Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, February 29, 2020

Dkt. Ndugulile: Nchi iko salama dhidi ya Virusi vya Covid-19

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza jambo katika mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Mt. Maria Goreth mjini Moshi Februari 29, 2020. (Picha na Jabir Johnson)


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulileamesema nchi ya Tanzania iko salama dhidi ya maambukizi ambayo yanatikisa dunia kwa sasa ya virusi vya Covid-19.

Akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha sita ya Shule ya Mt. Maria Goreth mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro leo Dkt. Ndugulile amesema hali ya maambukizi imeendelea kuibua hofu kwa mataifa mbalimbali lakini nchini Tanzania hali ni shwari.

“Tanzania tuko salama dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona ambayo vimeanzia China, tunaendelea kuimarisha mipaka, viwanja vya ndege kwa kuweka mifumo ya kuwaangalia wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaoingia Tanzania,” amesema Dkt. Ndugulile.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema wameenda kuimarisha hali ya usalama katika visiwa vya Zanzibar ambako Waitaliano wengi wanatiririka huko kila wakati.

Wasiozingatia usafi waendelea kutozwa faini Moshi

Wakazi wa Kata ya Bondeni katika Manispaa ya Moshi wametakiwa kuendelea kufanya usafi katika maeneo wanayoishi ili kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu wa mazingira.

Akizungumza na JAIZMELA NEWS Afrika Mtendaji wa kata hiyo Philipina Tenga alisema usafi ni jambo la msingi ili kupambana na maradhi kwani msingi wa siha njema ni usafi

"Tumekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wakazi wa kata hii (Bondeni) kuhusu usafi, pia kila Jumamosi tunakutana kufanya kwa pamoja na pia mwishoni mwa mwezi," alisema Tenga.

Mbowe akamatwa baadaya kumaliza mkutano, vurugu zaibuka Masama

Polisi Wilaya ya Hai wamemkamata Mbunge wa Hai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika viwanja vya Nkoromu Masama kati wilayani humo.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alikamatwa saa 12:00 baada ya kumaliza mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wananchi.

Wakati akijiandaa kuondoka eneo hilo, polisi walikwenda katika gari lake wakieleza kuwa wanamhitaji kituoni, ombi ambalo liliridhiwa na mwenyekiti huyo wa Chadema.

Awali, akizungumza katika mkutano huo Mbowe amesema licha ya kupitia kipindi kigumu na changamoto mbalimbali za kisiasa, hawezi kukoma kuendelea na mapambano.

Unaikumbuka siku Middlesbrough ilipowashangaza Bolton ya Jay Jay Okocha?

Februari 29, 2004 ilikuwa siku njema kwa klabu ya Middlesbrough ya England pale ilipovunja vitasa vya Bolton katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi. 

Mabao mawili ya haraka yalitosha kuipa taji Middlesbrough. Na hilo lilikuwa taji lake la kwanza kubwa katika historia ya klabu hiyo. 

Klabu ya Middlesbrough ilianzishwa mnamo mwaka 1876. 

Miaka miwili kabla Middlesbrough walikaribia kuchukua taji la FA na Kombe la Ligi mnamo mwaka 1997 walipofika fainali katika michuano hiyo. 

Mnamo mwaka 1998 Middlesbrough walirudi katika fainali ya Kombe la Ligi lakini walishindwa kuchukua taji hilo. 

Walipofika fainali ya Kombe la Ligi  kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1997 walipambana na Leicester City ambao walitwaa baa da ya mchezo wa marudiano. 

Wangeweza kuchukua lakini ndio hivyo.

Bolton walikuwa na historia ya kutwaa taji la FA mara nne wakifanya hivyo 1923, 1926, 1929 na 1958. 

Bolton walifika fainali ikiwa ni baada ya kushindwa mbele ya Liverpool kwa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool mnamo mwaka 1995.

Miamba hiyo ilikutana katika dimba la Millenium jijini Cardiff mbele ya watazamaji 72,634  ambao walikosa kuliona bao la kwanza siku hiyo. 

Ikiwa ni dakika ya pili ya mchezo wakiwa bado wanajiweka sawa katika viti vyao vya kukalia kiungo wa Middlesbrough Boudewijn Zenden alifumua mkwaju mkali katika lango la Bolton ambao ulimkuta mshambuliaji wao Joseph Desire na kuipa uongozi Middlesbrough.

Dakika tano baadaye Zenden aliipa uongozi Middlesbrough kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa kati wa Bolton Emerson Thome kumchezea rafu Job ndani ya eneo la hatari. 

Bolton walijaribu kuliandama lango la Bolton ambapo juhudi zao zilitaka kuzaa matunda katika dakika ya 21 ya mchezo kupitia kwa nyota wao Kevin Davies  lakini mlinda mlango wa Middlesbrough Marl Schwarzer aliokoa mchomo huo hivyo mchezo ukamalizika kwa mabao 2-1. 

Kwa wakati huo bao la mapema lilifungwa na Job na kuwa bao la mapema katika historia ya Kombe la Ligi kwa wakati huo.

Rekodi hiyo ilikuja kuvunjwa na nyota wa Loverpool John Riise aliyefungwa kwenye michuano hiyo katika dakika ya kwanza ya mchezo mwaka uliofuata.

MAKTABA YA JAIZMELA: Elpidio Rivera Quirino ni nani?

Februari 29, 1956 alifariki dunia mwanasheria na mwanasiasa wa Ufilipino Elpidio Rivera Quirino Mwanasia huyo aliweka rekodi ya kuwa Rais wa Sita wa taifa hilo. 

Alishika wadhifa huo kutoka mwaka 1948 hadi mwaka 1953. 

Katika siasa za Ufilipino aliingia wakati huo akiwa mwakilishi wa Ilocos Sur kutoka mwaka 1919 hadi 1925. 

