Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Tuesday, March 31, 2020

Watoa huduma kwa jamii hatarini kueneza Covid-19


Afisa Afya wa Mkoa wa Kilimanjaro Jonas Mcharo
 Watoa huduma katika taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali wapo hatarini kueneza maambukizi ya virusi vya Covid-19 endapo hawatazingatia tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona.

Hayo yalibainishwa na Afisa Afya wa Mkoa wa Kilimanjaro Jonas Mcharo, wakati akizungumza kwenye semina ya siku nne inayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na  kuwashirikisha Wataalamu wa Afya na Waandishi wa habari mkoani humo.

Mcharo alisema kumekuwa na tahadhari mbalimbali za kuchukua ikiwamo uvaaji wa mask na gloves ikiwa ni sehemu ya kujikinga lakini zote hazijathibitisha kitaalamu kama zinaweza kupunguza maambukizi ya kusambaa kwa virusi vya Covid-19.

“Kunawa mikono kwa sanitizers ndiko ambako Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha uvaaji huu wa mask na gloves bado haujathibitishwa kwani virusi hawa wanaambukiza kwa kasi kupitia kugusa na ndio sababu tunasisitiza kunawa mikono,” alisema Mcharo.

“Wahudumu wanaolengwa hapo ni katika maeneo ya kazi kama benki, madaktari wenyewe wanapaswa kuzingatia tahadhari; haishauriwi kuvaa mask hata kama utavaa je ni za ubora unaotakiwa?” alisisitiza.

Pia Mcharo aliongeza kuwa wahudumu wa benki wapo katika hatari ya kuambukiza wengine kutokana na uvaaji wa gloves zao wanapohudumia wateja pasipo kubadilisha.

“Kuna wahudumu wa benki wanavaa gloves ukiangalia ni kwamba anajikinga yeye je wewe kwani anawahudumia wengi bila kubadilisha. Sisi wenyewe madaktari tunavaa gloves kwa kila mgonjwa mmoja, wanapaswa kulitambua hilo,” aliongeza Mcharo.
Alisema mara nyingi virusi vya havina kinga ya chanjo,  silaha kubwa ya virusi ni kupambana na chanjo, hivyo  ni  vema Udhibiti wa  Maambukizi ya virusi ya ugonjwa wa Covid-19 mahali pa kazi ukadhibitiwa.

Alifafanua kuwa wataalamu wa afya wanahudumia wana jamii hivyo kama hawajapata elimu ya kujinga na virusi hivi  vinaweza kusababishwa kuenezwa kutoka kwa mtoa huduma za afya  kwenda kwa mgonjwa. kudhibiti maambukizi  kwenda kwa jamii.

Hata hivyo aliwatoa wasiwasi watanzania kuhusu juhudi ambazo serikali imekuwa ikiendelea kuzichukua dhidi ya ugonjwa huo akisisitiza kutosimamia habari za uongo zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuhusu hali ya ugonjwa huo kwani watoaji wakuu wa taarifa ni Waziri wa Afya, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya Zanzibar.

Wataalamu wa Afya kutoka wilaya za Siha, Rombo Hai, Same, Moshi DC, Mwanga na Manispaa ya Moshi ndio wanaopata semina hiyo kuhusu namna ya kupambana na maambukizi ya Covid-19.

STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 30, 2020


















Ndugu wa Aliyefariki kwa Corona Mloganzila azungumza


Ndugu wa mtanzania aliyekufa kwa ugonjwa wa Corona  amesema mdogo wake, Iddy amefariki kwa ugonjwa wa corona leo alfajiri ya Machi 31, 2020 katika kituo cha matibabu ya wanaougua ugonjwa huo kilichopo Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam. 

Ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu taarifa za msiba huo. Iddy ni Mtanzania wa kwanza kufariki dunia kwa ugonjwa huo nchini.

Taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyotolewa na Waziri Ummy Mwalimu imethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo hicho.

"Marehemu ni Mtanzania mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi mengine. Tunamuomba Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, na tunatoa pole kwa familia, ndugu jamaa wa marehemu, ilisomeka taarifa ya Waziri Ummy.

