Monday, November 4, 2019

Ujumbe wa Kuwait wazuru Djibouti



Ujumbe wa watu wane kutoka Kuwait upo nchini Djibouti tangu Jumamosi ya Novemba 2 mwaka huu ambapo leo Novemba 4, 2019 umekutana na Waziri wa Wanawake na Familia Moumina Houmed Hassan kujadili masuala mbalimbali katika kukuza diplomasia ya mataifa hayo mawili.

Imeelezwa kuwa ujumbe huyo kutoka Ghuba ya Uajemi umejadili kuhusu masuala ya mshikamano na yanayohusu jamii. 

Ujio wa ujumbe huo nchini humo sio wa bahati mbaya unafuatia ziara aliyoifanya Waziri Moumina Juni 16 hadi 18 mwaka huu nchini Kuwait. 

Waliozuru Djibouti ni Katibu Mkuu wa Wizara wa Mambo ya Kijamii wa Kuwait Abdoul-Aziz Abdoussalam Choueib, Mkurugenzi wa Masuala ya Kigeni Michari Abdoul-Aziz As-Sab, Mkurugenzi wa Taasisi za Kujitolea za nchini Kuwait Houda Saleh Rachid na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Al-Rahma Fahad Mohamed Al Chamari.   

CHANZO: La Nation

0 Comments:

Post a Comment