Mnamo mwaka 1925 alichaguliwa kuwa seneta ambapo alidumu kwa miaka sita hadi mwaka 1931. Mnamo mwaka 1934 alikuwa mwananchama wa Kamati ya Uhuru wa Ufilipino ambayo ilimpeleka jijini Washington D.C

Baada ya kustaafu mnamo mwaka 1953 Quirino alisisitiza kuendelea kuwatumikia watu wa Ufilipino hivyo alihudumu kama "Baba wa Huduma za Kigeni." 

Qurino alifariki dunia kwa maradhi ya moyo akiwa katika nyumba yake aliyostaafu nayo ya Novaliches katika mji wenye watu wengi nchini Ufilipino.

Alizikwa katika makaburi ya Manila South katika kitongoji cha Makati katika mji mkuu wa taifa hilo wa Manila. 

Hata hivyo wakati taifa hilo liliadhimisha miaka 60 ya kumbukizi tangu kifo chake mnamo Februari 29, 2016 mabaki ya mwili wake yalihamishwa kutoka eneo lake la awali yalikohifadhiwa na kupelekwa katika Makaburi ya Mashujaa yaliyopo Taguig hapo hapo jijini Manila. 

Quirino alishinda kuongoza taifa hilo kama Rais wa sita wa Ufilipino baada kifo cha Rais Manuel Roxas mnamo mwaka 1948. 

Mara tu baada ya kifo hicho Quirino aliapishwa kushika wadhifa wa kuisimamia serikali wakati huo akiwa Makamu wa Rais mpaka uchaguz utakapofanyika. Katika uchaguzi senate Fernando López alishinda kuwa Makamu wa Rais. 

Quirino alishinda kwa kupigiwa kura na wananchi wa Ufilipino. Kwa mara ya kwanza katika ardhi hiyo Rais, makamu wa Rais na maseneta wote walitoka katika chama cha Liberal. 

Uchaguzi huo ulipingwa kila kote kwamba ulijawa na rushwa na vurugu. 

Wapinzani wa Quirino walipigwa na wengine kuuawa na waliokuwa wakimuunga mkono au polisi ambapo vitendo vya rushwa vilikuwa wazi. 

Uchaguzi wa mwaka 1953 vyama vya Nacionalitsa na Demokratiki viliunda muungano ambao ulimwangusha Quirino ambaye hali yake ya kiafya haikuwa njema. 

Msemaji wa zamani wa serikali ya Ufilipino Ramon Magsaysay aliongoza kura za wengi wa wapiga kura wapatao milioni 1.5

Wakati wa utawala wake Quirino alitangaza malengo mawili muhimu la kwanza ikiwa ujenzi imara wa uchumi wa taifa hilo  na pili kurudisha imani ya raia kwa serikali ambapo katika kuhakikisha imani ya raia wa Ufilipino wanakuwa na uzalendo kwa taifa lao; alihakikisha bima kwa wasiokuwa na ajira, bima ya uzeeni, bima ya ajali na ulemavu wa kudumu, bima ya afya, bima ya uzazi, nafasi za kazi.

Jenerali Delphin Kahimbi is no more

Naibu mkuu wa majeshi ya FARDC, Nchini DRC na Mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi Jenerali Delphin Kahimbi amepatikana amefariki dunia nyumbani kwake jijini Kinshasa jana asubuhi.

Habari hiyo imetolewa na mkewe na washirika wenzake kadhaa wa karibu. Uchunguzi unaendelea, afisa mmoja wa jeshi amebaini. 

Jenerali Delphin Kahimbi aliitwa mara kadhaa katika siku za hivi karibuni kujibu tuhuma zinazomkabili (uhusiano na makundi yenye silaha na kujaribu kuhatarisha usalama).

Kulingana na vyanzo kutoka ikulu ya rais, Jenerali Delphin Kahimbi alikuwa amesimamishwa kazi.

Msemaji wa jeshi amekiri kwamba uchunguzi umeanzishwa ili kubaini sababu za kifo chake.
Kifo chake kinakuja ikiwa ni siku baada ya kusimamishwa kazi tu.Hii ni habari mbaya sana kwa DRC. 

Mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi, Jenerali Delphin Kahimbi, amefariki dunia katika hospitali ya Cinquantaire jijini Kinshasa, kwa mujibu wa chanzo ambacho hakikutaka jina lake litajwe.

Jenerali Delphin Kahimbi, ambaye alikuwa anakabiliwa na vikwazo vya Ulaya na Marekani tangu 2016, anatuhumiwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC.

Friday, February 28, 2020

Nzige wavamia Mashariki ya DRC

Kwa sasa ni wilaya tu ya Aru katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo, iliyoathiriwa na nzige hao wa jangwani. 

Lakini wadau mbalimbali katika nchi hiyo wanasema wana wasiwasi na uvamizi huo unaoendelea katika nchi mbalimbali za Afrika.

Baada ya Kenya, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Sudani, Tanzania na Uganda, mashariki mwa DRC sasa inakabiliwa na uvamizi wa nzige wa jangwani. Kulingana na vyanzo kadhaa kutoka Ituri, nzige wa jangwani walivamia wilaya ya Aru Februari 19.

Kwa sasa, hakuna hatua thabiti ambayo imechukuliwa ili kukabiliana na uvamizi huo.

Hata hivyo tishio bado lipo, ameonya Dieudonné Lossa, kiongozi wa chama cha wahandisi wa kilimo mkoani Ituri.

"Kinachotia wasiwasi sana kwanza ni uharibifu ambao wadudu hao watasababisha kwa mazao. Raia watapoteza mazao. Mashamba yao yatateketezwa. Kuna hatari ya kupoteza kila kitu. Kuna hatari ya kutokuwa na chakula chochote katika jiji la Bunia na Ituri kwa ujumla, " amesema Guerschom Dramani Pilo, Waziri wa Kilimo katika Mkoa wa Ituri amesema.