Amesema hadi sasa watu 19 wameambukizwa corona, aliyepona ni mmoja na kifo ni kimoja. Jana, Ummy alieleza kuwa kuongezeka kwa wagonjwa watano wa corona wakiwamo wawili waliokuwa wakifuatiliwa na kufanya idadi ya waliobainika kuwa na maambukizi nchini kufikia 19. 

Amesema mgonjwa wa pili ni mwana mke mwenye miaka 21 Mtanzania ambaye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa. Kuhusu mgonjwa wa tatu, Ummy amesema ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 Mtanzania ambaye pia ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatiliwa.


MAKTABA YA JAIZMELA: Jesse Owens ni nani?


Machi 31, 1980 alifariki dunia mwanariadha wa kimataifa raia wa Marekani Jesse Owens. Jina lake halisi ni James Cleveland.

Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 66 huko Tucson Arizona kwa ugonjwa wa saratani ya mapafu. Jesse Owens alianza uvutaji wa sigara akiwa na umri wa miaka 32 na inaelezwa kwa siku alikuwa anavuta pakiti moja.

Kwa miaka 35 tangu wakati huo alikuwa akivuta sigara. Mnamo Desemba 1979 alipelekwa hospitalini ambako alilazwa kuanzia hapo alikuwa akienda na kutoka kutoka na maradhi hayo. Alifariki dunia akiwa amezungukwa na mkewe pamoja na wanafamilia wengine.

Jesse Owens alizikwa katika makaburi ya Oak Woods  yaliyopo Chicago. Japokuwa Rais Jimmy Carter alipuuzia maombi ya Owens kuhusu mgomo wa Olimpiki lakini kiongozi huyo wa zamani alitoa rambirambi zake akisema, “Inawezekana hakuna mwanariadha aliyekuwa nembo ya mapambano dhidi udhalimu, umaskini na ubaguzi wa rangi kama Jesse Owens.” Jesse Owens alikuwa mwanariadha wa mbio za uwanjani maarufu track and field.

Aliweka rekodi ya kutwaa medali nne katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 1936 iliyofanyika mjini Berlin katika Ujerumani ya Kinazi iliyokuwa chini ya Adolf Hitler. Owens alikuwa mahiri katika kukimbia na miruko ya chini.

Enzi zake alijulikana sana na alichukuliwa kuwa ni mwanariadha mkubwa na maarufu katika historia yam bio za uwanjani. Aliweka rekodi tatu za dunia chini ya saa moja kwenye tukio la mbio la mwaka 1935 lililofahamika kwa jina la Big Ten Track  lililofanyika Ann Arbor huko Michigan. Katika tukio hilo lilifahamika  kama “The Greatest 45 minutes ever in sport.” 

Owens alishinda medali nne katika michuano ya Olimpiki mjini Berlin katika mita 100, mita 200, miruko ya chini na mbi za vijiti mita 100. Huyu ni mwanariadha aliyefanikiwa sana katika michuano hiyo na pia kama mtu mweusi.

Kutokana na kuonyesha uwezo huo alitunukiwa heshima iliyokuwa inatolewa na Adolf Hitler ya Aryan Supremacy licha ya kwamba hakuweza kualikwa katika ikulu ya Ujerumani kushikana mkono na Hitler.

Pia katika kutambua mchango wake nchini Marekani  kuna tuzo ya Jesse Owens kwa wanariadha wanaofanya vizuri katika mbio za uwanja ambayo hutolea kila mwaka.

ESPN ilimweka katika nafasi ya sita katika wanamichezo wakubwa katika Amerika ya Kaskazini waliowika kwenye karne ya 20 na alishika nafasi ya kwanza katika riadha.
Mnamo mwaka 1999 alikuwamo katika orodha ya Wanariadha bora wa karne ya 20 akishika nafasi ya sita.

Alizaliwa Septemba 12, 1913, alikuwa mtoto wa mwisho kati ya kumi waliozaliwa kwa baba mkulima Henry Cleveland Owens na mama Mary Emma Fitzgerald huko Oakville, Alabama. Akiwa na umri wa miaka tisa, familia yake ilihamia Cleveland, Ohio kwa ajili ya kutafuta fursa nzuri zaidi ya kazi.

