri ratiba ya
kula na hujikuta kazi zimembana na hatimaye kula haraka haraka. Imekuwa ni
tabia ambayo imekuwa ikichukuliwa kama mtu huyu anajali sana muda kwa kulak
wake haraka jambo ambalo sio kweli. Kula taratibu kunasaidia kumeng’enya
chakula chako vizuri lakini pia kunafanya ule chakula kidogo na kushiba haraka.
PATA USINGIZI WA KUTOSHA: Kupata Usingizi wa
kutosha kutakuepusha na kutaka kula chakula usiku sana, unapowahi kulala
unawahi kula hii inasaidia mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi yake vizuri.
0 Comments:
Post a Comment