Bila kukana tishio ambalo nzige hawa husababisha kwa kilimo, mamlaka mkoani Ituri wanahakikisha kwamba hali hiyo bado inaweza kudhibitiwa.

Waziri wa Kilimo katika Mkoa waIturi amesema kuwa timu ya wataalamu imepelekwa katika eneo la Aru ili kutathmini hali hiyo.

Unaikumbuka siku chungu kwa mashabiki wa Paris Saint Germain?

Februari 28, 2010 makundi mawili hasimu katika soka nchini Ufaransa kundi la mashabiki wa klabu ya Paris Saint German walipambana tena na lile la Marseille ambapo yalisababisha kifo cha shabiki mmoja na wengine 20 kukamatwa katika vurugu hizo.

Mchezo huo ulichezwa jijini Paris ambapo PSG walikuwa wenyewe katika mchezo huo wa Ligi Kuu nchini humo maarufu Ligue 1.

PSG walikuwa wakitafuta kulipa kisasi kwani mapema mwanzoni mwa msimu huo walipoteza.

Katika mchezo huo katika dakika ya 15 winga wa Marseille  Hatem Ben Arfa alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za PSG. Katika kipindi cha pili wageni hao walipata mabao kupitia kwa Licho Gonzalez katika dakika ya 54 na Benoit Cheyrou katika dakika ya 71 ambapo mchezo ulimalizika kwa Marseille kupata ushindi wa mabao 3-0.

Siku ilikuwa mbaya kwa mashabiki wa PSG ambao walikuwa uwanjani na waliokuwa nje ya uwanja wa Parc des Princes ambako makundi mawili ya mashabiki hasimu Boulogne Boys na Supras Auteuil yalipambana kabla ya mchezo, wakati wa mchezo na baada ya mchezo huo.

Iliwabidi polisi wa Ufaransa kutumia gesi za kutoa machozi ili kuondoa makundi hayo ambapo walifanikiwa kuwakamata mashabiki 20.

Watu wengi walipata majeraha madogo madogo, lakini mtu mmoja mwenye umri wa miaka 38 aliyfahamika kwa jina la Yann L alipata majeraha ya kichwani ambayo yalisababisha ashindwe kujitambue hadi mauti yalipomkuta majuma mawili baadaye. 

PSG walinyoshewa kidole cha lawama kwa vurugu hizo ambazo ziliwafanya wasiuze tiketi katika mechi zote za ugenini katika miezi iliyobaki katika msimu huo.

MAKTABA YA JAIZMELA: Rajendra Prasad ni nani?

Februari 28, 1963 alifariki dunia Rais wa Kwanza wa kuchaguliwa wa India Rajendra Prasad. Mwanasiasa huyo ambaye alisomea sheria na sayansi ya siasa alishikia wadhifa huo kutoka mwaka 1950 hadi 1962. Prasad alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 78 huko Patna.

Hali yake ya afya ilianza kuzorota mnamo mwaka 1960 alipopatwa na shambulio la moyo. Alianza kupatiwa matibabu na madatari bingwa wa nchini India akiwamo rafiki yake Dkt. Bidhan Chandra Roy kwa wakati huo alikuwa Waziri katika Jimbo la West Bengal.

Mnamo Machi 7, 1961 alianza kunyong’onyea zaidi akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kupatwa kiharusi katika ubongo, wakati huo alikuwa bado katika Ofisi ya Waziri wa Mambo Ndani wa India. Wakati akiwa katika wadhifa huo ambao kwa mujibu wa kikatiba ya India hakuwa na nguvu kubwa sana serikali kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu Jawaharlal Nehru. Mnamo mwaka 1916 alijiunga na Mahakama kuu ya Bihar  na Odisha.

Mnamo mwaka 1917 aliteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa kwanza wa baraza la seneti na Principal wa Chuo Kikuu cha Patna. Pia katika masuala yake ya sheria alikuwa akifanya kazi zake huko Bhagalpur mji maarufu kwa silk katika jimbo la Bihar.

Alizaliwa Desemba 3, 1884 huko Ziradei , India kwa wazazi Mahadev Sahai ambaye alikuwa akizungumza lugha za Kisankrit na Kiajemi na Mama yake aliyefahamika kwa jina Kamleshwari Devi ambaye alikuwa mahiri kwa kusimulia hadithi za zamani za Wahindu za Ramayana na Mahabharata. Prasad alipoanza kukua alikuwa akisimulia sana hadithio hizo na mama yake.

Katika familia yao hakuzaliwa peke yake walikuwa watano nay eye akiwa ni wa mwisho. Wa kwanza alikuwa kaka yake aliyefuatiwa na wadogo zake wa kike watatu. Licha ya kusimuliwa hadithi hakuzifaidi vizuri kwani mama yake alifariki dunia wakati akiwa bado mdogo na kaka na dada zake walianza kumtunza. Baadaye Prasad alikuja kuwa tajiri na mmiliki wa ardhi wa Kayastha. Alipokuwa mwalimu alifanya kazi katika taasisi mbalimbali.

Baada ya kumaliza shahada ya uzamili katika masuala ya uchumi  alifanikiwa kuwa kupanda hadi kuwa Profesa wa lugha ya Kiingereza katika Chuo cha Langat Singh huko Muzzaffapur katika Bihar na baada akawa Mkuu wa Chuo. Prasad aliachana na chuo hicho na kwenda zake kuchukua masomo ya sheria katika chuo cha Ripon huko Calcutta ambacho chuo hicho kwa sasa kinafahamika kwa jina la Surendranath Law College.