Kipindi hicho Wamarekani weusi akali ya milioni 1.5 waliokuwa wakiishi Kusini walihamia maeno ya mijini na upande wa kaskazini kwa ajili ya shughuli za viwandani. Inaelezwa aliitwa Jesse baada ya mwalimu wake kumuuliza jina lake ambapo aliangalia katika daftari lake la kumbukumbu na kutamka J.C kifupisho cha James Cleveland.

Lakini mwalimu wake alifikiri kuwa James ametamka Jesse kutokana na lafudhi ya Kusini hivyo tangu wakati huo akaanza kuitwa Jesse badala ya James.

Enzi za uhai wake aliwahi kusema, “Niliiachia miguu yangu muda mchache katika ardhi iwezekanavyo. From the air, fast down, and from the ground, fast up.”





Bunge la Bajeti ya mwisho kwa Serikali ya Awamu ya Tano kuanza Machi 31


Mkutano wa 19 wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajia kuanza leo Machi 31 jijini Dodoma huku Spika wa Bunge Job Ndugai akitoa utaratibu maalum utakaotumika tofauti na ilivyozoeleka ili kujikinga na virusi vya ugonjwa wa Corona. 

Moja ya hatua zilizochukuliwa  awali ni kusitisha makundi ya wageni wanaokwenda bungeni kujifunza namna bunge linavyoendesha shughuli zake Ndugai  amesema kati ya wabunge wote, wabunge 150 hamsini ndiyo wataruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge ili kupunguza msongamano. 

Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maalum kwa ajili ya bajeti kuu ya serikali unatarajiwa kukamilika  Juni 31 mwaka huu.

Monday, March 30, 2020

Kilimanjaro Boxing Club mbioni kuandaa mapambano

Bondia Rodi Josephat wa Moshi, Kilimanjaro

Klabu ya Ndondi ya Mkoa wa Kilimanjaro imesema kifungo kilichokuwa kikiwazuia kuandaa mapambano mkoani hapa kinakaribia kufika mwisho baada kukamilisha usajili wa klabu hiyo.

Akizungumza na JAIZMELA mwanamasumbwi Rodi Josephat amesema kwa muda mrefu walikuwa na kikwazo cha kuandaa mapambano ya ngumi kama ilivyo mikoa mingine lakini kwa sasa wamefanikiwa baada ya hatua za usajili wa klabu hiyo kuwa katika hatua za mwisho.

“Tulishindwa kuandaa mapambano kwasababu tulikuwa hatujasajiliwa na shirikisho la ndondi, kwa sasa tumefikia hatua nzuri tulianzia wilayani, kisha mkoani na imeshafika taifa ambako tunaamini ikirudi tutakuwa rasmi tunaweza kuandaa mpambano yetu wenyewe,” amesema Rodi.

Mwanamasumbwi huyo ameongeza kuwa sehemu yao ya mazoezi iliyopo mjini Moshi ilizuiliwa kwa muda kutokana na kushindwa kutambulika na uongozi wa mkoani hapo hali ambayo iliathiri mwenendo wa mchezo huo mkoani hapo.

Aidha Rodi amewataka wanamasumbwi mkoani hapo kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya mapambano yatakayokuwa yakifanyika baada ya kukamilisha usajili huo.

Hata hivyo amewataka wadau waliokuwa wakijitokeza kwa kudhamini mapambano ya ndondi kurudi tena ikiwa ni sehemu ya kuuendeleza mchezo huo.

STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 23, 2020



MAKTABA YA JAIZMELA: Mama wa Malkia Elizabeth II ni nani?



Machi 30, 2002; Alifariki dunia Mama wa Malkia Elizabeth II. Jina lake halisi ni Elizabeth Angela Marguerite Bowes-Lyon
Huyu alikuwa ni mke wa mfalme George VI ambaye ni mama wa Malkia Elizabeth II na Princess Margaret wa Countess ya Snowdon. 

