Taifa hili linashika nafasi
ya 11 barani Afrika kwa ukubwa wake. Linapakana na bahari ya Atlantiki kwa
upande wa Magharibi, Sahara Magharibi kwa upande wa Kaskazini na Kaskazini
Magharibi, Algeria kwa upande wa Kaskazini Mashariki, Mali kwa upande wa
Mashariki na Kusini Mashariki na Senegal kwa upande wa Kusini Magharibi.
Jina
la Mauritania limechukuliwa kutoka katika Dola za Zamani la Waberiberi ambalo
lilikuwa likitawala eneo hilo katika Karne ya 3 K.K hadi karne ya 7 B.K Dola hilo
la Waberiberi lilikuwa likitawala hadi katika maeneo ambayo sasa yanajulikana
kama Morocco na Algeria.
Inakadiriwa asilimia 90 ya eneo la Mauritania lipo
katika Jangwa la Sahara. Hiyo ndiyo sababu idadi kubwa ya watu inaishi katika
upande wa Kusini mwa taifa hilo ambako hali ya mvua inaonekana kuwa ya juu.
Mji
mkuu wa Mauritania ni Nouakchott uliopo katika Pwani ya Bahari ya Atlantiki. Mji
huo una idadi ya watu milioni 4.4
Serikali ya taifa hilo ilipinduliwa Agosti 6, 2008 katika jaribio la
kijeshi lililofanikiwa na kumweka madarakani Jenerali Mohamed Ouad Abdel Aziz.
Aprili 16, 2009 Aziz alijiuzulu kutoka katika jeshi na kuingia katika uchaguzi
Julai 19 ambao alishinda.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson.........................Novemba 25, 2019.
0 Comments:
Post a Comment