Mnamo mwaka 1909 wakati akiwa katika masomo ya sheria huko Kolkatta alikuwa akifanya kazi kama Profesa wa Uchumi katika chuo cha Calcutta City. Mnamo mwaka 1915 alionekana katika mtihani wa shahada ya uzamili ya Sheria ambako alipita na kutunukiwa medali ya dhahabu.

Alihitimu shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Allahabad mnamo mwaka 1937. Prasad alijiunga na harakati za kutafuta uhuru wa India wakati alipohudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Kitaifa cha India mnamo mwaka 1906.

Mkutano huo ulifanyika mjini Calcutta ambako alihudhuria kama mtu aliyejitolea kuunga juhudi za kutafuta suluhu la watu wa India. Wakati huo alikuwa akisoma pale Calcutta.Alijiunga na chama hicho mnamo mwaka 1911, katika mkutano mwingine ulifanyika hapo hapo Calcutta.

Mnamo mwaka 1916 alikutana na Mahtma Gandhi walipokuwa katika kikao cha Lucknow kilichoendeshwa na chama hicho hapo hapo Calcutta. Gandhi alimtaka Prasad aje na wenzake wanaotaka kujitolea kuunga mkono juhudi za kutafuta uhuru wa India. 

Mnamo mwaka 1920 Prasad aliamua kuachana na sheria na nyadhifa nyingine katika Chuo Kikuu na kuunga mkono harakati za kudai uhuru wa India.

Thursday, February 27, 2020

Unaikumbuka siku iliyoweka historia kwa Maradona?

Februari 27, 1977 Argentina iliizabua Hungaria mabao 5-1 katika mchezo wa kirafiki ambao uliweka rekodi kwa mchezaji chipukizi wa Argentina Diego Maradona kuanza safari yake ya soka la Kimataifa akiwa na Albiceleste. 

Maradona alikuwa na umri wa miaka 16 katika mchezo huo. 

Aidha kwa wakati huo Hungaria ilikuwa ni timu ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kufika katika fainali mbili za Kombe la Dunia mnamo mwaka 1938 na 1954. 

Pia ilikuwa timu ya taifa ambayo ilikuwa imebeba medali tatu za dhahabu za Michuano ya Olimpiki 1952, 1964 na 1968 pia walichukua medali ya fedha mnamo mwaka 1972. 

Licha ya medali hizo Hungaria ilishindwa kufuzu Kombe la Dunia mnamo mwaka 1974, michuano ya Olimpiki mnamo mwaka 1976 na Mashindano ya Ulaya mwaka 1976. 

Argentina wakati huo ilikuwa imefika fainali ya Michuano ya Olimpiki mnamo mwaka 1928 na fainali ya Kombe la Dunia mnamo mwaka 1930. Pia Argentina ilikuwa imebeba mataji ya Copa America mara 12.

Katika dimba la Bombanera jijini Buenos Aires mbele ya watazamaji akali ya 60,000 hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa mabao manne. Mabao ya Argentina yalifungwa na Daniel Bertoni aliyefunga hat trick katika mchezo huo na mabao mawili ya Leopoldo Luque.
Akitokea benchi Zombori Sandor aliipa Hungaria bao la kufutia machozi katika dakika ya 61 ya mchezo huo.

Dakika moja baadaye kulifanyika mabadiliko Albiceleste walimtoa Ricardo Villa akaiingia Jorge Benitez na alitolewa Luque  na kuingia Diego Armando Maradona wakati huo alikuwa akihudumu na klabu ya Argentina Juniors. 
Huo ndio ulikuwa ni mchezo wake kwanza kwa Argentina na baada ya hapo alihudumu na miamba hiyo mechi 91 ana kuiongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia mnamo mwaka 1986.

MAKTABA YA JAIZMELA: Boris Nemtsov ni nani?

Februari 27, 2015 alifariki dunia mwanasayansi na mwanasiasa wa Russia Boris Yefimovich Nemtsov. Nemtsov alikuwa mtaalamu wa Fizikia. 

Katika siasa alikuwa kiungo muhimu katika kuanzisha ubepari katika ardhi ya Usovieti. 

Alifanikiwa sana katika masuala ya siasa miaka ya 1990 wakati wa utawala wa Rais Boris Yeltsin. 
Kuanza mwaka 2000 hadi kifo chake alikuwa mpinzani wa Vladimiri Putin. 

Mwanasiasa huyo alichapwa risasi nne kutoka mgongoni mbele ya mpenzi wake raia wa Ukraine, Anna Duritskaya. 

Majuma kadhaa kabla ya kuuawa kwake Nemtsov alielezea hofu yake kwa Putin kwamba anaweza kumuua. 

Miaka miwili baadaye watu watano wa Chechnya walikamatwa na kukutwa na hatia na mahakama ya haki ya Moscow baada ya kukubali kuwa walikubaliana kufanya mauaji hayo kwa kiasi cha dola la Kimarekani 253,000 ambazo ni sawa na Shilingi milioni 585 za Tanzania. 

Hata hivyo hakuna mtu anayedaiwa kuwakodi watu hao kufanya mauaji. 

Nemtsov alikuwa akiikosoa serikali ya Putin kuwa imekuwa ya kibabe, isiyo na demokrasia, matumizi mabaya ya fedha kuelekea michuano ya Olimpiki ya Sochi na Uingiliaji wa kijeshi katika ardhi ya Ukraine. 

Baada ya mwaka 2008 Nemtsov alichapisha kwa kina ripoti kuhusu rushwa kwenye serikali ya Putin. 

Ikiwa ni sehemu ya mapambano ya siasa Nemtsov aliendelea kuwa mratibu wa maandamano ya Raia wa Russia wakipinga mswada uliouitwa Straregy 31. 