Huyu alikuwa ni Malkia wa Uingereza tangu alipotwaa mwaka 1936 hadi 1952 na kuanzia hapo alianza kuitwa mama wa Malkia Elizabeth. 
Mwaka 1952 alikabidhi taji la umalkia kwa binti yake na hiyo ndio sababu ya kuanza kuitwa jina hilo ili kuondoa mkanganyiko na jina la binti yake ambaye ni Malkia Elizabeth II. Mama wa Malkia Elizabeth wa pili alikuwa Malkia wa mwisho wa India. 

Alizaliwa katika familia ya kifalme ya Uingereza na alikuja kushika wadhifa huo alipoolewa mwaka 1923 pale Duke wa York na mtoto wa pili wa Mfalme George V na Malkia Mary. 

Mnamo mwaka 1936 mumewe hakutarajiwa kuwa Mfalme lakini alifikia hapo baada ya kaka yake Edward VIII kuondolewa katika nafasi hiyo kwani alikiuka amri ya kifalme pale alipomwoa mtalaka wa Kimarekani Wallis Simpson. 

Hivyo Elizabeth alikuwa Malkia. Enzi za utawala wake alishirikiana na mumewe kwenda katika ziara za usuluhishi wa kidiplomasia huko Ufaransa na Amerika ya Kaskazini ikiwa ni kabla ya kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939. 

Wakati wa vita hiyo Malkia Elizabeth alionyesha ukomavu na asiyeshindwa kwani alisimama katika hadhira ya Waingereza na kutoa hutuba nyingi za matumaini. 

Baada ya vita, hali ya mumewe ilidhoofu na aliachwa mjane akiwa na umri wa miaka 51 na binti yake ambaye alikuwa na umri wa miaka 25 ambaye ndiye malkia wa sasa ambaye anachukuliwa kushika wadhifa huo kwa muda mrefu alipokea taji hilo. Baaada kifo cha Malkia Mary mnamo mwaka 1953, Elizabeth alichukuliwa kuwa msimamizi wa familia ya kifalme. 

Alikuwa imara katika hadhira hata kabla ya kifo chake. Akiwa na miaka 101 na siku 238 aliaga dunia ikiwa ni miezi saba baada ya kifo cha binti yake mdogo Princess Margaret. 

Malkia wa sasa alizaliwa kwa jina la Elizabeth Alexandra Mary Windsor mjini London tarehe 21 Aprili 1926 kama mtoto wa kwanza wa mfalme George VI wa Uingereza na Elizabeth Bowes-Lyon.
Malkia Elizabeth II ni mkuu wa Jumuiya ya Madola yeye ni pia mkuu wa dola wa nchi za Antigua na Barbuda, Australia, Bahamas, Barbados, Belize, Canada, Grenada, Jamaica, New Zealand, New Papua Guinea, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent, Visiwa vya Solomon, Tuvalu, Ufalme wa Muungano wa Uingereza na Ireland ya Kaskazini. 

Alipokea taji katika ibada rasmi tarehe 2 Juni 1953 kwenye kanisa la Westminster Abbey. Katika nchi zote anaposhika cheo hana mamlaka ya kiserikali anatawala kama mfalme wa kikatiba katika muundo wa serikali ya kibunge.



Sunday, March 29, 2020

Bomoa bomoa Siha kwa wasiozingatia sheria


Wananchi   wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa isiyo ya lazima.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Jani, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa Sanya Juu  ambao walifika  ofisini kwake kwa ajili ya kutoa malalamiko yao ya kuwepo kwa ujenzi holela usiofuata utaratibu  unaoendelea katika mji huo.

Makamu mwenyekiti huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya  Sanya mjini alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili kuepuka ukiukwaji wa sheria za nchi katika ujenzi wa makazi yao.

“Niwaombe wananchi  wa wilaya ya Siha kuzingatia sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwa sababu tu watu wamekiuka sheria zilizopo,”alisema

Jani alifafanua kuwa  yapo malalamiko, mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa  mengine kwa barua ofini kwake  ikiwemo barua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa  majina ya Zakaria Materu, akilalamikia ujenzi  usiofuata taratibu.

