Bunge jipya la Tunisia jana
Jumatano limemchagua Rached Ghannouchi wa chama cha Kiislamu cha Ennahdha kuwa
spika wa bunge hilo baada ya kuuungwa mkono na mahasimu wake wa Chama cha Heart
of Tunisia.
Hatua hiyo muhimu kwa taifa hilo inaifanya kuingia katika serikali
ya muungano. Katika uchaguzi wa mwezi uliopita chama hicho cha Ennahdha kilijinyakulia
nafasi 52 pekee kati ya 217 hali iliyowalazimisha kuingia katika muungano na mahasimu ili kujishindia nafasi ya
kuongoza bunge hilo.
Hata hivyo uwezekano wa kuunda serikali ya muungano
unaweza kushindika nchini humo kwani serikali inaweza kuendelea kuwa mikononi
mwa Waziri Mkuu Youssef Chahed.
Uchaguzi
wa jana Jumatano ulikuwa ni mtihani mkubwa na muhimu kwa Ennahdha kutokana na kwamba
kabla ya hapo chama hicho kilifutwa mnamo mwaka 2011.
Tangu wakati huo Ennahdha
kimekuwa katika muungano wa serikali mbalimbali.
Ghannouchi anashika madaraka
hayo baada ya kurudi kutoka uhamishoni nchini Uingereza kutokana na mapinduzi ya
mwaka 2011.
Mwanasheria wa chama cha Heart of Tunisia Ridha Charfeddine amesema chama chao kilimpigia kura Ghannouchi
wa Ennahda baada ya makubaliano. Kiongozi wa chama cha Heart of Tunisia Nabil
Karoui sasa anatakuwa katika serikali ya muungano na Ennandha.
0 Comments:
Post a Comment