Novemba
30, 1874 alizaliwa mwanasiasa, mwanajeshi na mwandishi wa vitabu wa Uingereza
Winston Churchill.
Alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1940 na 1945
ambaye alitoa mchango mkubwa wa taifa lake kushinda katika Vita vya Pili vya
Dunia.
Pia alikuja kushika wadhifa huo tena kwa mara ya pili mnamo mwaka 1951
hadi 1955.
Katika kipindi chote cha uhai wake, muda wake mwingi aliutumia
kwenye uongozi na uandishi, alipata nafasi za uongozi kwenye ngazi mbalimbali
kwa miaka 55 (tangu mwaka 1900 mpaka 1955, akiwa mbunge kwa kipindi chote,
waziri kwa miaka 31 na waziri mkuu kwa miaka 9) na pia aliweza kuandika vitabu
zaidi ya 40.
0 Comments:
Post a Comment