Agustino Lyatonga Mrema |
Mapema hivi karibuni
vyama hivyo vya upinzani vikiongozwa na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema, vilitangaza kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa,
unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka kwa madai kuwa kufanya hivyo ni
kuendeleza uonevu unaofanywa katika mchakato wa uchaguzi huo.
Dkt. Mrema
alitoa kauli hiyo jana, wakati akimnadi mgombea wa TLP anaewania nafasi
ya uenyekiti wa kijiji cha Kiraracha Andrea Lekule, ambapo alisema kususia
uchaguzi wa serikali za mitaa ni kunawanyima fursa wananchi haki ya
kuwasilishiwa mawazo yao juu ya maendeleo ya nchi.
''Kiongozi yeyote wa
kisiasa ambaye amekomaa kisiasa, hapaswi kugomea uchaguzi, anachotakiwa ni
kupambana hadi dakika ya mwisho, viongozi wenzagu wa vyama vya upinzani
waliosusia ka uchaguzi wa serikali za mitaa, viongozi hao hawafai kuwepo
kwenye nafasi hizo kwani wanawasababishia wananchi kutokupata kiongozi sahihi
atayewaletea maendeleo,”alisema Dkt. Mrema.
Aidha Dkt. Lyatonga
Mrema alisema Chama Cha TLP, kimejipanga kushinda kwenye uchaguzi
wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novema 24 mwaka, kutokana na chama
hicho kuwa na sera nzuri za kuwaambia wananchi ili waweze kukichagua.
“Mimi sitegemei huruma
za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kama ambavyo watu wamekuwa wakisema kuwa CCM
waniachie hicho kijiji, sitegemei na haiwezekani tutashindana kwenye sanduku la
kura,”alisema Dkt. Mrema.
Alifafanua kuwa Chama
Cha TLP kitaendelea na mapambano ya kumwaga sera zake kwenye mikutano ya
kumnadi mgombea wa uenyekiti na kwamba fainali yake itahitimishwa
kwenye sanduku la kura Novemba 24.
Dkt. Mrema
alisema anaamini chama chake kitaibuka ushindi na kuchukua kijiji
cha Kiraracha, kutokana na kuwa na sera ambazo vyama vingine havina,
baada ya chama hicho kubaini kwamba vyama vingine kutokuwa na sera za
kumjali mwananchi hali ambayo imewasababaisha hata wengine kujiondoa
kwenye uchaguzi huo.
“TLP kimekuja
kushindana kwa nguvu zote kwa kushirikiana na wanachama wa TLP, washabiki
wa chama changu hivyo kusema kuwa mimi nategemea huruma za CCM huko ni
kujidanganya na kuhakikishi CCM nitaigaragaza mapema kabisa,”alisema.
Akiwa katika kampeni
za kumnadi mgombea uenyekiti wa kijiji cha Kiraracha kupitia tiketi ya
CCM, Thomas Mrema, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi,
alisema ili kuendelea kumpa heshima yake Dkt. Mrema aliwataka wananchi wa
kijiji hicho kuendelea kuipigia kura CCM kwani hiyo ndiyo heshima pekee ambayo
CCM inaweza kumpa Mrema.
“Chama Cha Mapinduzi
CCM kitaendelea kumshukuru Dkt. Mrema kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akisaidia
katika kuendelea kutuunga mkono licha ya kwamba hatukuwa na mapatano na
CCM,”alisema Boisafi.
STORY BY & PHOTO BY: Kija Elias, Moshi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi. |
DATE: Novemba 21, 2019
0 Comments:
Post a Comment