Maandamano hayo yalikuwa yakitaka uchaguzi huru ufanyike kwa tume huru. 

Wakati anauawa Nemtsov alikuwa jijini Moscow akijaribu kuratibu kundi la watu kwa ajili ya kuvipinga vikosi ya kijeshi vya Russia kutokana na mgogoro wa Ukraine na Russia. 

Pia Nemtsov kabla ya kuuawa alikuwa njiani kuandika ripoti kuhusu namna majeshi ya Russia yalivyokuwa yakipigana na wanajeshi wa zamani wa Russia katika ardhi ya Ukraine, taarifa ambazo Kremlin ilikuwa inazikataa. 

Taarifa hizo zilikuwa hazifahamika ndani na nje ya Russia. 

Nemtsov alikuwa gavana wa kwanza wa Nizhny Novgorod Oblast kutoka mwaka 1991 hadi 1997. Baadaye alifanya kazi na serikali ya Russia akiwa Mafuta na Nishati mwaka 1997. 

Pia Nemtsov alikuwa Makamu wa Baraza la Usalama la Russia kutoka mwaka 1997 hadi 1998. Miaka iliyofuata alijiingiza katika kuunda vikundi vya kisiasa. 

Hadi mauti yanamkuta Nemtsov alikuwa miongoni mwa viongozi wa Vuguvugu la Solidarnost (Mshikamano) na mbunge wa bunge la mkoa wa Yaroslavl Oblast na makamu mwenyekiti wa chama cha RPR-PARNAS. 

Baada ya mauaji hayo mwandishi Serge Schmemann wa gazeti la New York Times aliomboleza kifo cha mwanasiasa huyo, kwa kuandika, "A Reformer Who Never Backed Down."  

Pia mwandishi huo aliongeza "Tall, handsome, witty and irreverent, Mr. Nemtsov was one of the brilliant young men who burst onto the Russian stage at that exciting moment when Communist rule collapsed and a new era seemed imminent." 

Ikiwa na maana ya "Mrefu, mzuri, mwerevu na asiye na heshima, Nemtsov alikuwa mmoja wa vijana wenye busara ambao waliibuka Nchini Urusi katika hatua Ukomunisti ulipokuwa ukifikia zama zake za mwisho."

Nemtsov alizaliwa Oktoba 9, 1959 Sochi nchini Russia na alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 55.

Wednesday, February 26, 2020

Polisi Tanzania 1-1 Yanga SC: Walichinja Paka wakaambulia sare Ushirika




NA JABIR JOHNSON
Februari 18, 2020 kulichezwa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika dimba la Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. 

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 baina ya wenyeji Polisi Tanzania na Yanga SC. Mabao ya Tariq Seif wa Yanga na Sixtus Sabilo wa Polisi Tanzania yalitosha kutoa sare hiyo. 

Miongoni mwa michezo iliyokuwa na msisimko mkali ulikuwa ni huo kutokana na historia ya timu kutoka Dar es Salaam kwa miaka mingi zinapotua katika mji wa Moshi. 

Ikiwa imepita takribani miongo mitatu ya kutoziona timu za ligi kuu msimu wa 2019/2020 umeweka historia kwa wakazi wa Kilimanjaro na vitongoji vyake. 

Itakumbukwa mchezo wa kirafiki Yanga ilizabuliwa mabao 2-0 na Polisi Tanzania; baada ya kutua katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Polisi Tanzania ililazimisha sare ya 3-3 na mzunguko wa pili tena ililazimisha sare ya 1-1. 

Hata hivyo kwenye mchezo huo uliochezwa Moshi umeacha maswali mengi kutokana na mambo kadhaa ambayo ni vema ukayafahamu kuwa yalikuwepo kwenye mchezo huo.

1. Kuchinjwa kwa Paka
Macho yalishuhudia paka aliyebebwa na mojawapo wa mashabiki siku moja kabla ya mchezo huo na kushangaza zaidi ni kwamba katika ngazi za kupandia vyumba vya kubadilishia wachezaji wa Yanga vilivyoko upande wa goli la kaskazini ya Uwanja; kulikuwa na viashara vya damu ambayo inasadikika kuwa ya paka. 

Hili lilijihidhirisha siku ya mechi kwani Yanga hawakutaka kuingia katika vyumba vya kubadilishia na walisalia kukaa nje kwenye viti vyeupe vilivyoandaliwa kutokana na kuwa na wasiwasi mpaka pale walipojiridhisha kuwa kuna usalama. 

Maswali ni haya Paka yule siku moja kabla ya mchezo ni wa nani? alitoka wapi kwani ni nadra kuona Paka wakisafirishwa kama kuku na mbwa?; Kama alichinjwa, alichinjwa kwa sababu gani? na kama ni ushirikina ni mganga gani aliyehusika katika hilo na kwa watu wapi? Je ni timu au mashabiki wa timu? 

Haya ni baadhi ya maswali ambayo ni magumu mno kuyajibu. Lakini ukweli Paka alichinjwa.


2. Kijana na Bango la Bangi atolewa
Siku ya mchezo kama kawaida katika Ligi Kuu utani wa jadi baina ya Simba na Yanga kote nchini ni hali ya kawaida; kuwaona mashabiki wa timu hizo wakitambiana kwa tambo mbalimbali hata kama timu yake haichezi siku husika. 

Kijana mmoja aliyekuwa katika jukwaa la Polisi Tanzania ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliandika bango lililokuwa na maneno 'Bangi iruhusiwe..." huku akiwa ametengeneza kipande cha gazeti kilicho na mfano wa msokoto. 

Kijana huyo alikuwa akitambiana na mwenzake wa jukwaa la Yanga.

Lakini cha kustaajabisha kijana huyo alibebwa mzegamzega kwenye gari la jeshi la Polisi na kwenda kuhojiwa eti kwa kuhamasisha watu kuvuta dawa za kulevya. 

