Kampuni
kubwa la biashara kwa njia ya mtandao wa Internet Jumia Technologies limefunga
ofisi zake nchini Cameroon kwa kile kinachoelezwa kuwa kufanya kazi kwa hasara
katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
Taarifa
hiyo ya kutia simanzi kwenye taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika ukanda wa
Afrika wa Kati inakuja wakati kukiwa na mtafaruku baina ya jamii ya watu
wanaozungumza lugha ya Kiingereza katika mikoa iliyopo Kaskazini Magharibi na
Kusini Magharibi mwa Cameroon.
Jumia
imechukulia umaarufu katika ukanda wa Afrika kama zinavyosifika Amazon na
Alibaba kwa biashara hiyo kwa njia ya mtandao.
Taarifa
zinasema Jumia itaendelea kuwahudumia wateja wake katika taifa hilo kwa kutumia
Jumia Deals tofauti na ilivyokuwa ikitumika sasa.
Katika
taarifa yao Jumia wamesema, “ Tumefikia mwisho wa kutoa huduma zetu kutokana kwani
haifai kwa muktadha wa sasa hapa Cameroon.”
Jumia
iliyopewa jina la wateja wake ‘Amazon of Africa’ ilianzishwa mwaka
2012 na Mfaransa ambaye alikuwa mshauri wa zamani wa McKinsey na kupata
umaarufu wake kwa biashara ya mtandao barani Afrika.
CHANZO: REUTERS
0 Comments:
Post a Comment