Hili ni taifa lililopo
katika Pembe ya Afrika. Limepakana na Eritrea kwa upande wa Kaskazini,
Ethiopia kwa upande wa Magharibi na Kusini.
Pia linapakana kwa upande wa Kusini
Mashariki na Somalia.Mpaka mwingine uliosalia ni ule wa Bahari ya Shamu na
Ghuba ya Aden kwa upande wa Mashariki. Djibouti inachukua eneo la ukubwa wa
Kilometa za mraba 23,200.
Taifa hili linakaliwa na makabia mawili ya asili
ambayo ni Wasomali na WaAfar.
Pamoja na Somalia, Taifa hili lilikuwa ni
miongoni mwa taifa katika ardhi ya Punt.
Mwishoni mwa karne ya 19 mikataba
iliingiwa baina ya Wafaransa na sultani wa Somali na Afar.
Pia taifa hilo ni
taifa lenye watu kutokana mataifa mbalimbali wanaokaridiwa kufikia laki nane.
Idadi hiyo inalifanya kuwa taifa lenye idadi ndogo ya watu barani Afrika kwa
nchi zilizopo katika ardhi.
Lugha mbili zinazungumzwa katika taifa hili ambazo
ni Kifaransa na Kiarabu. Ukoo wa Issa ambao sasa unatambulikama kama wa
Kisomali na ule wa Afar ndio umelifanya taifa hilo kuwa na makabila makubwa mawili.
Yote mawili yanazungumza lugha ya Kikushi
ikiwa ni sehemu ya lugha zenye asili ya Afrika na Asia.
Taifa hili limekuwa ni
mahali pa majeshi ya majini kutoka mataifa makubwa.
Pia Djibouti imekuwa mahiri
duniani kutokana na meli ambazo zimekuwa zikipita hapo zikitoka Bahari ya Shamu
na kwenda Bahari ya Hindi.
Pia imekuwa ni eneo zuri kwa meli kujaza mafuta na
kusafarisha bidhaa kutoka nchi jirani ya Ethiopia. Mji mkuu wa taifa hilo ni
Djibouti City.
Imetayarishwa na Jabir
Johnson………………………….Novemba 4, 2019.
0 Comments:
Post a Comment