Hivi linaingia akilini kwenye michezo suala hilo. Haijulikani hadi sasa nini kinaendelea kwa kijana huyo aliyekatishwa kutazama mchezo huo.

3. Kiongozi wa soka kuiba tiketi
Suala la wizi wa tiketi limekuwa likipigiwa kelele mno na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katika mchezo huo kiongozi mmoja wa soka (jina tumelihifadhi kutovuruga uchunguzi) aliyekuwa katika geti akiruhusu watu kupita alipokuwa akipokea tiketi badala ya kuchana alikuwa anazificha kisha kwenda kuziuza kwa mara ya pili. 

Hata hivyo mamlaka zilizokuwepo zilifanya kazi nzuri na kubaini ukiukwaji kanuni za soka na sheria kwa ujumla na kumtia nguvu kwa ajili kujibu tuhuma hizo.

4. Ulinzi wa Farasi na Mbwa tafrani
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA ) limekuwa likijitahidi kusisitiza kuhusu uwepo wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viwanja vya michezo duniani. 

Pia FIFA pamoja na vyombo vyake limekuwa likiweka taratibu ya namna vyombo hivyo vinatakiwa kusimamia mchezo wa soka. 

Cha kustaajabisha ni kwamba askari wa Jeshi la Polisi walikuwa wengi katika uwanja wa Ushirika kushuhudia mchezo huo huku wakiwa katika mavazi ya kazi. 

Kama haitoshi waliingia na Farasi na mbwa wa Kijeshi pia mabomu ya machozi.

Kitendo hicho kilisikitisha sana kwani kufanya hivyo kungeweza kuleta maafa makubwa zaidi ya Mwamposa. 

Ukweli ni kwamba askari wengi walitumia kigezo cha mavazi yao na kazi yao kwa ujumla kupata nafasi ya kutazama mchezo huo. 

Halafu wenye farasi na wenyewe kwa kutaka sifa wakapita nazo pembeni ya uwanja wa kuchezea mpira kwa kasi. 

Kisaikolojia wachezaji na mashabiki wa soka walikuwa katika wakati mgumu kutambua kuwa ile ni burudani au ni ujio wa kiongozi wa kisiasa katika kufanya uzinduzi wa jambo fulani la kitaifa au kimataifa.

Sheria za soka katika ulinzi zimekaaje? Askari Polisi wanazifahamu? au ndio kiburi kutokana na idadi kubwa ya watanzania wapenda soka kutojua haki na wajibu wao?

5. Watu kupanda miti na kuta za Uwanja
Wapenzi na mashabiki wa soka walionekana kwenye miti inayozunguka Uwanja huo wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi na wengine walipanda kabisa katika kuta za uwanja huo kushuhudia mchezo huo. 

Swali la kujiuliza, hivi ingetokea wangeanguka na kupoteza maisha tungeuambia nini ulimwengu kuhusu maafa hayo ya kizembe? 

Askari Polisi walio wengi walikuwa ndani wanatazama  mchezo huo na farasi na mbwa zao. 
Awali walijaribu kuwatoa lakini kwasababu ya kuipenda zaidi mechi hiyo badala ya kudhibiti mihemko yao wakiwa kazini; wale mashabiki walirudi tena kwenye matawi ya miti kama Tarzan.
Charles Boniface Mkwasa

Malale Hamsini

6. Wanahabari Kilimanjaro njiapanda
Hapa ilikuwa changamoto hususani kwa wanahabari wa mkoa wa Kilimanjaro. 

Kiukweli ni kwamba waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro walio wengi sio waandishi wa habari za michezo na burudani walio wengi wemejikita katika masuala mengine. 

Sasa usumbufu uliojitokeza hapo ni kwa wale wasiojua kwa kina mchezo wa soka kufikiri kuwa wataingia tu kama wanavyoingia katika maeneo mengine hususani wale wenye mapenzi motomoto na timu hizi kubwa Simba na Yanga. 

Lakini kama haitoshi wakati wa kuchukua habari zenyewe hawajui nani ni nani; kwa kiasi fulani ilisikitisha mno. 

Wadau wa soka mkoani Kilimanjaro wamekuwa na tabia ya kulaumu kuwa kwanini habari nyingi za michezo mkoani Kilimanjaro sio za viwango lakini ukweli ndio huo kuwa wengi sio wabobezi katika michezo na burudani hususani soka. 

Katika hili ningeomba mamlaka husika ziwe zinafika mikoani kutoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu michezo yao hususani soka na isiwe Dar es Salaam pekee ili kuondoa usumbufu na hii itasaidia kuinua soka katika mkoa na taifa kwa ujumla.

Imetayarishwa na Jabir Johnson kwa maoni na ushauri +255 768 096 793 au baruapepe: jabirjohnson2020@gmail.com





Unaikumbuka siku ya kwanza ya Roberto Carlos kuitumikia Brazil?


Februari 26, 1992 mlinzi wa kushoto wa Brazil Roberto Carlos aliiitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa kwenye mchezo wa kirafiki ambao Seleccao walishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Marekani.

Baada ya hapo alicheza jumla ya mechi 125 akiwa na Seleccao na kushika nafasi ya pili kwa kuwa mchezaji aliyehudumu na miamba hiyo kwa kucheza mechi nyingi.

Aliitwa katika kikosi hicho akiwa na umri wa miaka 18 wakati huo ndiyo kwanza alikuwa ameanza safari yake ya soka katika medani ya kimataifa akiwa na klabu ya Serie B ya União São João miaka miwili kabla.

Kuitwa kwa nyota huyo kuliwastaajabisha wengi, lakini Kocha wa wakati huo Carlos Alberto Parreira ambaye alikuwa ametoka kuchukua wadhifa wa kuiongoza miamba hiyo alikuwa akitaka damu mpya ya vijana katika kikosi.

