Sierra leone ni nchi inayopatikana magharibi mwa bara la Afrika, mji mkuu wake unaitwa Freetown ambao ndiyo mji mkubwa ukifuatiwa na mji wa Bo. Nchi hii inapakana na Guinea kwa upande wa kaskazini, upande wa kusini-mashariki inapakana na Liberia na kusini magharibi bahari ya Antlantiki. Sierra leone inaukubwa wa kilometa za mraba 71,740.
Nchi hii imegawanyika katika sehemu nne yaani, mkoa wa kaskazini, magharibi, kusini na mashariki.
Kuna makabila 16 na kila moja likiwa na lugha yake na utamaduni wake.
Lakini makabila yaliyo makubwa ni Wamende na Watemne.nchi hii ni ya kiislamu kwa asilimia 60, huku asilimia 30 ikichukuliwa na dini za kiafrika na asilimia 10 ikichukuliwa na ukristo.
Asili ya neno Sierra Leone lilitokea mnamo mwaka 1462 wakati mreno aliyejulikana kwa jina la Pedro da Cintra alipofika eneo hilo na kukuta mlima ukiwa umesimama (leo hii ni Penisula ya Freetown) , ndipo alisema kwa Kireno Serra da Leoa ikiwa na maana ya Milima ya Simba na baadaye kutamkwa Sierra Leone.
Historia inasema Sierra Leone ilipata uhuru kwenye miaka ya 1961, ambapo harakati za uhuru ziliongozwa na Milton Margai (waziri mkuu wa kwanza) kutoka katika utawala wa Uingereza. Ukweli ni kwamba Siera Leone ni moja ya nchi iliyobarikiwa kuwa na utajiri wa madini ya almasi.
Wananchi walidhani maisha yatabadilika kutokana na utajiri huo, lakini baada ya uhuru serikali haikufanya mabadiliko, kwani wananchi waliendelea kuwa maskini na asilimia kubwa ya rasilimali zilkuwa zikifaidiwa na wachache wenye madaraka, na wazungu kutoka ulaya.
Hata Wananchi waliokuwa wakichimba madini hayo walikuwa na hali mbaya, huku wakiwanufaisha wafanyabiashara kutoka nje.
Ndipo hali ilibadilika kwenye miaka ya 1980 palipoundwa kundi lililojulikana kama RUF (Revolutionary United Front) lilikuwa likipinga serikali ya Joseph Momo.
Mpaka kufikia miaka 1991 machafuko yalianza na takribani watu wengi walipoteza maisha huku wengine wakiachwa na vilema na bila kusahau wengine wakiwa wakimbizi.
RUF waliamini kuwa Serikali iliyopo madarakani ilichaguliwa na wananchi, kumbe ubovu wa serikali unasababishwa na Wanachi.
Hivyo kwa kuwa mtu anapiga kura kwa kutumia mikono, basi RUF walikuwa wakiwakata watu mikono huku wakisema “NO MORE HAND, NO MORE VOTE”.
mpaka mwaka 2002 machafuko hayo yaliisha baada ya jeshi la nchi kuingilia kati na umoja wa mataifa pia. Ndipo kukawa na mikataba ya amani.
Mpaka sasa kuna familia ni maskini, kuna familia zimepoteza watu wao, na jambo la kusikitisha machafuko hayo yalihusisha mauaji yaliyokuwa yakifanywa na watoto wadogo waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya. Lengo la RUF lilkuwa kuwakomboa wananchi na walitaka rasilimali zitumike kwa ajili ya wananchi wote.
Kwa sasa Sierra Leone ni moja ya nchi ambayo inakumbwa na janga la ugonjwa wa Ebola.
Imetayarishwa na Jabir Johnson..........................Novemba 27, 2019.
0 Comments:
Post a Comment