“Wapo  baadhi ya watu wamejenga vibanda vya biashara huku wengine wakijenga  ukuta  kwenye hifadhi ya barabara inayoelekea  kwenye majengo ya halmashauri ya zamani na kuifanya  barabara hiyo kupitika kwa shida licha ya kuagizwa kuibomoa lakini hadi leo agizo hilo halijatekelezwa,”alisema.

Alisema ni vyema Wananchi wakazingatia sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi ili kuepuka ukiukaji wa sheria  za nchi katika ujenzi wa makazi

Akiongea na waandishi wa habari jana Zakatia Materu, alisema amemuandikia barua ya malalamiko diwani wa eneo hilo, Mkuu wa wilaya na Mkurungenzi mtendaji  wa halmashauri hiyo, kuhusu barabra hiyo ya kuelekea halmashauri ya zamani waiangalie kwani wapo baadhi ya wafanyabiashara wenye fedha zao wameamua kujenga hadi kwenye hifadhi ya barabara jambo ambalo limesababisha adha kwa watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mkurugenzi  mtendaji wa  halmashauri hiyo  Ndakio Muhuli, ili kupata kauli yake juu ya  kushindwa kutekeleza agizo lililotolewa na baraza la madiwani.

Akiongea Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndaki Muhuli,  alisema taarifa hizo  kwanza amezipata  hivyo, atatuma wataalamu wake, ili kwenda kulitembelea eneo hilo linalololalamikiwa ili  kujua ukweli wake kabla hajatekeleza maagizo yaliyotolewa.

STORY BY: Kija Elias
PHOTO: Maktaba
EMAIL: eliaskisena@gmail.com
DATE: Machi 22, 2020

Saturday, March 28, 2020

Bob Andy afariki dunia akiwa na umri wa miaka 75



Mwanamuziki wa reggae Keith Anderson maarufu Bob Andy amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 75 kutokana na kuugua kwa maradhi ya kansa.

Nyota huyo amefariki dunia nyumbani kwake Stony Hill, St. Andrew jijini Kingston huko Jamaica baada ya kupambana na Saratani kwa muda mrefu.

Mwanzilishi huyo wa kundi The Paragons alichukuliwa kuwa miongoni mwa waandishi wa muziki huo wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Haikutosha kutoa nyimbo kali kwa sauti yenye kuvutia kama I've Got to Go Back HomeFeeling Soul or Too Experienced bali Bob Andy alionyesha uwezo mkubwa kwa nyimbo kali kama I Don't Want To See You Cry for Ken Boothe na ile ya  Feel Like Jumping for Marcia Griffiths.

Baadaye alikuja kupata umaarufu mkubwa pale walipoungana wawili Bob na Marcia kwa ajili ya kulimata soko la kimataifa na wakafanikiwa kufanya hivyo mika ile ya 1970, nyimbo kama Young, Gifted And Black or Pied Piper zilijidhihirisha wazi kuwa Bob Andy alikuwa na kipaji kikubwa mno katika medani ya muziki wa reggae.

Baada ya Marcia kuondoka na kwenda zake kuungana na I-Threes, Bob Andy aligeukia kategori ya kucheza na kuigiza. Alifanya hivyo  alipoigiza akitumia jina la Luke katika filamu ya Children of Babylon mnamo mwaka 1980 pia  alitumia jina la Raisen katika filamu ya The Mighty Quinn mnamo mwaka 1989.

Hakuacha kazi yake ya muziki baada ya hapo alikwenda zake London na baadaye Miam ambako alifanya kazi kama prodyuza kabla ya kuachia albamu ya Hangin Tough mnamo mwaka 1997.

Ziara mbalimbali za muziki zilimfuata mkongwe huyo pale alipotua jijini Addis Ababa huko Ethiopia wakati wa kumbukizi ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa Bob Marley  mnamo mwaka 2005.

Mwaka mmoja baadaye alitunukiwa tuzo ya Kimataifa ya CD (Order of Distiction), kutokana na mchango wake katika medani ya muziki wa Jamaica. 

Kifo chake kimeushtua ulimwengu ambapo Marcia Griffiths kupitia gazeti la Jamaica Obsever alikaririwa akisema, “ Amefariki asubuhi hii ya saa 8:00 a.m…..(…) Jana nilifanya naye mawasiliano kwa njia ya video.”  Ulimwengu wa reggae ulitoa salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho.