Hatua hiyo aliifikia kutokana na matokeo mabaya kwenye Kombe la Dunia mnamo mwaka 1990.
Mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Marekani ulichezwa katika mji wa nyumbani kwa nyota huyo wa Fortaleza.

Hakika Roberto Carlos alionyesha kuwa sio wa mchezo mchezo akiisaidia Brazil kutoruhusu wavu wake kutikiswa dhidi ya Wamarekani hao.

Zaidi sana mlinzi mwenzake Antonio Carlos alitupia bao la tatu akipokea pasi murua ya kiungo Rai na kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0.

Hata hivyo Carlos alikosa fainali za Kombe la Dunia mnamo mwaka 1994 na alikuwa miongoni mwa waliochaguliwa katika kikosi bora cha Kombe la Dunia mwaka 1998 na 2002. 

Mnamo mwaka 2002 akiwa na Brazil alifanikiwa kutwaa taji hilo.

Mchezo wake wa mwisho katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil ilikuwa ni Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani, ambako walitolewa katika robo fainali na Ufaransa.



MAKTABA YA JAIZMELA: Earl Lloyd ni nani?

Alhamisi ya Februari 26, 2015 alifariki mchezaji wa kikapu na wa kwanza Mmarekani Mweusi kucheza Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani Earl Lloyd. 

Nyota huyo alifariki akiwa na umri wa miaka 86. 

Lloyd aliweka rekodi hiyo katika historia ya NBA mnamo mwaka 1950 akiwa na Washington Capitals ikiwa ni kabla ya marafiki wenzake weusi Sweetwater Clifton na Chuck Cooper nao kuweka rekodi hiyo. 

Rais wa West Virginia wakati huo Brian Hemphill alisema familia nzima ya West Virginia inaomboleza kuondokewa na nyota huyo ambaye alikuwa mshinda ndani na nje ya Uwanja.

Hemphill alikaririwa  akisema wakati Llyod alipokuwa akiingia mwaka ule wa 1950 alifungua njia ya usawa katika taifa la Marekani.

Lloyd aliisaidia Sycrause Nationals kutwaa taji la NBA mwaka 1955 akiungana na mchezaji mwingine mweusi Jim Tucker kucheza.   

Lloyd alikuwa na kimo cha futi 6 na inchi tano akiwa na wastani wa kufunga pointi 8.4 na wastani wa rebaundi 6.4 na mechi akali ya 560.

Aliukosa msimu 1951 na 1952 kutokana na kwamba wakati huo alikuwa akilitumikia jeshi la Marekani.

Katika medani ya kikapu kuna wakti aliwahi kumsaidia kutafuta kikosi kocha Bailey Howell hapo ndipo alipopata fursa ya kubaini vipaji vya nyota Willis Reed, Earl Monroe, Ray Scott na Wally Jones.

Pia nyota huo wa kikapu aliwahi kuwa kocha wa Detroit mwaka 1971 -1972 na pia alisimamia kikosi cha Pistons kwa mechi tisa za kwanza za msimu wa 1972-1973 na baada ya hapo alitimuliwa kutokana na matokeo mabaya akiwa na rekodi ya kushinda mechi 22 kati ya 55.

Mnamo mwaka 2003 aliingizwa katika Jumba la Wakongwe wa Kikapu kutokana na mchango wake katika mchezo huo.

Alizaliwa Alexandria huko Virginia lakini alikuwa akiishi Crossville huko Tennessee.
Lloyd alizaliwa Aprili 3, 1928 kwa wazazi Theodore Llyod Sr. na Daisy Lloyd. 

Baba yake alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha makaa ya mawe na mama yake alikuwa ni mama wa nyumbani. Alipata elimu yake kwa taabu kutokana na ubaguzi wa rangi uliokuwa umeshamiri nchini Marekani.

Hata hivyo alipita vigingi vyote na kufika high school ambako alitajwa katika kikosi cha All-Soutj Atlantic Conference mara tatu pia mara mbili aliitwa katika kikosi cha kikapu cha All-State Virginia.

Kuna wakati Lloyd aliwashukuru familia yake na walimu waliomsaidia kupita katika vipindi vigumu wakati wa masomo yake hadi kufikia mafanikio hayo.



Hosni Mubarak is no more

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amefariki dunia jijini Cairo akiwa na umri wa miaka 91 katika hospitali ya kijeshi ya Al-Galaa.

Hosni Mubarak alikuwa kiongozi wa Misri ambaye kwa karibu miaka 30 alikuwa nembo ya uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati kabla kulazimishwa na jeshi kujiuzulu. 

Alilazimishwa kufanya hivyo kufuatia siku 18 za maandamano ya nchi nzima yaliyokuwa sehemu ya vuguvugu la mapinduzi ya msimu wa mapukutiko katika nchi za kiarabu mnamo mwaka 2011.

Televisheni ya taifa imetangaza kuwa Mubarak amefariki akiwa na umri wa miaka 91. 

Muda wote wa utawala wake, alikuwa mshirika wa karibu wa Marekani, akipambana vikali dhidi ya uasi wa makundi ya itikadi kali za kiislamu na mlinzi wa mkataba wa amani kati ya Misri na Israel. 

Maelfu na maelfu ya Wamisri vijana waliandamana kwa siku 18 katika barabarani katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo na kwingineko mwaka 2011.

Hosni Mubarak alizaliwa Mei 4, 1928 huko Kafr Al Musaylhah.

Tuesday, February 25, 2020

Unaikumbuka Liverpool iliyotwaa Kombe la Ligi 2001?

February 25, 2001 katika Kombe la Ligi nchini England Liverpool na Birmingham City zilikutana katika fainali kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Millenium jijini Cardiff.

