Friday, November 15, 2019

Algeria ni taifa la namna gani?


 Algeria ni moja ya nchi inayopatikana katika bara la Afrika. 

Nchi ya Algeria inapakana na nchi ya Libya kwa upande wa mashariki, kwa upande wa kusini-mashariki inapakana na nchi ya Naija(Niger), kusini-magharibi inapaklana na nchi ya Mali, kaskazini-magharibi nchi ya Moroko na Tunia na upande wa kaskazini inapakana na bahari ya Mediterania. 

Mji mkuu wa Algeria ni Algiers. Nchi ya Algeria ina ukubwa wa maili za mraba 919,595, Sawa na kilometa za mraba 2,381,751. Kwa ukubwa huu wa eneo inaipa Algeria kuwa nchi ya Pili kwa ukubwa barani Afrika na ya kumi ulimwenguni. 

Kihistoria Algeria ilitawaliwa na kutawaliwa na chi ya Ufaransa mara baada ya Mkutano wa Berlin miaka ya 1884/1885. Na Algeria ilipata uhuru mnamo mwaka 1962. 

Kutokana vita vya mapinduzi kati ya Ufaransa na Algeria vilivyoanza mnamo miaka ya 1954 na kuisha mwaka 1962. 

Lengo la vita hivyo lilikuwa ni kumwondoa mfaransa katika ardhi ya Algeria. Wakati wa vita hivyo waalgeria walikuwa na chama chao kilichofahamika kwa jina la National Revolutionary Front (FLN). 

Asili ya nchi ya Algeria inahusiana sana na Waarabu waliotokea mashariki ya kati. Inasemekana kuwa kabla ya ujio wa Waarabu hao, kwenye ardhi ya Algeria walipata kuishi watu weusi. Watu hawo waliofahamika kama Wabantu.  

Mara baada ya ujio wa Waarabu hao, waliweza kuwakimbiza Wabantu, na wengine walibaki hapo. Wale waliobaki pale walifanikiwa kuona na kuzaa watoto. 

Waarabu hao ambao wanaakiolojia wanawaita “Beriberi” haikufahamika ni wakati gani walihamia hapo. Na walipofika hapo walianzisha mji wao walioitwa Algeier. Neno ‘algeier’ ni neno lenye maana ya Al- jazair, ikiwa na maana ya Kisiwa. 

Hivyo watu hao waliita eneo kisiwa. Lakini kuna kipindi kuanzia miaka ya 800-1200 wakazi hao wa Algeria walitawaliwa na Wafoiniki, Warumi na Wamisri kwa vipindi tofauti. Mpaka Mfaransa anaingia Algeria mnamo miaka ya 1840 taifa hilo halikufahamika kwa jina la Algeria. 

Na mara baada ya Mfaransa kukabithiwa koloni hilo miaka ya 1880/1890 ndipo ilipofahamika kwa jina la Algeria. Raisi wa kwanza alikuwa Abdirrahmane Fares(1911-1991) aliyepata kutawala chini ya chama cha National Revolutionary Front(FLN). 

Aliofanikiwa kudumu kwa miezi 2, yaani kuanzia 3 Julai 1962 hadi 25 September 1962. Baada kipindi kirefu Abdelaziz Bouteflika alishika madaraka hyo kuanzia mwaka 1999. 

Aprili 2, 2019 Bouteflika alijiuzulu ikiwa takribani miongo mwili ya kulitawala taifa hilo. Algeria ina takribani watu wapatao milioni 42.2 hivyo kuiweka kuwa nchi ya 32 kwa idadi kubwa ya watu.

Imetayarishwa na Jabir Johnson………………………………..Novemba 15, 2019

0 Comments:

Post a Comment