Boby Andy alizaliwa Oktoba 28, 1944 Kingston Jamaica

Buju Banton:  “Nitakukosa sana rafiki yangu. Asante sana kwa masomo kuhusu maisha.”

Clinton Fearon: “Kaka yangu Bob Andy amefariki dunia. Alikuwa moja ya watunzi wa nyimbo niliovutiwa nao, alikuwa na ushawishi mkubwa katika utunzi wangu. Ninakumbuka nilikutana naye muda mfupi nchini Jamaica wakati nilizuru Kingston. Wakati ule alikuwa akiishi na Marcia Griffiths. R.I.P brendin.”

David Rodigan: “ Nimejawa na huzuni kubwa kutokana na kuondokea na Bob Andy asubuhi hii akiwa nyumbani kwake Kingston, hakika alikuwa nembo ya muziki wa Jamaica na rafiki yangu kipenzi ambaye ninajivunia kufahamiana naye miaka 35 iliyopita. Hakika alikuwa mahiri katika uimbaji na utunzi wa zama zote sijawahi kuuona hapa duniani. Katika albamu yake ya ‘Songbook’ pekee ni ushuhuda ambao umetoa mchango mkubwa katika muziki na utu. Ulale mahali pema peponi hakuna maumivu sasa. Rambirambi zangu kwa watoto na wote waliompenda.”


Mwanamuziki wa Reggae Delroy Washington afariki dunia kwa Covid-19



LONDON, ENGLAND
Mwanamuziki mahiri wa Reggae Delroy Washington amefariki dunia jijini London, Uingereza. Nyota huyo wa muziki ambaye jina lake halisi ni Delroy Washington amefariki dunia wakati ambao fani ya muziki huo ikiwa na uhitaji naye. 

Mwanamuziki huyo amefariki dunia kwa maambukizi ya virusi vya Covid-19. Katika akaunti ya Instagram ya mwanamuziki Winston Francis @ winstonmrfixitfrancis aliandika kuelezea machungu ya kumpoteza rafiki yake na mkali wa muziki wa reggae kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

The Voice imethibitisha kuondokewa na mwanafamilia huyo katika medani ya muziki wa Reggae. 

Alizaliwa mnamo mwaka 1952 Westmoreland nchini Jamaica na familia yake ilihamia nchini Uingereza wakati akiwa mtoto miaka ile ya 1960.

Alianza muziki akiwa meneja wa kuratibu ziara na mara chache katika vipindi vya muziki katika bendi ya Rebel. Wakati alipoingia kikamilifu katika uimbaji alikuwa solo akirekodi na Count Shelly na baadaye akimsaidia Bob Marley  na The Wailers katika albamu mbalimbali.

Alikuja kuwa rafiki wa karibu wa waimbaji maarufu miaka ya 1970 na baadaye aliwavutia wengi nchini Uingereza kutokana na mistari katika nyimbo zake. Mnamo mwaka 1976 alitoa albamu yake I Sus na mwaka 1977 alitoa albamu iliyofahamika kwa jina la Rasta.

Pia alishiriki katika baadhi ya singo ikiwamo ile ya Likes of Jah Shaka. Mbali ya mchango wake mkubwa katika muziki alileta mabadiliko makubwa alipofanikiwa kuwa mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Muziki wa Reggae nchini Uingereza ambako alifanya kampeni ya kutambuliwa kwa London Borough huko Brent kama makao makuu ya Muziki wa Reggae nchini Uingereza na Ulaya kwa ujumla.

Lebo za muziki huo kama Island Records na Jet Star zilikuwa zikifanya kazi kutokea hapo. 

Hata hivyo Delroy anasalia katika vichwa vya wengi kwa alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa kijamii ambaye aliendeleza kazi nzuri zikiwamo 12 Tribes of Israel, HPCC Bridge Park or I & I Idren of Israel.

Hakika upole wake, ubunifu na roho yenye akili na umakini itakosekana miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa reggae.