Fainali hiyo ilikuwa ikiweka rekodi ya kuwa fainali ya 41 ya michuano hiyo  ambayo hushirikisha timu 92 zikiwamo za Ligi Kuu na zile za madaraja ya chini.

Liverpool ambao waliibuka mabingwa katika fainali hizo walikuwa wakiingia katika fainali ya nane wakiwa wameshinda sita na kuzikosa mbili. 

Wakati Birmingham ilikuwa ni fainali yake ya pili ya Kombe la Ligi. Katika fainali yake ya kwanza ambayo ilikuwa mwaka 1963 ambayo walipoteza mbele ya Aston Villa.

Birmingham walikuwa tayari wameshacheza mizunguko miwili zaidi ya Liverpool ambao walikuwa wamecheza mzunguko wa kwanza na wa pili. 

Hivyo basi Birmingham ilisonga mbele ikiwa imecheza mizunguko sita kufika katika fainali hizo huku Liverpool ikiwa imecheza mizunguko minne.

Katika mechi zote za mechi ilizocheza Liverpool zikiwa mteremko lakini sio dhidi ya Birmingham. Liverpool ilikuwa ikipata ushindi wa sio chini ya mabao matatu, isipokuwa dhidi ya Chelsea ilioshinda kwa mabao 2-1 katika mzunguko wa tatu.

Dhidi ya Birmingham Liverpool ilinyakua taji hilo kwa changamoto ya mikwaju ya penanti 5-4 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare.

Siku hiyo Robbie Fowler alilichungulia lango la Birmingham City kwa mkwaju wa mbali katika dakika ya 30 ya mchezo lakini katika dakika za majeruhi Darren Purse aliisawazishia timu yake baada ya Martin O'Connor kuangushwa chini na Stephane Henchoz na baadaye dakika 30 za muda wa ziada ambao ulimalizika bila nyavu kutikiswa na mikwaju ya penati kuamua fainali hiyo.

Liverpool ilikuwa ikibeba taji la kwanza kwa miaka sita tangu ilipchukua taji kama hilo mnamo mwaka 1995.

MAKTABA YA JAIZMELA: Jersey Joe Walcott ni nani?

Februari 25, 1994 alifariki dunia mwanamasumbwi  wa Marekani Jersey Joe Walcott. 

Siku  aliyopoteza maisha ilikuwa Ijumaa, maradhi ya kisukari yalimuondoa nyota mwanamasumbwi huyo akiwa katika hospitali ya Our Lady of Lourdes Medical Center mjini Camden huko New Jersey.

Jersey Joe mtoto wa wahamiaji maskini kutoka Barbados ambaye alikulia katika umaskini huo na baadaye kuweka rekodi vitabuni kwa mchezaji mwenye umri mkubwa kushinda taji la uzito mkubwa la dunia alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Binamu yake aliyefahamika kwa jina la Richard Cream ndiye aliyethibitisha kifo cha mwanamasumbwi. 

Jina lake halisi lilikuwa Arnold Raymond Cream. Alikuwa akifahamika kutokana uimara wake kwa asili na mwanamichezo ambaye alikuwa akimaanisha katika fani yake.

Jersey Joe hakuondoka katika medani hiyo ya uzito wa juu mpaka alipotwaa taji hilo baada ya kushindw akulitwaa kwa mara nne.

Aliwahi kukaririwa mara kadhaa akisema, "I always felt in my heart that God would give it to me."

Julai 18, 1951 akiwa na umri wa miaka 37 alimtandika Ezzard Charles ambaye alikuwa amemzabua mara mbili.

Katika raundi ya saba ya pambano hilo pale Forbes Field mjini Pittsburgh alifanikiwa kuweka rekodi hiyo ambayo inaelezwa ilikuja kuvunjwa na George Foreman mnamo mwaka 1994 kwa kutwaa taji la uzito huo akiwa na umri wa miaka 45. 

Jersey Joe alifahamika sana kutokana na kumtandika mara tatu mwanamasumbwi mahiri Joe Louis. Alimtandika Desemba 5, 1947 pale Madison Square alimpomzambua kwa KO mara mbili.

Mwanamasumbwi huyo alishindana kati ya mwaka 1930 hadi 1950. Alishikilia taji la uzito wa juu katika ya mwaka 1951 hadi 1952.

Alicheza mapambano 71 akishinda 51 na kupoteza 18. Mapambano mawili ya mwisho alitandikwa vibaya sana kwa KO na Rocky Marciano Mei 15, 1953 mjini Chicago, Illinois baada ya lile lililochezwa Septemba 23, 1952 Philadelphia, Pennsylvania.

Baada ya kustaafu masumbwi Jersye Joe hakuweza kwenda mbali sana na medani hiyo akaingia katika kucheza filamu na vipindi kadhaa vya televisheni.

Alikuwa mwamuzi wa mapIgano mbalimbali baada ya kustaafu kwake lakini baada ya mkanganyiko katika pambano lililowakutanisha Muhammad Ali na Sonny Liston Februari 25, 1964 ambapo Muhammad Ali alizabuliwa katika raundi ya saba wakati huo alikuwa hajabadili jina lake la Cassius Clay. 

Pambano hilo lilipigwa pale Miami Beach, jimboni Florida baada ya hapo hakuitwa tena kuamua mapambano hayo. 

Kutoka mwaka 1971 hadi 1974 Jersey Joe  alichaguliwa kuwa polisi katika Kaunti ya Camden, New Jersey na aliweka rekodi ya kuwa Mmarekani wa kwanza mweusi kushika nafasi hiyo katika kaunti ya Camden. 

Kutoka mwaka 1975 hadi 1984 Jersey Joe alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Jimbo la New Jersey.