Novemba 14,1889 alizaliwa
Waziri Mkuu wa kwanza wa India maarufu Pandit Jawaharlal Nehru.
Mwanasiasa huyu
anakumbukwa sana katika siasa za taifa hilo kutokana na mchango wake mkubwa
katika kuipatia uhuru. Mwanaharakati huyo ndiye kitovu cha siasa za India kabla
na baada ya kupata uhuru.
Nehru aliibuka katika siasa za taifa hilo baada ya kazi nzuri ya Mahtma Gandhi. Amar Chitra Katha imemtaja Nehru kama msanifu mkuu wa taifa la India. Pia Jawaharlal Nehru amekuwa akifahamika kama Pandit Nehru kutokana na chimbuko lake katika jamii ya Kashmir Pandit.
Siku ya kuzaliwa kwake huwa inasheherekewa kote nchini India kwa watu mbalimbali wakiwamo watoto wa taifa hilo kuelezwa tabia na maisha ya Pandit Nehru.
Kwa watoto amekuwa akifahamika kama Chacha Nehru ikiwa na maana ya Mjomba Nehru. Alifariki dunia Mei 27, 1964 mjini New Delhi akiwa na umri wa miaka 74.
Nehru alianza kuwika katika siasa za India mnamo mwaka 1930 hadi kupata uhuru wa taifa hilo. Nehru aliwapenda sana maskini wa taifa hilo.
Licha ya changamoto mbalimbali hususani kushindwa katika vita ya Sino-Indian ya mwaka 1962 bado Pandit Nehru alisalia kuwa kiongozi mwenye sifa njema kwa taifa hilo.

0 Comments:
Post a Comment