STORY & PHOTO BY: Jabir Johnson
EMAIL: jabirjohnson2020@gmail.com
DATE: Machi 27, 2020
Singles
"Jah Man a Come" (197?), Lord Koos
"Lonely Street" (1973), Count Shelly
"Papa Was a Rolling Stone" (1973), Sir Christopher
"Freedom Fighters" (1976), Axum
"Give All the Praise to Jah" (1977), Virgin - 12-inch
"Memories" (1978), Burning Sounds - Delroy Washington & Jah Son
"It's Like Magic" (197?), Burning Vibrations - 12-inch
"Magic" (1980), Direction Discs/Ballistic - Delroy Washington Band
"Cool Rasta" (19??), Ballistic
"For Your Love" (1981), Ankh/Pinnacle

Albert 'Apple Gabriel' Craig is no more


Mwanzilishi na mwanachama wa zamani wa kundi maarufu la muziki wa reggae Ulimwenguni la Israel Vibration Albert 'Apple Gabriel' Craig  amefariki dunia Jumatatu ya Machi 23, 2020. Tarehe rasmi ya kuzikwa bado haijawekwa bayana.

Imeelezwa chanzo cha kifo chake ni magonjwa mchanganyiko  lakini sio ugonjwa Corona kama wengi walivyodhani.

Katika ukurasa wa facebook wa Roots Radics' Flaba Holt iliandikwa kwamba Apple Gabriel hali yake ya kiafya haikuwa nzuri kwa muda mrefu hadi mauti yalipomkuta.

Apple Gabriel amekuwa akipigania uhai wake kutokana na maradhi ya Polio tangu akiwa mmtoto na mwili wake haukuwa katika hali nzuri huku ripoti zikisemma miaka 10 iliyopita alikuwa amedhoofu na hali ya kimaisha haikuwa nzuri kwake.

Mara ya mwisho kuonekana katika mitandao ya kijamii hususani Facebook ilikuwa ni Machi 7 mwaka huu ambapo alikuwa akizungumzia namna kiharusi kilivyomfanya hata upande mmoja wa mwili wake kupooza huku akiruhusiwa pasipo kufahamu mahali sahihi pa kwenda.

Maisha ya nyota huyo hayakuwa mepesi hata kidogo, aliendelea kupanda na kushuka baada ya kuachana na Israel Vibration mnamo mwaka 1997.  

Alianza vizuri katika maisha yake ya kuongoza uimbaji (solo career) albamu yake ya Another Moses ya mwaka 1999 ilipokelewa vema. 

Pia alifanya kazi na wasanii wengine na bendi kadhaa wakiwamo Groundation or Jahcoustix. Haikutosha aliopanda katika matamasha jukwaani kama mwaka 2009 nchini Israel. 

Hata hivyo alipambana hadi kufikia kilele cha mafanikio yake pale alipotoa albamu yake iliyofahamika kwa jina la Teach Them Right mnamo mwaka 2010. Licha ya yote hayo bado hali yake ya kiuchumi ilikuwa ngumu akiishi kama yatima na wakati mwingine alikosa hata pesa za kurekodi. 

Hatua hiyo ilimfanya aumie moyo kwani nyimbo alizokuwa nazo moyo ziliishia kuumiza moyo wake. Wengi wataendelea kumkumbuka Apple Gabriel kutokana na kipaji chake alichokuwa nacho. 
Msanii wa muziki wa reggae Heather Augustyn aliandika, " Apple Gabriel alikuwa na maisha magumu. Alikuwa akiugua kwa njia nyingi. 

Siku zake Apple Gabriel hapa duniani zilikuwa ngumu. Lakini moyo wake wa ushujaa na maneno yake yalimfanya Apple Gabriel kuwa mpole na imara, mcheshi na mtu makini, mbunifu na mzalishaji. Alikuwa mwanamuziki kweli kweli."

Baadhi ya nyimbo maarufu na kali wakati akiwa na Israel Vibration We A De Rasta, Why You So Craven, Oh Jah Solid Rock, Mud Up, Rude Boy Shuffling, Friday Evening na Walk The Streets of Glory. 

Apple Gabriel amefariki dunia tarehe ambayo miaka 21 iliyopita yaani mwaka 1999 aliachia albamu ya Another Moses. Alijiunga na Israel Vibration mnamo mwaka 1975. 


Walianzisha kundi hilo akiwa na wenzake Lascelle ‘Wiss’ Bulgin na Ccil ‘Skeleton’ Spence ambao sauti za watatu hao zilifanya kundi hili ling’are. Walitoa albamu ya kwanza iliyofahamika kwa jina la ‘The Same Song’ mnamo mwaka 1978 

Diskografia ya Apple Gabriel
(1978-1997)

Albums:
.1978 - The Same Song
.1978 - The Same Song Dub - [Reissue: "Israel Dub (Same Song Dub and Unconquered Dub)" 1991 and "Same Song + Dub" 2000]
.1980 - Unconquered People - (Reissue "Survive" 1995 and "Practice What Jah Teach" 1999)
.1980 - Unconquered People Dub - [Reissue: "Israel Dub (Same Song Dub and Unconquered Dub)" 1991].
.1981 - Why You So Craven
.1983 - Live At Reggae Sunsplash (The Gladiators & Israel Vibration)
.1988 - Strength Of My Life
.1990 - Praises
.1990 - Dub Vibration (Israel Vibration In Dub) - (Includes Dub Versions of "Strength Of My Life" and "Praises").
.1991 - Forever
.1992 - Vibes Alive
.1993 - IV
.1994 - IV D.U.B. - (Includes Dub Versions of "IV" and "Forever")
.1995 - On The Rock
.1995 - Dub The Rock
.1996 - Free To Move
.1997 - Live Again!

2) Apple Gabriel - Discography: (Solo Works)

Albums:
.1999 - Another Moses
.2002 - No Racism (Live From Eugene, Oregon)
.2010 - Teach Them Right

EPs:
.2001 - Give Me M.T.V. - (Ep with 4 Tracks) - (Unreleased Tracks)

Compilation/Best of:
.1985 - Israel Vibration Meets Cocoa Tea (Cactus label)
.1997 - RAS Portraits (Ras label)
.2000 - Power Of The Trinity (3 Cd Set) - (Ras label and Sanctuary label)
.2005 - Cool And Calm (Ras label)
.2005 - This Is Crucial Reggae (Sanctuary Records label)
.2010 - Feelin Irie (Continental Record Services label)

Unaikumbuka siku Manchester United ilipoweka rekodi sawa na ya Arsenal baada ya miaka 67?

Machi 28, 2001 England iliizabua Albania katika mchezo wa kuania kufuzu kucheza Kombe la Dunia kwa mabao 3-1.

Kinachostaajabisha katika mchezo huo ni kwamba nusu ya kikosi kilichoitwa katika mchezo huo kilikuwa na wachezaji kutoka klabu ya Manchester United. 

Katika mchezo huo kulishuhudia mabao hayo ya England yakifungwa na Michael Owen 73, Paul Scholes 85, na Andy Cole 90.

Mchezo huo ulichezwa katika dimba la Qemal Stafa katika makao makuu ya taifa la Albania jijini Tirana.  

Wachezaji watano wa kikosi hicho cha kwanza walikuwa ni kutoka klabu ya Manchester United ambao ni Gary Neville, Nicky Butt, David Beckham, Paul Scholes, na Andy Cole. 

Wakati huo Manchester United walikuwa ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu nchini England. 
Katika kipindi cha pili walitolewa wachezaji na kuingizwa Wes Brown na Teddy Sheringham na kufanya idadi ya wachezaji kuwa saba kutoka klabu moja. 

Rekodi hiyo ilikwenda sawa na ile iliyowekwa na klabu ya Arsenal mnamo mwaka 1934 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia ambao ulichezwa mwezi Novemba mwaka huohuo ambapo wachezaji saba katika kikosi kilichoitwa waliocheza mtanange huo walitoka kwa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa London. 

Kwa ufupi ni kwamba ilichukua miaka 67 kuweka rekodi sawa. Pia bao pekee la Albani lilifungwa na Altin Rrakli katika dakika ya 93 ya mchezo. Owen wakati akivunja vitasa vya Albania alikuwa akihudumu na Liverpool.